Kama Tundu Lisu anashambulia na CCM ishambulie pia isipaki basi, ipande na kushuka kama timu

Kama Tundu Lisu anashambulia na CCM ishambulie pia isipaki basi, ipande na kushuka kama timu

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Haina sababu kumlalamikia Tundu Lisu kwa sababu ushindi ni mbinu na CHADEMA wameamua kutumia mfumo wa kumuweka mshambuliaji mmoja mbele na kujaza viungo kibao katikati.

Naiona CCM ikijaribu kupaki bus mbinu za Morinho ambazo zinaruhusu mashambulizi ili wewe uzuie tu na kupata sare.
Mbinu hii haina msaada hapa haitafutwi sare bali ushindi.

CCM ni lazima ishambulie, lazima iwaweke mbele watu wenye uwezo mkubwa wa kuchanganua mambo.
Watu wanaoweza kuelezea uchumi wa kati kwa lugha inayotafsirika kwa wananchi waongoze mashambulizi halafu akina kibajaj na musiba wawe wanalinda goli yule Tundu asije kuzifumania nyavu

Nawatakia tuesday yenye baraka.

Maendeleo hayana vyama!
 
CCM imefanya mashambulizi kwa karibu miaka yote mitano, huku ikimnyang'anya mwamuzi filimbi yake na kuwaondoa washika kibendera wote. Sasa imeamua kupaki basi ili kulinda ushindi uchwara.

Mbinu pekee iliyobakia kwa CCM sasa ni kuwatumia wasanii walevi na wavuta bangi, Pole Pole amesema mbinu hiyo inafaa na mkuu kaipenda sana.
 
Top management imejaa walimu hawaelewi hata maana ya uchumi ni nini? JK alikuwa ni mchumi akisimama unatamani kuongeza sauti ya radio usikilize nondo.
 
Mbona simpo tu,
Walizibwa midomo kwa miaka mitano, sisi tulizunguka na kuzungumza nchi nzima kwa miaka mitano!
Tunataka wabwabwaje vyote vilivyo kifuani hasira ziwapungue then tukiwasha moto mtajua kwa mini tulinyamaza kwanza!
Nchi hii raha sana, PHD ya Magu si ya mchezo mchezo!
 
Acha Tundu lissu Aendelee kupoteza mvuto na genge lake kwa kujitekenya na kuchekwa wenyewe.

CCM Ni Chama kikongwe kilicho komaa kisiasa subirieni siku kikiingiza kikosi uwanjani ndo mtaona Watanzania walivyo wanafiki kwa Tundu lissu.
 
Acha Tundu lissu Aendelee kupoteza mvuto na genge lake kwa kujitekenya na kuchekwa wenyewe.

CCM Ni Chama kikongwe kilicho komaa kisiasa subirieni siku kikiingiza kikosi uwanjani ndo mtaona Watanzania walivyo wanafiki kwa Tundu lissu.
Unafiki ndio siasa yenyewe bwashee!
 
Bora CCM tunyamaze tu kwani MATAGA wataishia tu kumponza JPM - maana nina uhakika watatamba "Wewe Lissu ukuda wako ndo maana tulikumiminia mvua ya risasi".

Itakuwa soo.

Wana CCM tunazijua vizuri sana akili za MATAGA!
 
Nyie si mnamshambulia pia, mumekodi viongozi wa dini na wasanii kuendeleza mashambulizi. Tulieni mkamuliwe majipu hayo mpone

FB_IMG_1596970740939.jpg
 
Back
Top Bottom