Kama ulishawahi kunywa chai ya kuunguza Sukari tukutane hapa

Huku mikoani life hilo lipo mpaka kesho.
Kuna hii nyingine:
Kama kupika pilau unaona litakupotezea muda, pika wali wa kawaida wa maji, halafu vaa miwani ya jua. Hapo utakuwa unaona pilau.
Hapo ume solve rangi
vip kuhusu ladha.
 
Hiyo nimekunywa sana home miaka ya 1995/96
 
Nimejikuta nacheka kwanza, miaka ya 1997,98,99 tulikuwa tunaunguza sana sukari nyumbani
 
Afadhali hata wewe ulikuwa na sukari ya kuunguza, wenzio tulikuwa tunapasha maji ya moto tuuu. Halafu mguu barabarani, na leo tumemake
 
Mimi Chai zangu za rangisiwekagi majani,za maziwa pekee ndo naweka majani,nikajaribu leo kuunguza sukari jamani najuta chai mbaya,jamani mbaya hasa,mbaya sana najuta kwanza hata viungo vyangu havijasikika.
Nimekoma sirudii tena
 
Daah ebwana umenikumbusha mbali sana...kipindi hicho nikiwa chalii tu tunakaa maeneo ya Mikanjuni pale Tanga! Around 1990's mama amepika sana hiyo chai, and it was enjoyable enough!!!
 
Daah!umenikumbusha mbali sana enzi hizoo ukiona majani ya chai hayaonekani,nilishawahi Fanya huo mchezo,ukiiunguza unaweka maji chai tayari,nikiona nimeunguza nyingi natengeneza karatasi naimimina sukari niliyoiunguza kiasi inakuwa sukari gulu.[emoji39] [emoji39]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…