kifupi kirefu
JF-Expert Member
- Oct 29, 2018
- 539
- 3,507
Hii mikutano inayoandaliwa Kila Siku na Serikali inagharimu Fedha nyingi Sana za walipa Kodi. Lakini waudhuriaji ni watu walewale na wazungumzaji ni wale.
Dhima ya mikutano hii yote nikuwaaminisha wananchi kwamba Serikali Kuna Jambo inafanya Kwa ajili ya wananchi, wazungumzaji wote wanazungumza kauli tatu tu ambazo ni AMANI, MSAMAHA NA UMAHIRI WA KIONGOZI MKUU WA NCHI.
Unaweza kuona kama tupo sahihi lakini haya ni matumizi mabaya ya Fedha za umma. Ni mfumo mbovu wa wakubwa kujilipa fedha za umma. Vuta picha viongozi wakuu wa Nchi na vyombo vya ulinzi na usalama wanatumia kiasi gani kwa mafuta, malazi na posho za safari katika mkutano mmoja wa kiongozi wa Nchi kukutana na makundi?
Nani amewahi kuwaza kama Rais akiamua kutumia TBC na vyombo vya habari akazungumza na watanzania ataokoa kiasi gani? Viongozi wa kijamii, kidini na WA vyombo pamoja na wanasias wana majukwaa Yao yakuzumza huko walipo na wakamfikishia ujumbe Rais.
Marekani pamoja na utajiri wake hakuna mfumo huu wa Tanzania, China ambao niwafadhili wetu hakuna anayefanya haya, Afrika Kusini weusi wenzetu hakuna haya matumizi ya fedha; Sisi tunakusanya kidogo tunatumia kingi Kwa mambo yanayoepukika.
Nimwombe Mhe. RAIS afanye maamuzi magumu, apige gharama za mkutano mmoja anaofanya azidishe kqa mwaka apate jumla angetumia kiasi gani then hizo Fedha for remaining four years aziweke kwenye afya hasa ujenzi wa hospitali na zahanati TU.
Namwakikishia 2025 hakutakuwa na hoja ya afya kwenye kampeni. Lakini akiendelea na huu utaratibu madhara yake ni kwamba itafika 2025 hakuna sehemu ataomba kura Kwa sababu alikaa na viongozi wa Dini au machifu, ataomba kura Kwa kuwaonyesha wananchi amewafanyia Nini.
Siasa ni watu na ukitaka kufanikiwa bila kutumia Polisi na vyombo kuiba kura fanya maamuzi yakuachana kukaa na wanasiasa, viongozi wa dini na makundi mengine zungumza na Watanzania Kwa Umoja wao, zungumza na wananchi, jadili na wananchi. Hakuna mkutano wa ndani wa RAIS anaruhusiwa kuingia mlala hoi, ukitaka kuamini angalia hata aina ya machinga waliokuwa Ikulu.
Tupeleke Fedha kwenye miradi ya MAENDELEO tuachane na siasa zakukutana na watu ambao wanachokisema sicho wanachoamini, ukiondoka wote hao waliopo nyuma Yako unashangaa wanahamia Kwa aliyepo madarakani.
Huu ni mtizamo wangu, na hii inatokana na nilichokiona Leo. Viongozi wa Dini wamefarijika kukutana na Rais wakaacha kabisa kutumia jukwaa kumwakilisha Mungu