Kama ulikua huzijui haki zako ukikamatwa na POLICE wacha nikufahamishe

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,501
Reaction score
6,649
Kama ulikua huzijui haki zako ukikamatwa na POLICE wacha nikufahamishe;-
1751573823325.jpg
Watu wengi hawajui haki zao wakikamatwa na polisi,
Sasa kama huzijui haki zako ni hizo hapa;-

1). Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho, ni haki yako.

2). Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama,
Kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3). Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4). Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa,
Hata kwa kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5). Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6). Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7). Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8). Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9). Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10). Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11). Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12). Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13). Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14). Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15). Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16). Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17). Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18). Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19). Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20). Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21). Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22). Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

NB: Haki hizo utazipata nchi nyengine sio nchi ninayo ijua mimi.
 
Ahsante Kwa maelezo mazuri na ya kina kuhusu kukamatwa na polisi. Lakini Mimi nasema hivi, jitahidi usiingie mikononi mwa hao jamaa, na ikitokea umeingia, pambana Kwa akili zako kutokana na mazingira yalivyo, wale jamaa hawajui kutii haki zako na hauwezi kuwafanya kitu.
 
Hawa hawa wanao timba mahakamani wamefunika nyuso zao? Au hawa hawa ambao kumuuliza kitambulisho chake ni kosa la jinai?

Tanzania hii hii au ni kule cotswolds kwa kina dukes?

Anyway asante kwa Elimu
 
Kama ulikua huzijui haki zako ukikamatwa na POLICE wacha nikufahamishe;-
View attachment 3393153 Watu wengi hawajui haki zao wakikamatwa na polisi,
Sasa kama huzijui haki zako ni hizo hapa;-

1). Askari akikuweka chini ya ulinzi muulize kitambulisho, ni haki yako.

2). Askari akikukamata akuoneshe kitambulisho chenye muhuri wa mahakama,
Kama anasema ametumwa na mahakama kukumata, ni haki yako.

3). Askari akikukamata akwambie kwanini anakukamata na anakupeleka kituo gani, ni haki yako.

4). Unaruhusiwa na sheria kukataa kukamatwa,
Hata kwa kutumia nguvu kama hukuambiwa sababu ya kukamatwa.

5). Askari anapokiuka taratibu za ukamataji anageuka na kuwa mhalifu ni haki yako kujikinga naye.

6). Askari haruhusiwi kukuvuta shati, kukukaba koo, kukushika suruali kama hujakataa kutii amri halali.

7). Askari haruhusiwi kuondoka na mtu mwingine baada ya kumkosa mtuhumiwa halisi.

8). Askari haruhusiwi kupekua nyumba ya mtu bila kibali cha kupekua.

9). Askari lazima akuoneshe kibali cha kupekua na ukisome.

10). Kibali kieleze jina la aliyekitoa, kituo kilipotolewa,jina la mtu au sehemu ya upekuzi, au uchanganuzi wa mtu au sehemu.

11). Hairuhusiwi kupekuliwa usiku kuanzia saa 1 jioni mpaka saa 12 asubuhi.

12). Ni haki yako kumpekua askari kabla hajakupekua ili asipandikize kitu.

13). Usipekuliwa nyumbani bila kuwapo kiongozi wa mtaa.

14). Kila kitakachochukuliwa katika upekuzi lazima kiandikwe na askari aweke sahihi.

15). Mali iliyochukuliwa katika upekuzi lazima ibaki salama.

16). Mwanaume haruhisiwi kumpekua mwanamke na mwamke haruhisiwi kwa mwanaume.

17). Unaruhusiwa kukataa kupekuliwa iwapo taratibu hizi hazikufuatwa.

18). Askari haruhusiwi kukutukana wala kukupiga.

19). Unaruhusiwa kutozungumza lolote mpaka unayemuamini afike uwapo chini ya ulinzi, ni haki yako.

20). Usilazimishwe kuongea au kuandika ambacho hutaki, ni haki yako.

21). Usitoe maelezo bila uhakika yatatumika mahakamani yatakuletea shida.

22). Unaruhusiwa kukaa kimya na usizungumze kitu uwapo chini ya ulinzi.

NB: Haki hizo utazipata nchi nyengine sio nchi ninayo ijua mimi.
Labda kenya
 
Shida ni hili neno "JESHI LA POLISI" wao wanaamini kumkamata mtuhumiwa ni mapigano ya kimedani.

POLISI ni idara ya kiraia yenye kutoa ulinzi wa kadri na kudhibiti uhalifu kupitia utoaji wa elimu na mahakama.

Askari POLISI wa form four ( Div 4 ya 30) usitegemee akawa na Law enforcement strategies badala ya mabavu Ili kuziba udhaifu ( kufeli) yake.

Moja ya taasisi au idara iliyotakiwa kuwa na wasomi wengi hasa wajuzi wa Sheria ni POLISI .
Poor recruitment, poor officers!
 
Back
Top Bottom