MALCOM LUMUMBA
JF-Expert Member
- Jul 26, 2012
- 21,113
- 65,124
Vita ya Kagera ilikuwa ni ufunguo wa mambo mengi sana kwenye huu ukanda wetu. Pengine kama Iddi Amin angeshinda sidhani kama tungekuwa hali ya leo ingeendelea kuwepo: Tungekuwa na Afrika Mashariki ya tofauti sana, nzuri au mbaya hilo mimi silifahamu.
Lakini ni nadharia yangu kwamba kama ile vita ya mwaka 1979 Tanzania ingeshindwa basi, sidhani kama leo huu ndugu Yoweri Kaguta Musseveni angekuwa Rais wa Uganda wala ndugu Paul Kageme angekuwa Rais wa Rwanda. Hii ni kwasababu mwaka 1972 wakiwa peke yao, waasi wa Uganda walijaribu kumvamia Iddi Amin lakini walipigwa vibaya mno, walifanikiwa pale tu walipoungwa mkono na vikosi vya Tanzania mwaka 1979.
Ile vita iliwajenga kwa kiwango kikubwa sana kijeshi vijana na wanaharakati wa Kitutsi ambao walikuwa wanaishi uhamishoni aidha huko Uganda, Kenya na Tanzania. Wengi wao walipatia mafunzo ya kijeshi Tanzania na kusoma hapa Tanzania kwa pesa za watanzania: Baada ya vita kuisha walipoitwa Waganda wote mashuhuri duniani kule Arusha ili wafanye kikao cha nani aongoze nchi baada ya Iddi Amin, pesa, ushauri na utaalamu wa Watanzania vilitumika pia.
Museveni anakuwa Raisi wa Uganda miaka michache ya mbele na haya yanatokea:
1. Museveni anasaidia kuunda RPA
2. RPF inaanza kupigana na Hyabarimana
3. RPF inaingia Rwanda na kutawala
4. Uganda na Rwanda wanavamia Zaire
Yametokea mengi sana, lakini swali ninalojiuliza ni kwamba: Je, haya yangetokea kama Tanzania ingeshindwa Vita ya Kagera?
Je, Uganda na Watutsi waliokuwa uhamishoni wangeweza kuwa hapa walipo leo bila Tanzania kushinda ile vita?
Je, Tanzania tulikosea kuwasaidia hawa ndugu zetu, hasahasa baada ya kuona mambo ya ajabu wanayoyafanya kule Congo DRC, na kwingineko?