Kama Tanzania ingeshindwa vita ya Kagera: Je, Rwanda na Uganda zingefika hapa zilipofika leo?

Kama Tanzania ingeshindwa vita ya Kagera: Je, Rwanda na Uganda zingefika hapa zilipofika leo?

MALCOM LUMUMBA

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2012
Posts
21,113
Reaction score
65,124
Vita ya Kagera ilikuwa ni ufunguo wa mambo mengi sana kwenye huu ukanda wetu. Pengine kama Iddi Amin angeshinda sidhani kama tungekuwa hali ya leo ingeendelea kuwepo: Tungekuwa na Afrika Mashariki ya tofauti sana, nzuri au mbaya hilo mimi silifahamu.

Lakini ni nadharia yangu kwamba kama ile vita ya mwaka 1979 Tanzania ingeshindwa basi, sidhani kama leo huu ndugu Yoweri Kaguta Musseveni angekuwa Rais wa Uganda wala ndugu Paul Kageme angekuwa Rais wa Rwanda. Hii ni kwasababu mwaka 1972 wakiwa peke yao, waasi wa Uganda walijaribu kumvamia Iddi Amin lakini walipigwa vibaya mno, walifanikiwa pale tu walipoungwa mkono na vikosi vya Tanzania mwaka 1979.

Ile vita iliwajenga kwa kiwango kikubwa sana kijeshi vijana na wanaharakati wa Kitutsi ambao walikuwa wanaishi uhamishoni aidha huko Uganda, Kenya na Tanzania. Wengi wao walipatia mafunzo ya kijeshi Tanzania na kusoma hapa Tanzania kwa pesa za watanzania: Baada ya vita kuisha walipoitwa Waganda wote mashuhuri duniani kule Arusha ili wafanye kikao cha nani aongoze nchi baada ya Iddi Amin, pesa, ushauri na utaalamu wa Watanzania vilitumika pia.

Museveni anakuwa Raisi wa Uganda miaka michache ya mbele na haya yanatokea:

1. Museveni anasaidia kuunda RPA
2. RPF inaanza kupigana na Hyabarimana
3. RPF inaingia Rwanda na kutawala
4. Uganda na Rwanda wanavamia Zaire

Yametokea mengi sana, lakini swali ninalojiuliza ni kwamba: Je, haya yangetokea kama Tanzania ingeshindwa Vita ya Kagera?

Je, Uganda na Watutsi waliokuwa uhamishoni wangeweza kuwa hapa walipo leo bila Tanzania kushinda ile vita?

Je, Tanzania tulikosea kuwasaidia hawa ndugu zetu, hasahasa baada ya kuona mambo ya ajabu wanayoyafanya kule Congo DRC, na kwingineko?​
 
Malcom Lumumba,

Mjadala mzito sana huu mwalimu Malcom, lakini itabidi tu nikujibu. Tanzania haikuwa na lengo wala wazo la kuwasaidia hao unaowaita ndugu zetu.

Tanzania tulipigana Vita kulinda Utu, mipaka, na heshima yetu, hiyo kuwasaidia ni neno la diplomasia tu.

Waganda na Watutsi waliokuwepo uhamishoni wangeweza kufanya hayo bila msaada wa Tanzania, kupitia nguvu ya umma, japo ingechukua muda, ila ingekuja tu.
 
Mjadala mzito Sana huu mwalimu Malcom,
Lakini itabidi tu nikujibu, Tanzania haikuwa na lengo wala wazo la kuwasaidia hao unaowaita ndugu zetu, Tanzania tulipigana Vita kulinda Utu , mipaka, na heshima yetu , hiyo kuwasaidia ni neno la diplomasia tu .
Waganda na watutsi waliokuwepo uhamishoni wangeweza kufanya hayo bila msaada wa Tanzania, kupitia nguvu ya umma japo ingechukua muda ila ingekuja tu.
Mkuu, unadhani Tanzania ingeanguka baada ya 1979, Musseveni na Kagame waliojenga RNA na RPF wangekuwepo hapo walipo leo?

Halafu, Watutsi wamesoma na kufundishwa hapahapa Tanzania na kupewa Logistic Support kwenye vita dhidi ya Wahutu na Mobuthu.
 
Ukweli ni kuwa hatukuwa na ifahamu wa HIMA EMPIRE. Mwalimu alifanya kama Mwafrika kwa ajili ya Afrika dhidi Uovu wa Mwafrika. Kwa kutojua au kutotilia maanani dhana ya HIMA EMPIRE tukawaacha Watutsi ku~dominate Majeshi ya ukombozi wa Uganda. Tulifanyakosa acha tulipe gharama.

Tusuipokuwa makini, Watutsi watatumaliza. Kwanza kwa kutegemea UZURI & UREMBO wa wanawake wao, wanaolewa au kuzaa na Viongozi wetu. Lengo lao ni kuwa na watu wanaoweza remotely control them. Wakati mwingine hawazai nao bali huzaa na watutsi wenzao ma kwa kuwa kitanda hakizai haramu; huhesabiwa kuwa ni Watanzania. Pia wanajipenyeza na kudai ni Watanzania toka kabila la Wanyambo, Wahaya, Wanyiramba/Wanyaturu na Wachaga (Machame). Pia majina ya kwao ama wanayaacha au kuyageuza yafanane na kwetu. Mbinu inawasaidia sana kwani sisi sio wadadisi sana kuhusu ukabila.

Aidha wana~wanausalama wa taifa wa kutosha ktk miji ya Dar, Dodoma, Arusha na labda Mbeya. Wanafanyakazi dhalili na.za hovyo kama kuuza matunda au barmaid. Lengo ni kuwafuatilia wanasiasa na watu wenye ushawishi ktk jamii na kutengeneza urafiki wenye maslahi kwao. Kwa Dar watu nendeni Seblen Pub muone wahudumu na wateja ni kina nani: Mtaniambia.

Uzuri ni kuwa; Linchi hili ni likubwa sana hivyo wanashindwa kulishika lote kwa urahisi. Pia TISS wanajitahidi kuwatambua na kuwaumbua.

Naamini tutashinda tu hii vita ya kimkakati

Bazazi!
 
Mkuu, unadhani Tanzania ingeanguka baada ya 1979, Musseveni na Kagame waliojenga RNA na RPF wangekuwepo hapo walipo leo ???

Halafu, Watutsi wamesoma na kufundishwa hapahapa Tanzania na kupewa Logistic Support kwenye vita dhidi ya Wahutu na Mobuthu.

Malcom hao wangekuwepo tu, Tanzania ilivaa yenyewe mkenge ilidhani kwa kufanya hivyo ingehodhi maeneo yote ila nikinyume chake, tulitaka kulinda Utu, heshima na mipaka yetu.

Na kwa hasira zaidi tukaamua ili tuweze kuchukua mipaka kihalali na ushawishi zaidi tuweze kuwaweka na hao uliowataja.

Tanzania tungefeli kwenye hiyo Vita wangeibuka wengine na wengine list ingeendelea tu.
 
Ukweli ni kuwa hatukuwa na ifahamu wa HIMA EMPIRE. Mwalimu alifanya kama Mwafrika kwa ajili ya Afrika dhidi Uovu wa Mwafrika. Kwa kutojua au kutotilia maanani dhana ya HIMA EMPIRE tukawaacha Watutsi ku~dominate Majeshi ya ukombozi wa Uganda. Tulifanyakosa acha tulipe gharama.

Tusuipokuwa makini, Watutsi watatumaliza. Kwanza kwa kutegemea UZURI & UREMBO wa wanawake wao, wanaolewa au kuzaa na Viongozi wetu. Lengo lao ni kuwa na watu wanaoweza remotely control them. Wakati mwingine hawazai nao bali huzaa na watutsi wenzao ma kwa kuwa kitanda hakizai haramu; huhesabiwa kuwa ni Watanzania. Pia wanajipenyeza na kudai ni Watanzania toka kabila la Wanyambo, Wahaya, Wanyiramba/Wanyaturu na Wachaga (Machame). Pia majina ya kwao ama wanayaacha au kuyageuza yafanane na kwetu. Mbinu inawasaidia sana kwani sisi sio wadadisi sana kuhusu ukabila.

Aidha wana~wanausalama wa taifa wa kutosha ktk miji ya Dar, Dodoma, Arusha na labda Mbeya. Wanafanyakazi dhalili na.za hovyo kama kuuza matunda au barmaid. Lengo ni kuwafuatilia wanasiasa na watu wenye ushawishi ktk jamii na kutengeneza urafiki wenye maslahi kwao. Kwa Dar watu nendeni Seblen Pub muone wahudumu na wateja ni kina nani: Mtaniambia.

Uzuri ni kuwa; Linchi hili ni likubwa sana hivyo wanashindwa kulishika lote kwa urahisi. Pia TISS wanajitahidi kuwatambua na kuwaumbua.

Naamini tutashinda tu hii vita ya kimkakati

Bazazi!
Hizo ni stori tu za kwenye gahawa.

Nitajie nchi hata moja isiyolinda maslahi yake kwenye nchi za kigeni?
 
Acha kuwaza ujinga ujjnga na kujitia hofu
 
Malcom hao wangekuwepo tu, Tanzania ilivaa yenyewe mkenge ilidhani kwa kufanya hivyo ingehodhi maeneo yote ila nikinyume chake, tulitaka kulinda Utu , heshima , na mipaka yetu.
Na kwa hasira zaidi tukaamua ili tuweze kuchukua mipaka kihalali na ushawishi zaidi tuweze kuwaweka na hao uliowataja.
Tanzania tungefeli kwenye hiyo Vita wangeibuka wengine na wengine list ingeendelea tu.

Naweza kukubali maana kila kitu kinawezekana. Lakini sidhani kama Tanzania ingeangukia mikononi mwa vikosi vya Uganda na Libya leo hii Rwanda na Uganda zingefika hapo zilipo: Tungekuwa tumeingia kwenye ukurasa mwingine kabisa wa historia.
 
Ukweli ni kuwa hatukuwa na ifahamu wa HIMA EMPIRE. Mwalimu alifanya kama Mwafrika kwa ajili ya Afrika dhidi Uovu wa Mwafrika. Kwa kutojua au kutotilia maanani dhana ya HIMA EMPIRE tukawaacha Watutsi ku~dominate Majeshi ya ukombozi wa Uganda. Tulifanyakosa acha tulipe gharama.

Tusuipokuwa makini, Watutsi watatumaliza. Kwanza kwa kutegemea UZURI & UREMBO wa wanawake wao, wanaolewa au kuzaa na Viongozi wetu. Lengo lao ni kuwa na watu wanaoweza remotely control them. Wakati mwingine hawazai nao bali huzaa na watutsi wenzao ma kwa kuwa kitanda hakizai haramu; huhesabiwa kuwa ni Watanzania. Pia wanajipenyeza na kudai ni Watanzania toka kabila la Wanyambo, Wahaya, Wanyiramba/Wanyaturu na Wachaga (Machame). Pia majina ya kwao ama wanayaacha au kuyageuza yafanane na kwetu. Mbinu inawasaidia sana kwani sisi sio wadadisi sana kuhusu ukabila.

Aidha wana~wanausalama wa taifa wa kutosha ktk miji ya Dar, Dodoma, Arusha na labda Mbeya. Wanafanyakazi dhalili na.za hovyo kama kuuza matunda au barmaid. Lengo ni kuwafuatilia wanasiasa na watu wenye ushawishi ktk jamii na kutengeneza urafiki wenye maslahi kwao. Kwa Dar watu nendeni Seblen Pub muone wahudumu na wateja ni kina nani: Mtaniambia.

Uzuri ni kuwa; Linchi hili ni likubwa sana hivyo wanashindwa kulishika lote kwa urahisi. Pia TISS wanajitahidi kuwatambua na kuwaumbua.

Naamini tutashinda tu hii vita ya kimkakati

Bazazi!
Ila sasa hao Wahima wanawatishia watanzania tu, mbona hawawatishii Wakenya ???
 
Unafanya kama Nkurunzinza tu. Ukiwagundua wako ndani ya nchi yako halafu wanaleta mambo ambayo kwenu mnaona si sawa unawatanguliza fasta mbele ya haki.

Nkurunzinza asingekuwa anafanya hivyo wangeshambinua zamani sana au kungekuwa ovyo sana Burundi. Tatizo tunawachekea. Mchekee nyani uvune mabua.
 
Unafanya kama nkurunzinza tu. Ukiwagundua wako ndani ya nchi yako halafu wanaleta mambo ambayo kwenu mnaona si sawa unawatanguliza fasta mbele ya haki.

Nkurunzinza asingekuwa anafanya hivyo wangeshambinua zamani sana au kungekuwa ovyo sana Burundi. Tatizo tunawachekea. Mchekee nyani uvune mabua
Nashukuru sana Mkuu, lakini nadhani tunasahau kwanza swali la msingi nililouliza: Je, unadhani Rwanda na Uganda wangekuwa hapa walipo leo kama Tanzania ingeanguka kipindi cha vita ya Kagera ???

Kiufupi ni kwamba: Je, Kagame na Musseveni leo hii wangekuwepo hapo walipo kama isingekuwa ni mchango wa Tanzania ???
 
Hapana wasingekuwa.
 
Ndugu yangu Malcom Lumumba,

Pamoja na mambo mengine, umetaja yale yaliyotokea baada ya Museveni kuingia madarakani, kisha ukahoji:-
Yametokea mengi sana, lakini swali ninalojiuliza ni kwamba: Je, haya yangetokea kama Tanzania ingeshindwa Vita ya Kagera ???
Kwanza, mimi naomba nianze na Museveni mwenyewe!

Je, Museveni alipiga kambi Tanzania ili kuvuta nguvu ya kumuondoa Iddi Amin madarakani au alipiga kambi Tanzania kuvuta nguvu ili hatimae yeye aingie madarakani?

Mwanzoni ilikuwa rahisi sana kuamini pasipo na shaka kwamba alipiga kambi Tanzania ili kuondoa utawala kandamizi wa Iddi Amin! Na kwavile tayari Mwalimu alishakuwa against Amin, kwake Museveni ilikuwa ni rahisi sana kuuzika kwa zana ya kutaka kuuondoa utawala wa Amin!

Tanzania ikaingia vitani na Uganda, huku ikishirikiana na wafuasi wa Obotte pamoja na Museveni! Iddi Amin akang'olewa madarakani, na baada ya hili na lile, hatimae uchaguzi unafanyika Uganda unaomrudisha Obotte madarakani!

Historia inatukumbusha kwamba, muda mfupi baadae Museven anagoma kukubaliana na matokeo ya uchaguzi kwa hoja zile zile ambazo hadi karne ya 21 bado zinaendelea kutamalaki Afrika... kwamba uchaguzi uliomwingiza Obotte madarakani ulijaa udanganyifu!

Kufuatia tuhuma hizo, Museveni akishirikiana na akina Fred Rwigyema bila kumsahau PK hatimae wanaingia msituni kupambana na serikali ya Obotte!

Hapo ndipo ulipo msingi wa swali langu la awali kwamba, Museveni alipiga kambi Tanzania ili kumuondoa Dikteta Iddi Amin au ili aingie madarakani?! Na hapa tukumbuke kwamba, pamoja na Museven kupiga kambi Tanzania, pia alishakuwa na uzoefu wa kivita aliyokuwa anapigana huko Msumbiji!

Kwa maoni yangu, Museven hakupiga kambi Tanzania ili kumuondoa Amin bali alipiga kambi Tanzania ili kuhakikisha anaiongoza Uganda "no matter what!" Madai yake kwamba uchaguzi ulijaa fraud ni bullshit kwa sababu, tangu aingie madarakani hata mwenyewe hajawahi kufanya uchaguzi usio na mizengwe hata kwa chaguzi alizoitisha kwenye karne ya 21!

Ninachotaka kusema ni kwamba, endapo Tanzania ingeshindwa vita ile bado isingekuwa ndo mwisho wa Museven kutaka kuitawala Uganda!

Na kushindwa kwa Tanzania kungetengeneza " a More Aggressive and Notorious Idd Amin!"

Huyu More Aggressive and Notorious Iddi Amin angekuwa more brutal nchini kwake na matokeo yake angetengeneza wimbi jipya la Wakimbizi wa Uganda ambao majority kama ilivyokuwa wale wa awali ambao ni wafuasi wa Obotte, hawa nao wangeingia Tanzania na kujiunga na Waasi chini ya Museven!

Wimbi hili bila shaka lingehusisha na Wanywaranda waliokuwa Uganda ambao nao walipigana bega kwa bega na Museven ili kumuondoa Obotte madarakani!

Kwa kuangalia hilo, it would be a matter of time kabla Museven na wafuasi wake hawajarudi tena Uganda kama ambavyo wafuasi wa Obotte walivyofanya majaribio kadhaa ya kuingia Uganda kumpiga Iddi Amin ili kumrudisha Obotte madarakani... nazungumzia matukio ya kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!

Hata hivyo, kushindwa kwa Tanzania huenda kungefanya Kagera kusipitike tena! Sasa wangepitia wapi?! Tayari hapa tuna Waasi wa Uganda na Waasi wenye asili ya Rwanda!

Pia tusisahau nchini kwetu tulikuwa na "muasi" mwingine anayeenda kwa jina la Laurent Kabila wa Zaire aliyekuwa na lengo la kumng'oa Mabotu madarakani!

Tukiacha upande wa Mashariki na Kaskazini ya Uganda, Uganda pia ingeingilika ama kupitia Tanzania, Rwanda au Zaire!!

Kwa maana nyingine, it's also a matter of time kwa huu "Utatu Mtakatifu" wa Museven, PK na Kabila kabla haujapanga uanzie wapi! Kwamba, walianzishe Rwanda ili wapate " a playing ground" kama ambavyo PK alivyokuwa ameipata Uganda as a playing ground, au waanzie Kivu ambako Kabila alikuwa na ushawishi kama njia ya kuingia Uganda!

Aidha kushindwa kwa Tanzania huenda kungesababisha tu kutoendesha tena "all-out war" dhidi ya Amin lakini huenda kungeanzisha " a Covert Army" ambayo inge-team up na akina Museven dhidi ya Amin!!

Na kama nilivyosema hapo kabla, Waasi Uganda wangeongezeka, Iddi Amin kiburi kingeongezeka, Ushenzi wa Amin kwa raia wa Uganda hususani wale wa kabila la akina Museven na Obotte ungeozeka, na matokeo yake, huenda Amin angekuwa na maadui wengi zaidi ambao ni Waganda kuliko ilivyokuwa kabla ya 1979 Uganda-Tanzania War!

Na kutokana na hayo, sioni ni namna gani Amin angeweza kufika in 1990's kabla hajafurumushwa!

Hapa ninachoona ni kama ile miaka 6 ya Uganda's Bush war iliyomwingiza Museven madarakani dhidi ya wafuasi wa Obotte, ingekuwa ni miaka ya kumuondoa Amin madarakani baada ya Tanzania kushindwa!

Kwa maana nyingine, haya ya sasa ya akina Kagame huenda yangechelewa tu lakini yangetokea!

Swali lako la pili kwamba:-
Je, Uganda na Watutsi waliokuwa uhamishoni wangeweza kuwa hapa walipo leo bila Tanzania kushinda ile vita ???
Kwa maoni yangu, YES, wangekuwapo, kwa kuangalia niliyoeleza hapo juu! Na kwamba:-
Je, Tanzania tulikosea kuwasaidia hawa ndugu zetu, hasahasa baada ya kuona mambo ya ajabu wanayoyafanya kule Congo DRC, na kwingineko ???
Hapa naomba niwe makini kidogo ili nisihamishe mjadala! Nitaongea kwa uchache sana kwa hofu ile ile ya kuhamisha mjadala... Tanzania hatupo innocent kutokana na Vita vya Uganda!

By 1979 Tanzania ilikuwa LAZIMA iingie vitani dhidi ya Amin lakini ukiangalia matukio tangia kuondolewa Obotte madarakani na Iddi Amin, Tanzania tukaanza kuitengeneza ile vita "in favor of our beloved Obotte"!

Tukam-provoke Kichaa Iddi Amin, nae akaitikia provocation yetu!!

Hivyo basi, hatukuwasaidia, bali ile vita ilikuwa ni ya kwetu wenyewe! Museven nae akatumia fursa kuonesha lengo lake ni kumuondoa Kichaa Iddi Amin kumbe alikuwa anatutumia tu ili aende kuitawala Uganda!!

Mwalimu alishindwa kuliona hili kwa sababu akili yake yote ilikuwa dhidi ya Amin! Na kama alishaliona lakini akasimamia nadharia ya "adui wa adui yako ni rafiki", well and good.
 
Ila sasa hao Wahima wanawatishia watanzania tu, mbona hawawatishii Wakenya ???
Hima Empire inahusisha ya Tanzania, Uganda, Kenya, Rwanda, Burundi na DRC Mashariki. Kenya wanao na ndio sababu kuna Mauaji yalifanyika ya Wapinzani wa PK.

Uzuri ni kuwa watu muendelee kuwaza kuwa ni stori za kijiweni ila mkae mkijiandaa kutawaliwa na Wahima. Uwekeni huu uzi kwa rejea ya siku zijazo

Bazazi
 
Nashukuru sana Mkuu, lakini nadhani tunasahau kwanza swali la msingi nililouliza: Je, unadhani Rwanda na Uganda wangekuwa hapa walipo leo kama Tanzania ingeanguka kipindi cha vita ya Kagera ???

Kiufupi ni kwamba: Je, Kagame na Musseveni leo hii wangekuwepo hapo walipo kama isingekuwa ni mchango wa Tanzania ???

Tungepigwa vita ile ina maana Idd Amini angeshinda na hivyo kubaki madarakani.

Amin hakuwa na mpango wa kuachia madaraka. Amini angekuwa more powerfull na more deadly. Upinzani wa aina yoyote ungekuwa unazimwa kwa force kubwa.

Hata kabla hatujaingia kupigana na Amin kulikuwa na vikundi vinapigana na Amin. Lakin inasemwa kuwa vilikuwa dhaifu kwa namna nyingi. Mwanajeshi Amin alikuwa anavivuruga kila kukicha.

Baba wa Taifa inasemwa kuwa alikuwa hamfagilii Amin. Sababu zinatajwa kadhaa....
Huenda Tz ilikuwa inavibeba baadhi ya hivi vikundi vya hujuma dhidi ya Nduli. Lakin naona ilionekana kama vilikuwa haviwezi kufua dafu mbele ya mwanajeshi yule

Dawa labda ikawa kumuingilia mazima. Mipango ikasukwa Amin akaingia kichwa kichwa. Watu tukazama. Nduli akatoka nje ya mipaka. Tukaona atarudi tena. Tukamfuata mpaka chumbani kwake Kampala. Tukamtimua nduki. Huyoooo Arabuni

Kuna watu wanasema ilitosha tulivyomtoa nje ya mipaka. Kwenda kumng'oa kabisa haikuwa lazima. Any way, ishakuwa. Hajarudi tena

Baada ya kumfurumua madarakan ndo hapo tukaanza kutengeneza wa kushika Ikulu ya Kampala. Akina Lule, Binaisa mpaka M7.

Wengi wa hawa jamaa walikuwa wapinzani wa Amin na huenda tulikuwa tunawapiga tafu kiaiana bila mafanikio. Inasemwa majeshi ya Tz yalipigana bega kwa bega na vikundi vya wengi wa hawa.

Any way. Bila Amin kutimuliwa Kampala M7 asingekaa ashike white house ya Kampala, labda baadae sana Tena sana. M7 alikuwa zake nasikia Moshi akifundisha
M7 alimsaidia Kagame kwa Hali Na Mali kushika Kigali

Amin alikuwa mtata Na mtemi haswaaa. kwenye vyombo vyake vya ulinzi akiwa amejaza watu kutoka maeneo atokako. Akiwadaka hao wapinzani wapiganaji wa msituni alikuwa anawafinya vilivyo. Huyo M7 and therefore Kagame wangeibukia wapi?

Naamini tulimchukia Amin kuliko Amin alivyotuchukia sie
 
Back
Top Bottom