Ndugu yangu
Malcom Lumumba,
Pamoja na mambo mengine, umetaja yale yaliyotokea baada ya Museveni kuingia madarakani, kisha ukahoji:-
Kwanza, mimi naomba nianze na Museveni mwenyewe!
Je, Museveni alipiga kambi Tanzania ili kuvuta nguvu ya kumuondoa Iddi Amin madarakani au alipiga kambi Tanzania kuvuta nguvu ili hatimae yeye aingie madarakani?
Mwanzoni ilikuwa rahisi sana kuamini pasipo na shaka kwamba alipiga kambi Tanzania ili kuondoa utawala kandamizi wa Iddi Amin! Na kwavile tayari Mwalimu alishakuwa against Amin, kwake Museveni ilikuwa ni rahisi sana kuuzika kwa zana ya kutaka kuuondoa utawala wa Amin!
Tanzania ikaingia vitani na Uganda, huku ikishirikiana na wafuasi wa Obotte pamoja na Museveni! Iddi Amin akang'olewa madarakani, na baada ya hili na lile, hatimae uchaguzi unafanyika Uganda unaomrudisha Obotte madarakani!
Historia inatukumbusha kwamba, muda mfupi baadae Museven anagoma kukubaliana na matokeo ya uchaguzi kwa hoja zile zile ambazo hadi karne ya 21 bado zinaendelea kutamalaki Afrika... kwamba uchaguzi uliomwingiza Obotte madarakani ulijaa udanganyifu!
Kufuatia tuhuma hizo, Museveni akishirikiana na akina Fred Rwigyema bila kumsahau PK hatimae wanaingia msituni kupambana na serikali ya Obotte!
Hapo ndipo ulipo msingi wa swali langu la awali kwamba, Museveni alipiga kambi Tanzania ili kumuondoa Dikteta Iddi Amin au ili aingie madarakani?! Na hapa tukumbuke kwamba, pamoja na Museven kupiga kambi Tanzania, pia alishakuwa na uzoefu wa kivita aliyokuwa anapigana huko Msumbiji!
Kwa maoni yangu, Museven hakupiga kambi Tanzania ili kumuondoa Amin bali alipiga kambi Tanzania ili kuhakikisha anaiongoza Uganda "no matter what!" Madai yake kwamba uchaguzi ulijaa fraud ni bullshit kwa sababu, tangu aingie madarakani hata mwenyewe hajawahi kufanya uchaguzi usio na mizengwe hata kwa chaguzi alizoitisha kwenye karne ya 21!
Ninachotaka kusema ni kwamba, endapo Tanzania ingeshindwa vita ile bado isingekuwa ndo mwisho wa Museven kutaka kuitawala Uganda!
Na kushindwa kwa Tanzania kungetengeneza " a More Aggressive and Notorious Idd Amin!"
Huyu More Aggressive and Notorious Iddi Amin angekuwa more brutal nchini kwake na matokeo yake angetengeneza wimbi jipya la Wakimbizi wa Uganda ambao majority kama ilivyokuwa wale wa awali ambao ni wafuasi wa Obotte, hawa nao wangeingia Tanzania na kujiunga na Waasi chini ya Museven!
Wimbi hili bila shaka lingehusisha na Wanywaranda waliokuwa Uganda ambao nao walipigana bega kwa bega na Museven ili kumuondoa Obotte madarakani!
Kwa kuangalia hilo, it would be a matter of time kabla Museven na wafuasi wake hawajarudi tena Uganda kama ambavyo wafuasi wa Obotte walivyofanya majaribio kadhaa ya kuingia Uganda kumpiga Iddi Amin ili kumrudisha Obotte madarakani... nazungumzia matukio ya kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!
Hata hivyo, kushindwa kwa Tanzania huenda kungefanya Kagera kusipitike tena! Sasa wangepitia wapi?! Tayari hapa tuna Waasi wa Uganda na Waasi wenye asili ya Rwanda!
Pia tusisahau nchini kwetu tulikuwa na "muasi" mwingine anayeenda kwa jina la Laurent Kabila wa Zaire aliyekuwa na lengo la kumng'oa Mabotu madarakani!
Tukiacha upande wa Mashariki na Kaskazini ya Uganda, Uganda pia ingeingilika ama kupitia Tanzania, Rwanda au Zaire!!
Kwa maana nyingine, it's also a matter of time kwa huu "Utatu Mtakatifu" wa Museven, PK na Kabila kabla haujapanga uanzie wapi! Kwamba, walianzishe Rwanda ili wapate " a playing ground" kama ambavyo PK alivyokuwa ameipata Uganda as a playing ground, au waanzie Kivu ambako Kabila alikuwa na ushawishi kama njia ya kuingia Uganda!
Aidha kushindwa kwa Tanzania huenda kungesababisha tu kutoendesha tena "all-out war" dhidi ya Amin lakini huenda kungeanzisha " a Covert Army" ambayo inge-team up na akina Museven dhidi ya Amin!!
Na kama nilivyosema hapo kabla, Waasi Uganda wangeongezeka, Iddi Amin kiburi kingeongezeka, Ushenzi wa Amin kwa raia wa Uganda hususani wale wa kabila la akina Museven na Obotte ungeozeka, na matokeo yake, huenda Amin angekuwa na maadui wengi zaidi ambao ni Waganda kuliko ilivyokuwa kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!
Na kutokana na hayo, sioni ni namna gani Amin angeweza kufika in 1990's kabla hajafurumushwa!
Hapa ninachoona ni kama ile miaka 6 ya Uganda's Bush war iliyomwingiza Museven madarakani dhidi ya wafuasi wa Obotte, ingekuwa ni miaka ya kumuondoa Amin madarakani baada ya Tanzania kushindwa!
Kwa maana nyingine, haya ya sasa ya akina Kagame huenda yangechelewa tu lakini yangetokea!
Swali lako la pili kwamba:-Kwa maoni yangu, YES, wangekuwapo, kwa kuangalia niliyoeleza hapo juu! Na kwamba:-Hapa naomba niwe makini kidogo ili nisihamishe mjadala! Nitaongea kwa uchache sana kwa hofu ile ile ya kuhamisha mjadala... Tanzania hatupo innocent kutokana na Vita vya Uganda!
By 1979 Tanzania ilikuwa LAZIMA iingie vitani dhidi ya Amin lakini ukiangalia matukio tangia kuondolewa Obotte madarakani na Iddi Amin, Tanzania tukaanza kuitengeneza ile vita "in favor of our beloved Obotte"!
Tukam-provoke Kichaa Iddi Amin, nae akaitikia provocation yetu!!
Hivyo basi, hatukuwasaidia, bali ile vita ilikuwa ni ya kwetu wenyewe! Museven nae akatumia fursa kuonesha lengo lake ni kumuondoa Kichaa Iddi Amin kumbe alikuwa anatutumia tu ili aende kuitawala Uganda!!
Mwalimu alishindwa kuliona hili kwa sababu akili yake yote ilikuwa dhidi ya Amin! Na kama alishaliona lakini akasimamia nadharia ya "adui wa adui yako ni rafiki", well and good.