Kama tuna haki tudai lakini tuepuke mihemko! Refa wa kati tunamuangushia jumba bovu!

Bome-e

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
17,179
Reaction score
26,188
Wakuu,kuna suala nimeliona kuanzia kwa mashabiki,wachambuzi na hata viongozi mbalimbali juu ya mechi ya Yanga vs Mamelods!
Lawama nimeona zikienda kwa refa wa kati kwa kuacha kwenda kuangalia VAR kuhusu mpira wa Aziz Ki lakini akaenda kuangalia foul ya Lomalisa kwenye VAR ili aangalie kama ilistahili kadi nyekundu au la!
Ndio hapo naona watu wanachanganya,wanashindwa kuelewa majukumu ya refa wa kati!Nitaeleza kwa ufupi na mwenye kuelewa ataelewa cha msingi usitangulize mihemko!

*Refa wa kati huwajibika kwenda kuangalia VAR pale ambako kuna tukio la utata ambapo ataenda kujiridhisha!Matukio haya ni yale ambayo yeye kama refa wa kati ana uwezo wa kuamua kwa utashi wake!Mfano matukio ya penalty na foul,mambo hayo hutegemea utashi wa refa!Refa anaweza kuamua iwe penalty au isiwe penalty,anaweza akaamua iwe kadi ya njano au nyekundu!Hapo VAR haimwambii kuwa atoe kadi ya njano au nyekundu bali anatumia utashi wake kwa kuzingatia kanuni za mpira wa miguu!VAR haimwambii refa wa kati atoe penalty au asitoe,ni utashi wake kulingana na kile anachokiona!

*Sehemu ya pili ni matukio ya utata ambayo refa wa kati hana utashi nayo!Matukio haya ni kama Offside na mpira kuvuka mstari wa goli!Matukio haya huamuliwa na VAR moja kwa moja!Kwa mantiki hiyo,kama refa wa kati hana utashi kwenye maamuzi basi ndio maana wasaidizi wake humpa taarifa tu kuwa hiyo ni offside au goli limeingia au halijaingia!
Ulishawahi kuona refa wa kati anaenda kwenye VAR kuangalia kama ni offside,hicho kitakuwa kichekesho!

Kwa wanaomlalamikia refa wa kati eti kwanini hakwenda kujiridhisha kwenye VAR kama mpira wa Azizi ki nadhani sasa mmeelewa!
Nimeshangaa viongozi wa Yanga katika barua yao ya malalamiko,wamemlalamikia refa wa kati kuacha kwenda kuangalia VAR kwenye mpira wa azizi Ki lakini refa huyo huyo akaenda kuangalia VAR kwenye tukio la Lomalisa la foul ili kujua ni kadi ya njano au nyekundu!

Ukisoma taratibu bila jazba utanielewa!

NB: Penalty;Hata kwa kutumia VAR,tukio moja linaweza kuamuliwa tofauti na marefa wawili tofauti!Kuna refa anaweza kusema hii ni penalty na refa mwingine akasema hiyo sio penalty,hiyo ndio maana ya utashi!

Offside:Kwa kutumia VAR,refa hana choice!Ikishachorwa ile mistari miwili ndio basi,refa hana choice!
Ndio maana Offside na goal,refa hupewa tu taarifa kupitia microphone!
Tumeelewana wakuu au nieleze zaidi?

Refa wa kati apewe maua yake,alichezesha ile mechi vizuri sana!

Picha hii kwa macho na angle ya camera,unajiridhisha 100% kuwa mpira wote umevuka mstari,angle ya camera ilipobadilishwa,kuna sehemu ya mpira ilikuwa bado iko juu ya mstari!

Screenshot_20240408-163102.png
 
Ulaya huko, afu mburukenge za matombo TZ zinademka kisistaduu kuwa Yanga hakudhulumiwa goli halali,

Ubinadamu ni kazi/Humanity is a work.
Screenshot_2024-04-07-16-00-31-66_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
 
Wizi ni wizi tu hakuna kuhalalisha ujambaka.

Yanga tuliibiwa goli
Hujaelewa nilichoandika,wabongo ni full mihemko!
Mimi hata sijazungumzia goli kama ni halali au sio halali
 
Wewe ndie upunguze mhemko hujaelewa point ya mashabiki wa Yanga,refa wa kati hata hakukoshughulisha kwenda kuichungulia VAR hicho ndio kinalalamikiwa sana

Ndio maana nasema hujanielewa!Ungesoma maelezo yangu ungenielewa!
Refa wa kati hupewa tu taarifa na timu yake ya wasaidizi iliyo kwenye vyumba!Na taarifa aliyopewa ni kuwa sio goli!Vipi kama Refa wa kati angepewa taarifa kuwani goal,ungelalamika?
 
Wakuu,kuna suala nimeliona kuanzia kwa mashabiki,wachambuzi na hata viongozi mbalimbali juu ya mechi ya Yanga vs Mamelods!
Lawama nimeona zikienda kwa refa wa kati kwa kuacha kwenda kuangalia VAR kuhusu mpira wa Aziz Ki lakini akaenda kuangalia foul ya Lomalisa kwenye VAR ili aangalie kama ilistahili kadi nyekundu au la!
Ndio hapo naona watu wanachanganya,wanashindwa kuelewa majukumu ya refa wa kati!Nitaeleza kwa ufupi na mwenye kuelewa ataelewa cha msingi usitangulize mihemko!

*Refa wa kati huwajibika kwenda kuangalia VAR pale ambako kuna tukio la utata ambapo ataenda kujiridhisha!Matukio haya ni yale ambayo yeye kama refa wa kati ana uwezo wa kuamua kwa utashi wake!Mfano matukio ya penalty na foul,mambo hayo hutegemea utashi wa refa!Refa anaweza kuamua iwe penalty au isiwe penalty,anaweza akaamua iwe kadi ya njano au nyekundu!Hapo VAR haimwambii kuwa atoe kadi ya njano au nyekundu bali anatumia utashi wake kwa kuzingatia kanuni za mpira wa miguu!VAR haimwambii refa wa kati atoe penalty au asitoe,ni utashi wake kulingana na kile anachokiona!

*Sehemu ya pili ni matukio ya utata ambayo refa wa kati hana utashi nayo!Matukio haya ni kama Offside na mpira kuvuka mstari wa goli!Matukio haya huamuliwa na VAR moja kwa moja!Kwa mantiki hiyo,kama refa wa kati hana utashi kwenye maamuzi basi ndio maana wasaidizi wake humpa taarifa tu kuwa hiyo ni offside au goli limeingia au halijaingia!
Ulishawahi kuona refa wa kati anaenda kwenye VAR kuangalia kama ni offside,hicho kitakuwa kichekesho!

Kwa wanaomlalamikia refa wa kati eti kwanini hakwenda kujiridhisha kwenye VAR kama mpira wa Azizi ki nadhani sasa mmeelewa!
Nimeshangaa viongozi wa Yanga katika barua yao ya malalamiko,wamemlalamikia refa wa kati kuacha kwenda kuangalia VAR kwenye mpira wa azizi Ki lakini refa huyo huyo akaenda kuangalia VAR kwenye tukio la Lomalisa la foul ili kujua ni kadi ya njano au nyekundu!

Ukisoma taratibu bila jazba utanielewa!

NB: Penalty;Hata kwa kutumia VAR,tukio moja linaweza kuamuliwa tofauti na marefa wawili tofauti!Kuna refa anaweza kusema hii ni penalty na refa mwingine akasema hiyo sio penalty,hiyo ndio maana ya utashi!

Offside:Kwa kutumia VAR,refa hana choice!Ikishachorwa ile mistari miwili ndio basi,refa hana choice!
Ndio maana Offside na goal,refa hupewa tu taarifa kupitia microphone!
Tumeelewana wakuu au nieleze zaidi?

Refa wa kati apewe maua yake,alichezesha ile mechi vizuri sana!
Umeandika ushubwada tu, kwa akili zako ww na mwanasheria wa YANGA nani Bora na unafikili ile barua imeandikwa na mtu mmoja ?
 
Nn maana ya Video Assistant Referee ? Na kwann ipo uwanjani kama maelekezo huwa yanatoka chumba Cha wasaidizi?
 
Nn maana ya Video Referee Assistant? Na kwann ipo uwanjani kama maelekezo huwa yanatoka chumba Cha wasaidizi?
Inamaana hujaelewa maelezo yangu?Nitafutie clip hata moja ambayo refa walati ameenda kuangalia kama mpira umevuka mstari au offside kwenye VAR!
 
Sasa kwann inawekwa uwanjani kama haimsaidii referee kwenye maamuzi yenye utata?
 
Back
Top Bottom