Kama Tanzania ingeshindwa vita ya Kagera: Je, Rwanda na Uganda zingefika hapa zilipofika leo?

Kama Tanzania ingeshindwa vita ya Kagera: Je, Rwanda na Uganda zingefika hapa zilipofika leo?

Mimi huwa nasemaga kila siku kwamba utakapotangaza nia ya Uraisi wa JMT mimi ntajitolea kupiga kampeni kuanzia Masasi hadi Muleba hata kwa mguu!

Braza umetisha sana na umechambua vizuri mno na hili ndilo jibu nililokuwa nalitafuta hapa. Ambacho mimi huwa kinanifanya nifikirie ni kuhusu Mzee Nyerere, hivi hadi wakina Museveni na Kagame wanaanza kufanya vurugu kule Uganda ina maana Tanzania hatukufikiri hata kidogo ???

Maana ukiangalia matukio ya Afrika Mashariki hadi kufika mwaka 1998 Tanzania ilikuwa inayafuatilia kwa umakini sana. Kama unakumbuka wakati mauaji yanatokea Rwanda kulitokea mvutano mkubwa sana baina ya Mzee Nyerere na Mwinyi ambapo alitaka Tanzania ifanye kitu na kuita hadi waandishi wa habari lakini Mzee Mwinyi akafunga vioo vyote na kuweka mziki mkubwa. Sijui kwanini ilikuwa iko vile lakini inaleta sana maswali.

Upande mwingine, wakina Kabila, Museveni na Kagame walivyomtoa Mobuthu kule Zaire mwaka 1997 Mzee Nyerere alionekana kufurahishwa sana na kile kitendo na baada ya lile tukio akaenda kabisa kutoa muhadhara kwa uongozi mpya kwamba "Zaire haina wajomba watakaoiletea maendeleo".

Ina maana Nyerere alikuwa hana ufahamu wowote juu ya tabia za hawa jamaa wawili ambao amekaa nao tokea vita za Msumbiji, Uganda na Rwanda kwa wakati wote huo ??? Mara nyingi alikuwa akienda kwenye mikutano mikubwa alikuwa akijisifia sana kumtoa Mobuthu na unaona kabisa alikuwa anawafahamu Museveni na Kagame vizuri.

Kaka Chige kuna baadhi ya mambo huwa yanaacha maswali mengi sana yenye ukakasi kuliko majibu yenye kueleweka!
Thanks for complement but dah, I'm speechless! Nimechelewa sana kuiona hii post ambavyo ina lots of constructive questions na hoja fikirishi! Itabidi haya nayo tuyajadili kwa kina ingawaje nadhani sitakuwa available or active enough in the next 24 hours!! zitakuwa
 
Braza Malcom Lumumba salama?

Mjadala mzurii.Mi nafikiri ingekuwa ngumu au ingechukua muda mrefu kwa PK na M7 kuwa walipo. Amin alijua waasi wa Uganda ipo siku wangemvamia, hawakuwa TZ bure. Ndiyo maana moja ya sababu ya vita ni Idi Amini kushambulia na kufanya mto Kagera kuwa mpaka. Hii ingempa water barrier nzuri dhidi ya uvamizi. Sasa angeshinda vita angepata hii water barrier na ingekuwa ngumu kwa waasi kuivuka huku jeshi la Tz liko hoi kwa kipigo. Wangepita wapi? Rwanda hakupitiki, Zaire kuna Mobutu.

Nakubaliana ile vita ina repercussions ndefu sana, kieneo na kihistoria. Pengine tungepigwa hata mauaji ya kimbari yasingetokea, pengine hata zile Congo wars zisingetokea! lakini hizi ni counterfactual s tu japo zinatusaidia sana kuelewa tulipo.
 
Braza Malcom Lumumba salama?

Mjadala mzurii.Mi nafikiri ingekuwa ngumu au ingechukua muda mrefu kwa PK na M7 kuwa walipo. Amin alijua waasi wa Uganda ipo siku wangemvamia, hawakuwa TZ bure. Ndiyo maana moja ya sababu ya vita ni Idi Amini kushambulia na kufanya mto Kagera kuwa mpaka. Hii ingempa water barrier nzuri dhidi ya uvamizi. Sasa angeshinda vita angepata hii water barrier na ingekuwa ngumu kwa waasi kuivuka huku jeshi la Tz liko hoi kwa kipigo. Wangepita wapi? Rwanda hakupitiki, Zaire kuna Mobutu.

Nakubaliana ile vita inarepercussions ndefu sana, kieneo na kihistoria. Pengine tungepigwa hata mauaji ya kimbari yasingetokea, pengine hata zile Congo wars zisingetokea! lakini hizi ni counterfactual s tu japo zinatusaidia sana kuelewa tulipo.
Mkuu mimi nipo salama kabisa. Hapo juu Kaka Chige ametoa uchambuzi mzuri sana, upitie kama utapata nafasi. Lakini sasa leo asubuhi nilikuwa natafakari juu ya Vita ya Kagera, nikagundua kwamba kuna kitu ambacho nilisahau kukiangalia kwa ukaribu ambacho ni: Ongezeko la ushawishi wa mataifa ya nje ambayo ni rafiki wa Idd Amin kama Libya, Palestine na Saud Arabia endapo Uganda ingeshinda ile vita.

Nataka nifukunyue nyaraka kwa undani zaidi ili niweze kufahamu ni kwa kiwango gani haya mataifa ya nje yalikuwa na ushawishi nchini Uganda. Faida zipi za kidiplomasia, kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni yalikuwa yanategemea hadi kupelekea yamuunge mkono Iddi Amini.

MENGINEYO MUHIMU KUJUA:

Mahusiano ya kidiplomasia baina ya Rwanda ya Wahutu na Uganda ya Iddi Amin yalikuwaje ???

Mahusiano ya kidiplomasia baina ya Uganda ya Iddi Amini na Zaire ya Mobuthu yalikuwaje ???

Mahusiano ya Kidiplomasia baina ya Rwanda ya Wahutu na Zaire ya Mobuthu yalikuwaje ???

Vita ya Kagera ni uzi moja mrefu sana unaotupeleka kwenye matukio makubwa kwenye huu ukanda: binafsi nataka kuufuatilia huo uzi hadi unapotokea ili kuyaelewa yanayotokea kipindi hiki na kujaribu kutabiri yatakayotokea kipindi kijacho na nini utakuwa mustakabali wa Tanzania ijayo...............

Mkuu panapo majaliwa ya Mungu naahidi kwamba nitarejea na hiyo tafiti........
 
Mkuu ningependa kujua zaidi Nkurunzinza ame deal nao vipi hawa ma covert?
Ni hatari pale dini au kabila au jamii moja linapotaka kuwa juu ya makundi au jamii nyingine huku vitu kama rangi, umbo LA pua, imani, kimo, ukubwa wa macho, urefu wa shingo, urefu wa miguu vikiwa vigezo

Yaani Ukiwa mweusi hata uwe Na uwezo kiasi gani kwa brain yako wewe ni sifuri tu mbele ya mjerumani - kisa rangi. Hata uwe Na uwezo kiasi gani lakin kama pua yako ni bapa kama sambusa wew aisee ni sifuri tu mbele ya MTU mwenye pua iliyochongoka kama ya 'mrembo wa kiitaliano'. Teh teh teheee

Kua uyaone

Ni rahisi tu. Unawafanya kama nkurunzinza tu. Network zao zote zitakuwa hazishiki tena
 
Unafanya kama nkurunzinza tu. Ukiwagundua wako ndani ya nchi yako halafu wanaleta mambo ambayo kwenu mnaona si sawa unawatanguliza fasta mbele ya haki.

Nkurunzinza asingekuwa anafanya hivyo wangeshambinua zamani sana au kungekuwa ovyo sana Burundi. Tatizo tunawachekea. Mchekee nyani uvune mabua
Kuna kitu cha muhimu sana tumekisahau kukitaja hapa: Hivi bila Raisi Jakaya Kikwete na Waziri wake Benard Membe unadhani Pierre Nkhurunzinza bado angekuwepo kule Burundi mpaka kufika leo hii ???

Tanzania ingepata madhara gani kimkakati kama Raisi Jakaya Kikwete angeamua kufunga mikono yake ya kijeshi na kidiplomasia kipindi kile Raisi Nkhurunzinza alipofanyiwa jaribio la kimapinduzi na mamluki kutoka nje ???

Matatizo ya Burundi yanaathiri vipi usalama wa Tanzania na kwanini walihangaika sana kutaka kumtoa Pierre miaka michache iliyopita ???

Hebu tujadili zaidi.......
 
Je, Tanzania tulikosea kuwasaidia hawa ndugu zetu, hasahasa baada ya kuona mambo ya ajabu wanayoyafanya kule Congo DRC, na kwingineko?
Walioyafanya na yanayofanyika hapo DRC yana baraka za wakubwa (mabeberu) wao wanatumika tu.
 
Mkuu ningependa kujua zaidi Nkurunzinza ame deal nao vipi hawa ma covert?

Yeye nasikia anawatanguliza mbele ya haki tuuuu. Akigundua cell sijui network zao anawamaliza. Wanaenda kuambiana kwamba nkurunzinza ni noma. Wenyewe wanasema isingekuwa hivyo Burundi ingekuwa very shaghalabaghala mpaka dakika hii. PK hataki kabisa nkurunzinza abaki pale.

Nkuru hacheki na kima. Ukikutwa unafanya espionage na matakataka ya aina hiyo Huna bahati.
 
Kuna kitu cha muhimu sanabtumekisahau kukitaja hapa: Hivi bila Raisi Jakaya Kikwete na Waziri wake Benard Membe unadhani Pierre Nkhurunzinza bado angekuwepo kule Burundi mpaka kufika leo hii ???

Tanzania ingepata madhara gani kimkakati kama Raisi Jakaya Kikwete angeamua kufunga mikono yake ya kijeshi na kidiplomasia kipindi kile Raisi Nkhurunzinza alipofanyiwa jaribio la kimapinduzi na mamluki kutoka nje?

Matatizo ya Burundi yanaathiri vipi usalama wa Tanzania na kwanini walihangaika sana kutaka kumtoa Pierre miaka michache iliyopita?

Hebu tujadili zaidi...

Burundi nayo ina idadi kubwa ya Tutsi, baada ya Hutu. PK akifanikiwa kumweka MTU wake Burundi (of course Tutsi) atakuwa amejikusanyia nguvu zaidi pamoja na kufanikisha tamaa zao binafsi kama wanavyoitaga superiority etc. Ukija kumchanganya na m7 itakuja kuwa shida kwa nchi jiran kama tz. Nafikiri bongo haihitaji kuzungukwa na nchi zenye ukaribu na maelewano makubwa halafu zilizojaa ukabila halafu zikiwa chini ya viongozi wababe, wapenda vita, wakabila, you name it. Wanaweza kulianzisha muda wowote.

Jiran akiwa na nguvu msuli halafu akawa mkorofi mtapata taabu sana. Of course naona hata ukijumlisha na Burundi bado watakuwa bado sana kwetu, lakini itakuwa si haba.

Kama kweli kuna suala la Hima Empire, Basi mkwamo mmoja ni Burundi kutokuwa chini ya Tutsi.

Weakness moja kubwa ya hao jamaa ni upinzani mkali wa Hutu against them. Mtu yeyote akitaka kuwashinda hao jamaa ni suala la kuungana na au kuwawezesha Hutu.

Nafikiri Nkurunzinza asingeweza toboa bila msaada wa Tz. Hata angetoboa ingemgharimu sana. Chezea hela anayopata PK kutoka Congo.
 
Burundi nayo INA idadi kubwa ya Tutsi, baada ya Hutu. PK akifanikiwa kumweka MTU wake Burundi (of course Tutsi) atakuwa amejikusanyia nguvu zaidi pamoja na kufanikisha tamaa zao binafsi kama wanavyoitaga superiority etc. Ukija kumchanganya na m7 itakuja kuwa shida kwa nchi jiran kama tz. Nafikiri bongo haihitaji kuzungukwa na nchi zenye ukaribu na maelewano makubwa halafu zilizojaa ukabila halafu zikiwa chini ya viongozi wababe, wapenda vita, wakabila, you name it. Wanaweza kulianzisha muda wowote

Jiran akiwa na nguvu msuli halafu akawa mkorofi mtapata taabu sana. Of course naona hata ukijumlisha na Burundi bado watakuwa bado sana kwetu, lakin itakuwa si haba.

Kama kweli kuna suala LA hima empire , Basi mkwamo mmoja ni Burundi kutokuwa chini ya Tutsi.

Weakness moja kubwa ya hao jamaa ni upinzan mkali wa Hutu against them. Mtu yeyote akitaka kuwashinda hao jamaa ni suala LA kuungana na au kuwawezesha Hutu

Nafikiri Nkurunzinza asingeweza toboa bila msaada wa tz. Hata angetoboa ingemgharimu sana. Chezea hela anayopata PK kutoka Congo
Basi kama ni hivyo Paul Kagame is overrated!
 
Mjadala mzito Sana huu mwalimu Malcom,
Lakini itabidi tu nikujibu, Tanzania haikuwa na lengo wala wazo la kuwasaidia hao unaowaita ndugu zetu, Tanzania tulipigana Vita kulinda Utu , mipaka, na heshima yetu , hiyo kuwasaidia ni neno la diplomasia tu .
Waganda na watutsi waliokuwepo uhamishoni wangeweza kufanya hayo bila msaada wa Tanzania, kupitia nguvu ya umma japo ingechukua muda ila ingekuja tu.
Huna habari nyingi wewe, hujui kabla ya vita kins museveni walikuwa wanapambana na Iddi Amin kutokea Tanzania?
 
Ukweli ni kuwa hatukuwa na ifahamu wa HIMA EMPIRE. Mwalimu alifanya kama Mwafrika kwa ajili ya Afrika dhidi Uovu wa Mwafrika. Kwa kutojua au kutotilia maanani dhana ya HIMA EMPIRE tukawaacha Watutsi ku~dominate Majeshi ya ukombozi wa Uganda. Tulifanyakosa acha tulipe gharama.

Tusuipokuwa makini, Watutsi watatumaliza. Kwanza kwa kutegemea UZURI & UREMBO wa wanawake wao, wanaolewa au kuzaa na Viongozi wetu. Lengo lao ni kuwa na watu wanaoweza remotely control them. Wakati mwingine hawazai nao bali huzaa na watutsi wenzao ma kwa kuwa kitanda hakizai haramu; huhesabiwa kuwa ni Watanzania. Pia wanajipenyeza na kudai ni Watanzania toka kabila la Wanyambo, Wahaya, Wanyiramba/Wanyaturu na Wachaga (Machame). Pia majina ya kwao ama wanayaacha au kuyageuza yafanane na kwetu. Mbinu inawasaidia sana kwani sisi sio wadadisi sana kuhusu ukabila.

Aidha wana~wanausalama wa taifa wa kutosha ktk miji ya Dar, Dodoma, Arusha na labda Mbeya. Wanafanyakazi dhalili na.za hovyo kama kuuza matunda au barmaid. Lengo ni kuwafuatilia wanasiasa na watu wenye ushawishi ktk jamii na kutengeneza urafiki wenye maslahi kwao. Kwa Dar watu nendeni Seblen Pub muone wahudumu na wateja ni kina nani: Mtaniambia.

Uzuri ni kuwa; Linchi hili ni likubwa sana hivyo wanashindwa kulishika lote kwa urahisi. Pia TISS wanajitahidi kuwatambua na kuwaumbua.

Naamini tutashinda tu hii vita ya kimkakati

Bazazi!
Ndiyo maana TRUMP anatuponda sana sisi waafrika akili zetu ziko hoi bin taabani kuangalia WANAWAKE tu!
 
Haikuwa vita braza ilikuwa propaganda ya kumzuia Iddy Amini kutanga uislamu Uganda. Alipata Support kubwa toka kwa Gadaffi na walikuwa na mpango wa kujenga Mskiti mkubwa Uganda, ndo kisa kikaanzia hapo.
Ukipata nafasi nenda bukoba waulize Wazee wa kule wakusimulie Malcom Lumumba.
 
Ndugu yangu Malcom Lumumba,

Pamoja na mambo mengine, umetaja yale yaliyotokea baada ya Museveni kuingia madarakani, kisha ukahoji:-
Kwanza, mimi naomba nianze na Museveni mwenyewe!

Je, Museveni alipiga kambi Tanzania ili kuvuta nguvu ya kumuondoa Iddi Amin madarakani au alipiga kambi Tanzania kuvuta nguvu ili hatimae yeye aingie madarakani?

Mwanzoni ilikuwa rahisi sana kuamini pasipo na shaka kwamba alipiga kambi Tanzania ili kuondoa utawala kandamizi wa Iddi Amin! Na kwavile tayari Mwalimu alishakuwa against Amin, kwake Museveni ilikuwa ni rahisi sana kuuzika kwa zana ya kutaka kuuondoa utawala wa Amin!

Tanzania ikaingia vitani na Uganda, huku ikishirikiana na wafuasi wa Obotte pamoja na Museveni! Iddi Amin akang'olewa madarakani, na baada ya hili na lile, hatimae uchaguzi unafanyika Uganda unaomrudisha Obotte madarakani!

Historia inatukumbusha kwamba, muda mfupi baadae Museven anagoma kukubaliana na matokeo ya uchaguzi kwa hoja zile zile ambazo hadi karne ya 21 bado zinaendelea kutamalaki Afrika... kwamba uchaguzi uliomwingiza Obotte madarakani ulijaa udanganyifu!

Kufuatia tuhuma hizo, Museveni akishirikiana na akina Fred Rwigyema bila kumsahau PK hatimae wanaingia msituni kupambana na serikali ya Obotte!

Hapo ndipo ulipo msingi wa swali langu la awali kwamba, Museveni alipiga kambi Tanzania ili kumuondoa Dikteta Iddi Amin au ili aingie madarakani?! Na hapa tukumbuke kwamba, pamoja na Museven kupiga kambi Tanzania, pia alishakuwa na uzoefu wa kivita aliyokuwa anapigana huko Msumbiji!

Kwa maoni yangu, Museven hakupiga kambi Tanzania ili kumuondoa Amin bali alipiga kambi Tanzania ili kuhakikisha anaiongoza Uganda "no matter what!" Madai yake kwamba uchaguzi ulijaa fraud ni bullshit kwa sababu, tangu aingie madarakani hata mwenyewe hajawahi kufanya uchaguzi usio na mizengwe hata kwa chaguzi alizoitisha kwenye karne ya 21!

Ninachotaka kusema ni kwamba, endapo Tanzania ingeshindwa vita ile bado isingekuwa ndo mwisho wa Museven kutaka kuitawala Uganda!

Na kushindwa kwa Tanzania kungetengeneza " a More Aggressive and Notorious Idd Amin!"

Huyu More Aggressive and Notorious Iddi Amin angekuwa more brutal nchini kwake na matokeo yake angetengeneza wimbi jipya la Wakimbizi wa Uganda ambao majority kama ilivyokuwa wale wa awali ambao ni wafuasi wa Obotte, hawa nao wangeingia Tanzania na kujiunga na Waasi chini ya Museven!

Wimbi hili bila shaka lingehusisha na Wanywaranda waliokuwa Uganda ambao nao walipigana bega kwa bega na Museven ili kumuondoa Obotte madarakani!

Kwa kuangalia hilo, it would be a matter of time kabla Museven na wafuasi wake hawajarudi tena Uganda kama ambavyo wafuasi wa Obotte walivyofanya majaribio kadhaa ya kuingia Uganda kumpiga Iddi Amin ili kumrudisha Obotte madarakani... nazungumzia matukio ya kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!

Hata hivyo, kushindwa kwa Tanzania huenda kungefanya Kagera kusipitike tena! Sasa wangepitia wapi?! Tayari hapa tuna Waasi wa Uganda na Waasi wenye asili ya Rwanda!

Pia tusisahau nchini kwetu tulikuwa na "muasi" mwingine anayeenda kwa jina la Laurent Kabila wa Zaire aliyekuwa na lengo la kumng'oa Mabotu madarakani!

Tukiacha upande wa Mashariki na Kaskazini ya Uganda, Uganda pia ingeingilika ama kupitia Tanzania, Rwanda au Zaire!!

Kwa maana nyingine, it's also a matter of time kwa huu "Utatu Mtakatifu" wa Museven, PK na Kabila kabla haujapanga uanzie wapi! Kwamba, walianzishe Rwanda ili wapate " a playing ground" kama ambavyo PK alivyokuwa ameipata Uganda as a playing ground, au waanzie Kivu ambako Kabila alikuwa na ushawishi kama njia ya kuingia Uganda!

Aidha kushindwa kwa Tanzania huenda kungesababisha tu kutoendesha tena "all-out war" dhidi ya Amin lakini huenda kungeanzisha " a Covert Army" ambayo inge-team up na akina Museven dhidi ya Amin!!

Na kama nilivyosema hapo kabla, Waasi Uganda wangeongezeka, Iddi Amin kiburi kingeongezeka, Ushenzi wa Amin kwa raia wa Uganda hususani wale wa kabila la akina Museven na Obotte ungeozeka, na matokeo yake, huenda Amin angekuwa na maadui wengi zaidi ambao ni Waganda kuliko ilivyokuwa kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!

Na kutokana na hayo, sioni ni namna gani Amin angeweza kufika in 1990's kabla hajafurumushwa!

Hapa ninachoona ni kama ile miaka 6 ya Uganda's Bush war iliyomwingiza Museven madarakani dhidi ya wafuasi wa Obotte, ingekuwa ni miaka ya kumuondoa Amin madarakani baada ya Tanzania kushindwa!

Kwa maana nyingine, haya ya sasa ya akina Kagame huenda yangechelewa tu lakini yangetokea!

Swali lako la pili kwamba:-Kwa maoni yangu, YES, wangekuwapo, kwa kuangalia niliyoeleza hapo juu! Na kwamba:-Hapa naomba niwe makini kidogo ili nisihamishe mjadala! Nitaongea kwa uchache sana kwa hofu ile ile ya kuhamisha mjadala... Tanzania hatupo innocent kutokana na Vita vya Uganda!

By 1979 Tanzania ilikuwa LAZIMA iingie vitani dhidi ya Amin lakini ukiangalia matukio tangia kuondolewa Obotte madarakani na Iddi Amin, Tanzania tukaanza kuitengeneza ile vita "in favor of our beloved Obotte"!

Tukam-provoke Kichaa Iddi Amin, nae akaitikia provocation yetu!!

Hivyo basi, hatukuwasaidia, bali ile vita ilikuwa ni ya kwetu wenyewe! Museven nae akatumia fursa kuonesha lengo lake ni kumuondoa Kichaa Iddi Amin kumbe alikuwa anatutumia tu ili aende kuitawala Uganda!!

Mwalimu alishindwa kuliona hili kwa sababu akili yake yote ilikuwa dhidi ya Amin! Na kama alishaliona lakini akasimamia nadharia ya "adui wa adui yako ni rafiki", well and good.
We jamaa una akili nyingi sana sijui unafanya kazi wapi. Huu uchambuzi umejaa akili za kipekee
 
Ukweli ni kuwa hatukuwa na ifahamu wa HIMA EMPIRE. Mwalimu alifanya kama Mwafrika kwa ajili ya Afrika dhidi Uovu wa Mwafrika. Kwa kutojua au kutotilia maanani dhana ya HIMA EMPIRE tukawaacha Watutsi ku~dominate Majeshi ya ukombozi wa Uganda. Tulifanyakosa acha tulipe gharama.

Tusuipokuwa makini, Watutsi watatumaliza. Kwanza kwa kutegemea UZURI & UREMBO wa wanawake wao, wanaolewa au kuzaa na Viongozi wetu. Lengo lao ni kuwa na watu wanaoweza remotely control them. Wakati mwingine hawazai nao bali huzaa na watutsi wenzao ma kwa kuwa kitanda hakizai haramu; huhesabiwa kuwa ni Watanzania. Pia wanajipenyeza na kudai ni Watanzania toka kabila la Wanyambo, Wahaya, Wanyiramba/Wanyaturu na Wachaga (Machame). Pia majina ya kwao ama wanayaacha au kuyageuza yafanane na kwetu. Mbinu inawasaidia sana kwani sisi sio wadadisi sana kuhusu ukabila.

Aidha wana~wanausalama wa taifa wa kutosha ktk miji ya Dar, Dodoma, Arusha na labda Mbeya. Wanafanyakazi dhalili na.za hovyo kama kuuza matunda au barmaid. Lengo ni kuwafuatilia wanasiasa na watu wenye ushawishi ktk jamii na kutengeneza urafiki wenye maslahi kwao. Kwa Dar watu nendeni Seblen Pub muone wahudumu na wateja ni kina nani: Mtaniambia.

Uzuri ni kuwa; Linchi hili ni likubwa sana hivyo wanashindwa kulishika lote kwa urahisi. Pia TISS wanajitahidi kuwatambua na kuwaumbua.

Naamini tutashinda tu hii vita ya kimkakati

Bazazi!
Seblen Pub ipo wapi?
 
Nyerere mwenyewe ana tuhumiwa kua ni HIMA.

Which is which?
 
Back
Top Bottom