Kama tuna haki tudai lakini tuepuke mihemko! Refa wa kati tunamuangushia jumba bovu!

Kwa hiyo tuelewe kwamba kuidhinisha hili ni goli au siyo goli si kazi ya refa?
Kwa uelewa wako,uwanjani Kuna marefa wangapi?Hao wengine wako kwa ajili gani?je,kila tukio tatanishi,refa wa Kati anapaswa kwenda kuamua mwenyewe?Je,uamuzi wa refa mmoja na uamuzi wa marefa watatu kwenye tukio moja,ni upi more likely to be correct?
Je,referee angeambiwa ni goli na wasaidizi wake na akaweka mpira Kati,angepata hizi lawama kwanini hajaenda yeye binafsi kuangalia?
Uwanjani majukumu yamegawanywa,wasaidizi wake wakimwambia kuwa mpira umevuka mstari wa goli basi hiyo inatosha kwa refa kuweka mpira Kati!
 
Tatizo hatuwaungi mkono DSTV,we VAR gani ni upande mmoja tu ina maana DSTV walishindwa kuweka kamera tatu golini tuone na video za upande mwengine.azam angepewa hiyo tenda mbona makamera yanamwagika tu.
 
Wanakaza mafuvu tuu

Tukio la offside au mpira kuvuka line, huamuliwa na teknolojia moja kwa moja refa yeye hupewa taarifa tuu na chumba cha VAR kuwa ni goli au sio goli

Matukio kama penati, faulu, mtu kunawa mpira, hayo yanahitaji utashi wa refa kuamua hivo kujiridhisha

Nimewashangaa sana Yanga na wachambuzi kulinganisha tukio la lomalisa na hilo la goli
 
Kosa labda ni kutooneshwa ni namna gani mpira ulionekana baada ya kuchora line kama tunavooneshwa kwenye offside,

Sio kulaumu eti kwanini refa hakwenda kuangalia wakati haamui yeye tukio kama hilo
 
Hatimaye nimekutana na comment ya mtu anayeelewa mpira!
 
Kosa labda ni kutooneshwa ni namna gani mpira ulionekana baada ya kuchora line kama tunavooneshwa kwenye offside,

Sio kulaumu eti kwanini refa hakwenda kuangalia wakati haamui yeye tukio kama hilo
Exactly
 
Kama siyo goli yanga walitakiwa wapewe kona
 
Umeelewa mada lakini?Umekurupuka,mimi sijazungumzia kama ni goli au sio goli!
Tuliza mihemko utaelewa nilichoandika!
W endio utulize mihemko, kama hujazungumzia kuwa goli ama sio goli huoni kama hujielewi.
 
Refa ameshaeleza kwanini alienda kuangalia faulu ya lomalisa kwenye var na kwanini hakuangalia marudio ya goli kwenye var Ila kwa sababu ile timu wenye akili ni wawili ndio maana unaona hayo malalamiko.
Kwanini haikuwa kona..!!???
 
Ilikuwa nini baada ya hapo?
Baada ya lile goli kwa mpira kudunda golini, mchezaji wa masandawana aliutoa mpira nje na kipa wao akaenda kuuchukua nje ya goal line. Baada ya mpira kusimama kwa muda, kwenye kuuanzisha, refa alimpa kipa apige kama vile aliudaka. Hili lilikuwa kosa jingine..!! Ndo hapo nakuuliza wewe bwana Bome-e, kwa vile mpira ulivuka goal nje ya goli, kwanini haikuwa kona?
 
Ingepigwa kona,moyo wako ungeridhika?Tuache hizi lialia,tujipange kwa michuano ijayo!
 
Ingepigwa kona,moyo wako ungeridhika?Tuache hizi lialia,tujipange kwa michuano ijayo!
Unatoka nje ya hoja sasa, au umeishiwa hoja..!!?? Suala si kuridhika au kutorishika kwangu, maana hata kama sijaridhika na nisichoridhika nacho ndiyo haki, hamna namna. Hii nimeiweka kukuonyesha kwamba refa alikuwa na lake moyoni ambalo linakinzana na haki..!!

BTW, kama umeishiwa hoja, kubaliana na wenye hoja..!! usilete habari za kuridhika au la..!! Hata mwizi akishindwa kuiba huwa haridhiki, lakini wizi si jambo la haki..!! Suala ni haki.
 
Yaani unajaribu kuaminisha kwamba refa alikuwa na jambo lake na Yanga!Ingekuwa hivyo,angeweza kutoa red card kwa Lomalisa!Halafu aliyesema mpira haukuvuka mstari sio refa wa kati bali ni wasaidizi wake 3 ambao wako vyumba vya VAR!
Mechi ya Simba na Alahyl,kuna mchezaji wa simba alipiga mpira ukamgonga kichwani mpinzani na ukarudi kwenye possession ya Simba,refa akasimamisha mpira na akaenda kumuangalia mchezaji aliyeumia!Baada ya hapo refa akawapa mpira Alahyl waanzishe mpira!Hapo napo utasema refa alikula njama?
Tuache hizi lialia
 
Tunajaribu kuangalia tukio halisi na yaliyojiri baadae ya tukio, scenario and possible arguments
Tukubaliane na jambo moja kwanza kabla ya kurukia jambo lingine!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…