Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Kazi nyingi za kuajiriwa siku ukiipoteza haupotezi kazi peke yake ila inapoteza na marafiki wote uliokutana nao kazini
Waheshimu sana marafiki uliokua nao kabla hujapata kazi usiwatenge hata baada ya kupata kazi kwakua wale ndo marafiki wa kweli siku ukiipoteza kaz utarud kuwatafuta tu , na wale marafik uliokutana nao kazin watakua wanakukwepa hata ukikutana nao njian na ukiwapigia sim hawatapokea au wakipokea stori inakua na mkatomkato anajua utampiga kizinga hata cha 10k au kumlilia njaa
Umenena vyema mkuu..

Hakuna mtu namheshimu kama anayenijua since nastruggle na sina kitu[emoji848]

Haya mambo ya kukutana kazini kila mmoja ana mchele wake tujenge urafiki huwa siyaentantain kabisa, koz najua ni unafiki tuu..
 
Ukweli mtupu,
Hawa walioajiriwa,ujanja na kutembea mbele ni kutokana na ajira walizo nazo,wakizipoteza,wanakuwa kama vichaa Bora hata sie ambao hatujawahi kuzipata hizo ajira,tumeishazoea maisha yetu ya kitaa,shahada na vyeti kapuni,tunapiga boda boda tu
Mbona sasa huu wivu mkuu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji23]
 
Kazi nzuri. Nikiona watu wa Dar wanaamka saa 10 za usiku kwenda kazini. Wanarudi nyumbani saa 4 za usiku. Mshahara laki 210,00 net pay. Kodi, ada za watoto, matibabu, chakula, wazazi wa mke wanaumwa wote wamekuja kutibiwa hapo kwako.
Unajiuliza nilimkosea nini Mungu, hupati jibu.
Haahaaahaa[emoji1787][emoji23][emoji23][emoji16][emoji16][emoji16]
 
Kazi nyingi za kuajiriwa siku ukiipoteza haupotezi kazi peke yake ila inapoteza na marafiki wote uliokutana nao kazini
Waheshimu sana marafiki uliokua nao kabla hujapata kazi usiwatenge hata baada ya kupata kazi kwakua wale ndo marafiki wa kweli siku ukiipoteza kaz utarud kuwatafuta tu , na wale marafik uliokutana nao kazin watakua wanakukwepa hata ukikutana nao njian na ukiwapigia sim hawatapokea au wakipokea stori inakua na mkatomkato anajua utampiga kizinga hata cha 10k au kumlilia njaa
Ukweli mtupu huu
 
Kazi nzuri. Nikiona watu wa Dar wanaamka saa 10 za usiku kwenda kazini. Wanarudi nyumbani saa 4 za usiku. Mshahara laki 210,00 net pay. Kodi, ada za watoto, matibabu, chakula, wazazi wa mke wanaumwa wote wamekuja kutibiwa hapo kwako.
Unajiuliza nilimkosea nini Mungu, hupati jibu.
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]
 
Hivi huwa ni kwanini mkuu? No love at all among staffs [emoji848]
Tatizo sio kwa hao mastaff bali tatizo ni kwa watu wenyewe.

Wewe ukihisi kwamba kila ambaye unaongea nae ni rafiki basi una matatizo, au ndio hawa wanadhani kwamba staff wenzao wanaongea na kucheka ni marafiki, hili ni kosa kubwa sana.

Tatizo sio staff bali tatizo ni hawa watu wenye fikra hizi
 
Habari wakuu!!

Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,

Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.

Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,

Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atalayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hskuna atakayehangaika nawewe,

Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zalo ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipereka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,

haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gali zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,

UMASIKINI HAUNA TOFAUTI NA MAKALIO YA MBWA!

Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo mitaani

kijana kama wewe ni boda boda umeoa unawatoto na unarisha familia heshimu sana hiyo kazi

Mwenye macho na asome kisha atafakari

Nawasilisha.
Kiongozi imekuaje tena mpaka ukaja na mada kama hii 😀😀😀
 
Back
Top Bottom