Kama tuna haki tudai lakini tuepuke mihemko! Refa wa kati tunamuangushia jumba bovu!

Unahalalisha kosa kwa kutumia kosa..!! Hoja mufirisi kabisa..!!
 
Refa ameshaeleza kwanini alienda kuangalia faulu ya lomalisa kwenye var na kwanini hakuangalia marudio ya goli kwenye var Ila kwa sababu ile timu wenye akili ni wawili ndio maana unaona hayo malalamiko.
Sasa tufanye lile halikuwa goli iweje sasa mpira ule uliposhindwa kuvuka mstari mchezaji wa mamelody aliutoa kwa kichwa iilikuwaje haikuwa kona?
 
Mashindano ya afcon nakumbuka victor osimeh aliangushwa ndani ya box mwamuzi akapeta tu kwa kuruhusu mpira uendelee ila baadae alipoona victor yupo chini tu akaenda kuangalia VAR
 
Ingepigwa kona,moyo wako ungeridhika?Tuache hizi lialia,tujipange kwa michuano ijayo!
Mwanzoni nilidhani unazungumzia uhalisia wa tukio lilivyoamuliwa bila ushabiki. Sasa mambo ya moyo kuridhika yanatoka wapi? Jibu tu je ni sahihi kufunika kona? Kitendo cha kutokuiona kona ni wenge waamuzi walilolipata baada ya kufanya maamuzi mabovu. Lines man kwanini hakufanya kazi yake?
 
Mashindano ya afcon nakumbuka victor osimeh aliangushwa ndani ya box mwamuzi akapeta tu kwa kuruhusu mpira uendelee ila baadae alipoona victor yupo chini tu akaenda kuangalia VAR
Ukirudi kwenye thread,hilo nimelielezea vema!
 
Una ushahidi gani kama maamuzi ya kukataa goli yalikuwa mabovu?
 
ALIYEKATAA BAO LA YANGA AITWA FIFA.

Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) limemteua refa Beida Dahane aliyechezesha mechi ya Mamelodi na Yanga, Ijumaa iliyopita kuchezesha mechi za soka za mashindano ya Olimpiki itakayofanyika Ufaransa kuanzia Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu.

Dahane (32) ni miongoni mwa marefa 12 kutoka Afrika ambao wamepata fursa hiyo huku kiujumla wakiteuliwa marefa 89 kutoka nchi tofauti duniani.

Marefa kutoka Afrika walioteuliwa kuchezesha Olimpiki mwaka huu ni walioteuliwa kuchezesha michezo ya Olimpiki mwaka huu ni Karboubi Bouchraw wa Morocco, Mahmood Ismail(Sudan), Diana Chkotesha(Zambia), Fatiha Jermoumi(Morocco), Elvis Noupue (Cameroon), Stephen Yiembe.(Kenya), Mahmoud Ashour (Misri), Lahlou Benbraham (Algeria), Ahmed Abdoulrazack (Djibouti), Emiliano Dos Santos (Angola) na Shamirah Nabadda Uganda).

Ijumaa iliyopita Dahane alizua mjadala baada ya kukataa bao la kiungo wa Yanga, Stephane Aziz Ki ambalo kwa mujibu wa baadhi ya picha za video na za mnato, mpira ulivuka wote mstari wa goli ingawa kwa uamuzi wa refa, haukuvuka wote.

Katika mchezo huo Yanga iliondolewa kwenye hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa penalti 3-2.
 
Refa aliumudu mchezo vizuri sana,tatizo watu wanaendeshwa kwa hisia na ushabiki zaidi!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…