Kama Tanzania ingeshindwa vita ya Kagera: Je, Rwanda na Uganda zingefika hapa zilipofika leo?

Ndugu yangu Malcom Lumumba,

Pamoja na mambo mengine, umetaja yale yaliyotokea baada ya Museveni kuingia madarakani, kisha ukahoji:-
Kwanza, mimi naomba nianze na Museveni mwenyewe!

Je, Museveni alipiga kambi Tanzania ili kuvuta nguvu ya kumuondoa Iddi Amin madarakani au alipiga kambi Tanzania kuvuta nguvu ili hatimae yeye aingie madarakani?

Mwanzoni ilikuwa rahisi sana kuamini pasipo na shaka kwamba alipiga kambi Tanzania ili kuondoa utawala kandamizi wa Iddi Amin! Na kwavile tayari Mwalimu alishakuwa against Amin, kwake Museveni ilikuwa ni rahisi sana kuuzika kwa zana ya kutaka kuuondoa utawala wa Amin!

Tanzania ikaingia vitani na Uganda, huku ikishirikiana na wafuasi wa Obotte pamoja na Museveni! Iddi Amin akang'olewa madarakani, na baada ya hili na lile, hatimae uchaguzi unafanyika Uganda unaorudisha tena Obotte madarakani!

Historia inatukumbusha kwamba, muda mfupi Obotte anagoma kukubaliana na matokeo ya uchaguzi kwa hoja zile zile ambazo hadi karne ya 21 bado zinaendelea kutamalaki Afrika... kwamba uchaguzi uliomwingiza Obotte madarakani ulijaa udanganyifu!

Kufuatia tuhuma hizo, Museveni akishirikiana na akina Fred Rwigyema bila kumsahau PK hatimae wanaingia msituni kupambana na serikali ya Obotte!

Hapo ndipo msingi wa swali langu kwamba Museveni alipiga kambi Tanzania ili kumuondoa Dikteta Iddi Amin au ili aingie madarakani?! Na hapa tukumbuke kwamba, pamoja na Museven kupiga kambi Tanzania, pia alishakuwa na uzoefu wa kivita aliyokuwa anapigana huko Msumbiji!

Kwa maoni yangu, Museven hakupiga kambi Tanzania ili kumuondoa Amin bali alipiga kambi Tanzania ili kuhakikisha anaiongoza Uganda "no matter what!" Madai yake kwamba uchaguzi ulijaa fraud ni bullshit kwa sababu, tangu aingie madarakani hata mwenyewe hakuwahi kufanya uchaguzi usio na mizengwe hata hii karne ya 21!

Ninachotaka kusema ni kwamba, endapo Tanzania ingeshindwa vita ile bado isingekuwa ndo mwisho wa Museven kutaka kuitawala Uganda!

Na kushindwa kwa Tanzania kungetengeneza " a More Aggressive and Notorious Idd Amin!" Huyu More and Aggressive Iddi Amin angetengeneza wimbi jipya la Wakimbizi wa Uganda ambao majority kama ilivyokuwa wale wa awali ambao ni wafuasi wa Obotte, hawa nao wangeingia Tanzania na kujiunga na Waasi chini ya Museven!

Wimbi hili bila shaka lingehusisha na Wanywaranda waliokuwa Uganda ambao nao walipigana bega kwa bega na Museven ili kumuondoa Obotte madarakani!

Kwa kuangalia hilo, it's a matter of time kabla Museven na wafuasi wake hawajarudi tena Uganda kama ambavyo wafuasi wa Obotte walivyofanya majaribio kadhaa ya kuingia Uganda kumpiga Iddi Amin ili kumrudisha Obotte madarakani... nazungumzia matukio ya kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!

Hata hivyo, kushindwa kwa Tanzania huenda kungefanya Kagera kusipitike tena! Sasa wangepitia wapi?! Tayari hapa tuna Waasi wa Uganda na Waasi wenye asili ya Rwanda!

Pia tusisahau nchini kwetu tulikuwa na "muasi" mwingine anayeenda kwa jina la Laurent Kabila wa Zaire!

Tukiacha upande wa Mashariki na Kaskazini ya Uganda, Uganda pia ingeingilika ama kupitia Tanzania, Rwanda au Zaire!!

Kwa maana nyingine, it's also a matter of time kabla ya huu "Utatu Mtakatifu" wa Museven, PK na Kabila haujapanga uanzie wapi! Kwamba, walianzishe Rwanda ili wapate " a playing ground" kama ambavyo PK alivyokuwa ameipata Uganda as a playing ground, au waanzie Kivu kama njia ya kuingia Uganda!

Aidha kushindwa kwa Tanzania huenda kungesababisha tu kutoendesha tena "all-out war" dhidi ya Amin lakini huenda kungetengeneza " a Covert Army" ambayo inge-team up na akina Museven dhidi ya Amin!!

Na kama nilivyosema, Waasi Uganda wangeongezeka, Iddi Amin kiburi kingeongezeka, Ushenzi wa Amin kwa raia wa Uganda hususani wale wa kabila la akina Museven na Obotte ungeozeka, na matokeo yake, huenda Amin angekuwa na maadui wengi zaidi ambao ni Waganda kuliko ilivyokuwa kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!

Na kutokana na hayo, sioni ni namna gani Amin angeweza kufika in 1990's kabla hajafurumushwa!

Hapa ninachoona ni kama ile miaka 6 ya Uganda's Bush war iliyomwingiza Museven madarakani dhidi ya wafuasi wa Obotte, ingekuwa ni miaka ya kumuondoa Amin madarakani baada ya Tanzania kushindwa!

Kwa maana nyingine, haya ya sasa ya akina Kagame yangechelewa tu lakini yangetokea!

Swali lako la pili kwamba:-Kwa maoni yangu, YES, wangekuwapo, kwa kuangalia niliyoeleza hapo juu! Na kwamba:-Hapa naomba niwe makini kidogo ili nisihamishe mjadala! Nitaongea kwa uchache sana kwa hofu ile ile ya kuhamisha mjadala... Tanzania hatupo innocent kutokana na Vita vya Uganda!

By 1979 Tanzania ilikuwa LAZIMA iingie vitani dhidi ya Amin lakini ukiangalia matukio tangia kuondolewa Obotte madarakani na Iddi Amin, Tanzania tukaanza kuitengeneza ile vita "in favor of our beloved Obotte"!

Tukam-proveke Kichaa Iddi Amin, nae akaitikia provocation yetu!!

Hivyo basi, hatukuwasaidia, bali ile vita ilikuwa ni ya kwetu wenyewe! Museven nae akatumia fursa kuonesha lengo lake ni kumuondoa Kichaa Iddi Amin kumbe alikuwa anatutumia tu ili aende kuitawala Uganda!!

Mwalimu alishindwa kuliona hili kwa sababu akili yake yote ilikuwa dhidi ya Amin! Na kama alishaliona lakini akasimamia nadharia ya "adui wa adui yako ni rafiki", well and good.
Mimi huwa nasemaga kila siku kwamba utakapotangaza nia ya Uraisi wa JMT mimi ntajitolea kupiga kampeni kuanzia Masasi hadi Muleba hata kwa mguu!

Braza umetisha sana na umechambua vizuri mno na hili ndilo jibu nililokuwa nalitafuta hapa. Ambacho mimi huwa kinanifanya nifikirie ni kuhusu Mzee Nyerere, hivi hadi wakina Museveni na Kagame wanaanza kufanya vurugu kule Uganda ina maana Tanzania hatukufikiri hata kidogo?

Maana ukiangalia matukio ya Afrika Mashariki hadi kufika mwaka 1998 Tanzania ilikuwa inayafuatilia kwa umakini sana. Kama unakumbuka wakati mauaji yanatokea Rwanda kulitokea mvutano mkubwa sana baina ya Mzee Nyerere na Mwinyi ambapo alitaka Tanzania ifanye kitu na kuita hadi waandishi wa habari lakini Mzee Mwinyi akafunga vioo vyote na kuweka mziki mkubwa. Sijui kwanini ilikuwa iko vile lakini inaleta sana maswali.

Upande mwingine, wakina Kabila, Museveni na Kagame walivyomtoa Mobuthu kule Zaire mwaka 1997 Mzee Nyerere alionekana kufurahishwa sana na kile kitendo na baada ya lile tukio akaenda kabisa kutoa muhadhara kwa uongozi mpya kwamba "Zaire haina wajomba watakaoiletea maendeleo".

Ina maana Nyerere alikuwa hana ufahamu wowote juu ya tabia za hawa jamaa wawili ambao amekaa nao tokea vita za Msumbiji, Uganda na Rwanda kwa wakati wote huo? Mara nyingi alikuwa akienda kwenye mikutano mikubwa alikuwa akijisifia sana kumtoa Mobuthu na unaona kabisa alikuwa anawafahamu Museveni na Kagame vizuri.

Kaka Chige kuna baadhi ya mambo huwa yanaacha maswali mengi sana yenye ukakasi kuliko majibu yenye kueleweka!
 
Ndugu yangu Malcom Lumumba,

Pamoja na mambo mengine, umetaja yale yaliyotokea baada ya Museveni kuingia madarakani, kisha ukahoji:-
Kwanza, mimi naomba nianze na Museveni mwenyewe!

Je, Museveni alipiga kambi Tanzania ili kuvuta nguvu ya kumuondoa Iddi Amin madarakani au alipiga kambi Tanzania kuvuta nguvu ili hatimae yeye aingie madarakani?

Mwanzoni ilikuwa rahisi sana kuamini pasipo na shaka kwamba alipiga kambi Tanzania ili kuondoa utawala kandamizi wa Iddi Amin! Na kwavile tayari Mwalimu alishakuwa against Amin, kwake Museveni ilikuwa ni rahisi sana kuuzika kwa zana ya kutaka kuuondoa utawala wa Amin!

Tanzania ikaingia vitani na Uganda, huku ikishirikiana na wafuasi wa Obotte pamoja na Museveni! Iddi Amin akang'olewa madarakani, na baada ya hili na lile, hatimae uchaguzi unafanyika Uganda unaorudisha tena Obotte madarakani!

Historia inatukumbusha kwamba, muda mfupi Obotte anagoma kukubaliana na matokeo ya uchaguzi kwa hoja zile zile ambazo hadi karne ya 21 bado zinaendelea kutamalaki Afrika... kwamba uchaguzi uliomwingiza Obotte madarakani ulijaa udanganyifu!

Kufuatia tuhuma hizo, Museveni akishirikiana na akina Fred Rwigyema bila kumsahau PK hatimae wanaingia msituni kupambana na serikali ya Obotte!

Hapo ndipo msingi wa swali langu kwamba Museveni alipiga kambi Tanzania ili kumuondoa Dikteta Iddi Amin au ili aingie madarakani?! Na hapa tukumbuke kwamba, pamoja na Museven kupiga kambi Tanzania, pia alishakuwa na uzoefu wa kivita aliyokuwa anapigana huko Msumbiji!

Kwa maoni yangu, Museven hakupiga kambi Tanzania ili kumuondoa Amin bali alipiga kambi Tanzania ili kuhakikisha anaiongoza Uganda "no matter what!" Madai yake kwamba uchaguzi ulijaa fraud ni bullshit kwa sababu, tangu aingie madarakani hata mwenyewe hakuwahi kufanya uchaguzi usio na mizengwe hata hii karne ya 21!

Ninachotaka kusema ni kwamba, endapo Tanzania ingeshindwa vita ile bado isingekuwa ndo mwisho wa Museven kutaka kuitawala Uganda!

Na kushindwa kwa Tanzania kungetengeneza " a More Aggressive and Notorious Idd Amin!" Huyu More and Aggressive Iddi Amin angetengeneza wimbi jipya la Wakimbizi wa Uganda ambao majority kama ilivyokuwa wale wa awali ambao ni wafuasi wa Obotte, hawa nao wangeingia Tanzania na kujiunga na Waasi chini ya Museven!

Wimbi hili bila shaka lingehusisha na Wanywaranda waliokuwa Uganda ambao nao walipigana bega kwa bega na Museven ili kumuondoa Obotte madarakani!

Kwa kuangalia hilo, it's a matter of time kabla Museven na wafuasi wake hawajarudi tena Uganda kama ambavyo wafuasi wa Obotte walivyofanya majaribio kadhaa ya kuingia Uganda kumpiga Iddi Amin ili kumrudisha Obotte madarakani... nazungumzia matukio ya kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!

Hata hivyo, kushindwa kwa Tanzania huenda kungefanya Kagera kusipitike tena! Sasa wangepitia wapi?! Tayari hapa tuna Waasi wa Uganda na Waasi wenye asili ya Rwanda!

Pia tusisahau nchini kwetu tulikuwa na "muasi" mwingine anayeenda kwa jina la Laurent Kabila wa Zaire!

Tukiacha upande wa Mashariki na Kaskazini ya Uganda, Uganda pia ingeingilika ama kupitia Tanzania, Rwanda au Zaire!!

Kwa maana nyingine, it's also a matter of time kabla ya huu "Utatu Mtakatifu" wa Museven, PK na Kabila haujapanga uanzie wapi! Kwamba, walianzishe Rwanda ili wapate " a playing ground" kama ambavyo PK alivyokuwa ameipata Uganda as a playing ground, au waanzie Kivu kama njia ya kuingia Uganda!

Aidha kushindwa kwa Tanzania huenda kungesababisha tu kutoendesha tena "all-out war" dhidi ya Amin lakini huenda kungetengeneza " a Covert Army" ambayo inge-team up na akina Museven dhidi ya Amin!!

Na kama nilivyosema, Waasi Uganda wangeongezeka, Iddi Amin kiburi kingeongezeka, Ushenzi wa Amin kwa raia wa Uganda hususani wale wa kabila la akina Museven na Obotte ungeozeka, na matokeo yake, huenda Amin angekuwa na maadui wengi zaidi ambao ni Waganda kuliko ilivyokuwa kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!

Na kutokana na hayo, sioni ni namna gani Amin angeweza kufika in 1990's kabla hajafurumushwa!

Hapa ninachoona ni kama ile miaka 6 ya Uganda's Bush war iliyomwingiza Museven madarakani dhidi ya wafuasi wa Obotte, ingekuwa ni miaka ya kumuondoa Amin madarakani baada ya Tanzania kushindwa!

Kwa maana nyingine, haya ya sasa ya akina Kagame yangechelewa tu lakini yangetokea!

Swali lako la pili kwamba:-Kwa maoni yangu, YES, wangekuwapo, kwa kuangalia niliyoeleza hapo juu! Na kwamba:-Hapa naomba niwe makini kidogo ili nisihamishe mjadala! Nitaongea kwa uchache sana kwa hofu ile ile ya kuhamisha mjadala... Tanzania hatupo innocent kutokana na Vita vya Uganda!

By 1979 Tanzania ilikuwa LAZIMA iingie vitani dhidi ya Amin lakini ukiangalia matukio tangia kuondolewa Obotte madarakani na Iddi Amin, Tanzania tukaanza kuitengeneza ile vita "in favor of our beloved Obotte"!

Tukam-proveke Kichaa Iddi Amin, nae akaitikia provocation yetu!!

Hivyo basi, hatukuwasaidia, bali ile vita ilikuwa ni ya kwetu wenyewe! Museven nae akatumia fursa kuonesha lengo lake ni kumuondoa Kichaa Iddi Amin kumbe alikuwa anatutumia tu ili aende kuitawala Uganda!!

Mwalimu alishindwa kuliona hili kwa sababu akili yake yote ilikuwa dhidi ya Amin! Na kama alishaliona lakini akasimamia nadharia ya "adui wa adui yako ni rafiki", well and good.
This is deep!
Narudia kusoma mara mbilimbili hili bandiko. Braza wewe una akili nyingi sana.
 
Sikuwahi kuwaza kama ushindi wa Tanzania kwenye vita vya Kagera ulikuwa na faida kubwa sana ya kisiasa kwa Rwanda na hasa mpaka kumpata huyu raisi wao wa sasa.

Ngoja niendelee kufyonza matarials hapa....
 
Mkuu wa afrika kazi tunayo ila kwa sasa hizo vitu hazito wezekana ila shida iliyopo KUBWA waafrika watawala wajidai kupendelea makabila yao ktk kuwapa nyazifa nzuri serikalini na kuwaacha makabila au jamii nyngine wasindikizaji kitu ambacho mwsho wasiku mtawala hyo akitoka anaacha moto kwa waliobaki

Hapo kuna kuangalia kwanini mpaka miaka hii Rais wa nchi ya Africa anapendelea zaidi watu wake kushika nyadhifa nyingi (zote?) muhimu serikalini na impact yake ni nini kwa nchi husika kwa muda huo au baadae.

Ni mambo mengi hapa ya kuongelea. Labda ingeanzishwa Uzi wake.

Lakin kuna hii historia, ambayo hata baada ya miaka 50 au 60 bado haijatuacha salama. Mbelgiji mmoja akiielezea Kongo miaka ile alisema ile si nchi Ila a bunch of tribes. Mkusanyiko Fulani wa makabila. Na yasiyo na umoja wa aina yoyote.

Wazungu walipotutawala walijaribu kututenganisha kwa dhati. Wakiona dini haiko effective walitumia ukabila/ ukanda. Hilo lisipofanya kazi walihamia kwenye kimo, umbo LA pua na nk kama kwa ndugu zetu Rwanda, Burundi. Tofauti zetu ziliimarishwa zaidi ya ufanano wetu. Hili linatutesa mpaka leo. Na kwa baadhi ya nchi hili ndio chanzo cha mitafaruku isiyoisha
 
Ukweli ni kuwa hatukuwa na ifahamu wa HIMA EMPIRE. Mwalimu alifanya kama Mwafrika kwa ajili ya Afrika dhidi Uovu wa Mwafrika. Kwa kutojua au kutotilia maanani dhana ya HIMA EMPIRE tukawaacha Watutsi ku~dominate Majeshi ya ukombozi wa Uganda. Tulifanyakosa acha tulipe gharama.

Tusuipokuwa makini, Watutsi watatumaliza. Kwanza kwa kutegemea UZURI & UREMBO wa wanawake wao, wanaolewa au kuzaa na Viongozi wetu. Lengo lao ni kuwa na watu wanaoweza remotely control them. Wakati mwingine hawazai nao bali huzaa na watutsi wenzao ma kwa kuwa kitanda hakizai haramu; huhesabiwa kuwa ni Watanzania. Pia wanajipenyeza na kudai ni Watanzania toka kabila la Wanyambo, Wahaya, Wanyiramba/Wanyaturu na Wachaga (Machame). Pia majina ya kwao ama wanayaacha au kuyageuza yafanane na kwetu. Mbinu inawasaidia sana kwani sisi sio wadadisi sana kuhusu ukabila.

Aidha wana~wanausalama wa taifa wa kutosha ktk miji ya Dar, Dodoma, Arusha na labda Mbeya. Wanafanyakazi dhalili na.za hovyo kama kuuza matunda au barmaid. Lengo ni kuwafuatilia wanasiasa na watu wenye ushawishi ktk jamii na kutengeneza urafiki wenye maslahi kwao. Kwa Dar watu nendeni Seblen Pub muone wahudumu na wateja ni kina nani: Mtaniambia.

Uzuri ni kuwa; Linchi hili ni likubwa sana hivyo wanashindwa kulishika lote kwa urahisi. Pia TISS wanajitahidi kuwatambua na kuwaumbua.

Naamini tutashinda tu hii vita ya kimkakati

Bazazi!
Mtikila alianza kutuhumu kwama Mzee alikuwa ni mtu wa Bahima. Ila kwa ujumla ile vita ndio mstabali wa kinachoendelea hivi sasa katika nchi za maziwa makuu. Mambo mengi sana yametukia baada ya ile vita. Iwapo Amini angeshinda naona maisha nayo yangekuwa tofauti kabisa.
 
Vita ya Kagera ilizaa mambo mengi sana kwenye ukanda huu ambayo yanatokea leo hii.
 
Back
Top Bottom