Hata kama huo mpango upo je unafikiri atafanikiwa?
Je serikali ya Drc na raia wa huko unafikiri watakubali hilo?
Je jumuiya ya kimataifa, nchi jirani na Drc na nchi rafiki za Drc (SADC) wataruhusu/watakubali hilo?
Kufanikiwa/kutofanikiwa hio itategemea mkuu.
Serikali ya Drc/wananchi wake hawana chochote cha kufanya maana PK alishawavamia mara 2 na hawakufanya chochote cha maana na mpk sasa bado huko maporini Congo ana vijana wake.
Serikali ya Congo bado haijawa imara kijeshi na hata Georgraphy ya Congo ilivyokaa si ya mchezo,lkn pia kuitawala nchi kubwa kama Congo yenye ukubwa wa mara 2.5 ya Tanzania inabidi uwe na taasisi imara kweli kweli kitu ambacho Congo bado hawajawa na uwezo huo.Angalia mfano tu Msitu wa Congo pekee ume cover (1,145,000 sq km) yaani ni mkubwa kuliko nchi yote ya Tz(945,087 sq km) nadhani mpk hapo tu unaweza kuelewa nchi ya dizaini hio ni ngumu kiasi gani kuitawala au waasi wakijificha humo shughuli yake inakuaje.
Kipindi cha vita vya pili vya Congo walioifanya Congo isikamatwe tena na PK mostly ni angola,Zimbabwe na kiasi flani Namibia ambapo kipindi hicho mahusiano yao binafsi ya kina Mugabe na Dos Santos vs na PK yalikua ni mabaya saana lkn PK ni kama alishaona umuhimu/nguvu ya Sadc na akaamua kujenga urafiki nao na sasa wamekua washkaji zake sana tu.
Rais wa sasa wa Angola Lourenço ni mshkaji wake sana tu na Kagame na ni msuluhishi mgogoro wa Rwd vs Uganda na hata Uganda inalalamika urafiki binafsi wa PK na Lourenço ni mkubwa,trip za kigali/ haziishi.
Rais wa Zimbabwe Mnangagwa(akijulikana kama the crocodile kipindi cha vita hio ya Congo alikua front na majeshi ya Zimbabwe) nae ni mshkaji wake kila siku trip zao za kigali/harare na hata sasa madini ya Zimbabwe ambapo yaliwekewa vikwazo kuna michalato inafanyikia Kigali,yanauzika fresh huko wanakojua wao.
Rais wa Tz naona nae wana mahusiano mazuri tu ya kikazi/kibiashara,Magu amefanikisha 90% ya mizigo yote ya Rwanda kupitia Bandari ya Dar lkn pia sera za Magu ni za kuangalia sisi tunafaidika nini na kutokujiingiza kwny migogoro ya watu maana yeye mwenyewe hua anasema nchi hii tumesaidia nchi nyingi sana lkn in return tumepata zero.
Zambia Rais wao Lungu n PK wako fresh kabisa.
Namibia pia wako nayo kwny mahusiano bora kuliko kipindi chochote kile.
South Africa ndio mahusiano yao na PK hua yako 50%|50% sababu ya wakina Nyamwasa kuishi kule na Karegeya alivyouwawa kule,lkn South Africa inapitisha sheria kwamba Mkimbizi yoyote wa kisiasa atayeishi nchini kwao hataruhusiwa kujihusisha na siasa za nchi kwao alikotoka either kwa kuunda chama chake/kufanya vuguvugu zozote akiwa nchini humo la sivyo atanyang’anywa hio hadhi ya ukimbizi na tayari wakina Nyamwasa wameshalamikia jambo hilo so maji yatakua shingoni hapo.Na kwa maana hio uhusiano wa Rwanda na SA utaboreka maana hakutakua na sababu ya msingi ya PK kutuma vijana wake huko SA.
Malawi pia sio kama wana inshu yoyote na PK na wanyalu wengi sana wako huko wanaishi huko malawi wakipiga biashara zao.
Comoro wako nayo poa sana na hata muasi wa Rwanda aliyekua anajiita major Sankara walimdakia hapo hapo Comoro.
Nchi nyingine kama Mauritius,Madagaskar,Eswatin etc sijazotaja sababu sijaona kama hua wanajihusisha sana kijeshi kwny migogoro ya sadc,hata hio Comoro nimeitaja tu sababu ya huyo Sankara.
So nadhani PK kua na mahusiano bora na Key players wa Sadc(Tz,Angola,Zimbabwe,Malawi,S/Africa,Zambia) inamuweka kwny nafasi bora siku ikifika akitaka kufanya mambo huko Congo.
Ni mtizamo tu.