Kama ulishawahi kunywa chai ya kuunguza Sukari tukutane hapa

Kama ulishawahi kunywa chai ya kuunguza Sukari tukutane hapa

Zero IQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2016
Posts
13,959
Reaction score
24,935
Kwa wale wenzangu na mimi tuliowahi kunywa chai ya kuunguza sukari kama majani ya chai tukutane hapa.

Chai ile ilikuwa inatengenezwa kwa kuchukua Sukari unaiweka kwenye sufuria iliyopo motoni baada ya hapo sukari itayeyuka na kuungua kidogo alafu unachukua maji unaweka basi kitu kinakuwa Cheusi kama umeweka majani ya chai na ilikuwa tamu tu.

Kama ulishawahi kunywa hiyo chai kweli udogoni mwako au ata sasa hivi basi utakuwa umepitia maisha halisi ya mtanzania.

Tuambie hapa kama wewe ulishawahi kuinywa na inakukumbusha wapi kipindi hicho.!?

.
 
Chai sio rangi.
Chai ni majani ya chai.
Ukiunguza sukari unapata rangi inayofanana na ile inayopatikana ukiweka majan ya chai, basi tunajidanganya ni chai!

Aisee kama uliwah kunywa chai ya kuunguza sukari wewe ni MUHENGA !
 
Nkikumbuka hayo maisha sometime huwa machozi yanantoka tu.
Juzi kati majani ya chai yalikuwa yameisha ofisini kwetu so nkawaambia wale wafanyakaz wenzangu masista duu "chomeni sukari fasta tupate chai njaa znatuuma" huwezi amini hawajui kitu kuhusu hii sayansi....
Mama zetu walifanya kazi sana.
 
Mkuu we acha tu watu tunatoka mbali sana
 
Huku mikoani life hilo lipo mpaka kesho.
Kuna hii nyingine:
Kama kupika pilau unaona litakupotezea muda, pika wali wa kawaida wa maji, halafu vaa miwani ya jua. Hapo utakuwa unaona pilau.
 
Chai sio rangi.
Chai ni majani ya chai.
Ukiunguza sukari unapata rangi inayofanana na ile inayopatikana ukiweka majan ya chai, basi tunajidanganya ni chai!

Aisee kama uliwah kunywa chai ya kuunguza sukari wewe ni MUHENGA !
Sio uhenga wala nini kuna familia mpaka kesho wanatumia hiyo style
 
Ndio, ilikuwa sukari inaunguzwa inapatikana chai maridadi sana
kisha unapaka sabuni mwilini yaani mbadala wa mafuta
safari ya shule inaanza. Mimi mara moja moja huwa nafanya mpaka leo
Noma sana aseee
 
Back
Top Bottom