The Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 11,099
- 13,709
Tangu aingie madarakani, rais Samia Suluhu Hassan amekuwa na bifu na baadhi ya wanachama wenzake. Alianza na Job Ndugai spika wa zamani wa bunge letu. Baadaye, akafuatia Dk Bashiru Ally akiwakilisha kile kilichokuja kujulikana kama Sukuma gang. Juzi alianza bifu na Josephat Gwajima kidhabu aliyepewa ubunge na hayati Magufuli hatujui ni kimkakati au kikabila. Na sasa kuna bifu la wazi na Luhaga Mpina. Je hii inamnufaishaje Samia na chama chake au kuna mpango tusiojua? Je CCM inaonekana imeshikamana lakini ukweli ni vipande vipande kiasi cha kutegemea vyama nyemelezi na vya mfukoni kama ACT, CHAUUMA na vingine vingi? Hivyo, hawahofii chochote hata wakianza kutifuana kimitandao?