OMOYOGWANE
JF-Expert Member
- Dec 30, 2016
- 4,701
- 11,920
Habari wakuu!!
Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,
Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.
Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,
Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atakayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hakuna atakayehangaika na wewe,
Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zako ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipeleka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo Mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,
Haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gari zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,
Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo mitaani
Kijana kama wewe ni boda boda umeoa unawatoto na unarisha familia heshimu sana hiyo kazi
Mwenye macho na asome kisha atafakari
Nawasilisha.