Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Habari wakuu!!

Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,

Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.

Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,

Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atakayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hakuna atakayehangaika na wewe,

Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zako ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipeleka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo Mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,

Haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gari zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,

Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo mitaani

Kijana kama wewe ni boda boda umeoa unawatoto na unarisha familia heshimu sana hiyo kazi

Mwenye macho na asome kisha atafakari

Nawasilisha.
Kweli kabisa, kuacha kazi ni rahisi mno, kupata tena ni kivumbi..
 
Mazingira yanadumaza fikira haswa, watanzania tumedumaa sana, yaani unasema hata kama unapata 3000 kwa siku ambayo haitoshi, inaishia kula tu na wakati mwingne isitoshe, unaishia kukopa mpaka basi lakini bado unashauri mtu asiache aganganie mpaka kufa kwake. Kwani akiamua kupambana na kujiajiri mwenyewe kwa nguvu zote unafikiri hatafanikiwa? uvivu wa kufikiri na woga ndio unapelekea useme yote hayo na kuiona ajira ndoo kila kitu.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app

Asante! ajira ni utumwa kazi siyo lazima uwe umeajiriwa kazi ziko nyingi za kujiajiri na unaweza toboa na kujiona muda uliotumia kuajiriwa ulipoteza. Huko tunaoenda tusiwaaminishe watoto wetu kuwa ukisoma lazima uajiriwe mwambie soma ujiajiri.
 
Mkuu we umejiajiri
 
Huo Ni uoga mkubwa na kushindwa kuwaza nje ya box.

Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,

Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.

Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,

Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atakayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hakuna atakayehangaika na wewe,

Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zako ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipeleka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo Mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,

Haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gari zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,

Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo m

[/QUOTE]hizi Ni habari zinakuhusu wewe na waoga wenzio wa maisha
 
Hakuna maisha matamu kama ya kujiajiri...Mimi nina miaka6 sasa sijui nini maana ya kuajiriwa na sijawai kulala na njaa....kuajiriwa ni utumwa
 
Unahamasisha watu waendelee kuwa watumwa kwa kuajiriwa? Jiajiri mtoto wa kiume acha utumwa!
 
Kazi nyingi za kuajiriwa siku ukiipoteza haupotezi kazi peke yake ila inapoteza na marafiki wote uliokutana nao kazini
Waheshimu sana marafiki uliokua nao kabla hujapata kazi usiwatenge hata baada ya kupata kazi kwakua wale ndio marafiki wa kweli siku ukiipoteza kazi utarudi kuwatafuta tu , na wale marafiki uliokutana nao kazini watakua wanakukwepa hata ukikutana nao njian na ukiwapigia simu hawatapokea au wakipokea stori inakua na mkatomkato anajua utampiga kizinga hata cha 10k au kumlilia njaa
Ndo maana sipendi marafiki wa unipendea kwenye neema tu ...
 
Ukweli mtupu,
Hawa walioajiriwa, ujanja na kutembea mbele ni kutokana na ajira walizo nazo, wakizipoteza, wanakuwa kama vichaa Bora hata sie ambao hatujawahi kuzipata hizo ajira, tumeishazoea maisha yetu ya kitaa, shahada na vyeti kapuni, tunapiga boda boda tu
Haaaahaaaaa
 
Mission town ni wizi ulipachikwa jina lenye staha!

Ni kama vile tu rushwa ilivyopewa jina la ' takrima ' na wana ccm kipindi fulani.

Ukimuona mtu anajinasibu kwa jina la mission town kaa nae mbali futi nyingi sana maana jela ni muda wowote
Haha hahaa...afu kweli
 
Habari wakuu!!

Huu ni ushauri kwa watu wote waliopo kwenye ajira sehemu mbali mbali serikalini au makampuni binafsi n.k,

Haiijarishi wewe ni polisi, mwanajeshi, Mwalimu, daktari, mhasibu, sekretari, mwandishi wa habari, kiongozi wa kisiasa, Modetator JF n.k hata kama unalipwa elfu moja kwa siku, heshimu sana kazi yako na ipende kama unavyompenda mke wako au watoto wako.

Siku ukipoteza hiyo kazi sio ajabu kujikuta unapoteza na vitu vingine vya muhimu kama vile mke, heshima, marafiki ndugu hata biashara uliyoamua kuianzisha nayo ikafa kifo cha mende,

Hakuna watu wanafiki kama walio maofisini, hakikisha hupotezi kazi baki huko huko na wanafiki wenzio maana siku utakapopoteza kazi hakuna atakayehangaika na wewe hapo ofisini kwako ulipo sasa ama huko utakakokuwa unapereka vyeti na CV zako narudia tena hakuna atakayehangaika na wewe,

Siku ukitaka kujitolea watapokea CV zako ulizotype na kuprint kwa pesa ya msaada kama umezipeleka private watakuambia watakupigia simu na hiyo ndio bye bye, kama ni serikalini hayupo Mkurugenzi, au mkuu yeyote atakayehangaika na makaratasi yako yatawekwa kwenye faili yaungane na barua za wenzako za mwaka juzi ambazo hazijajibiwa,

Haijarishi unalipwa laki moja au mbili kwa mwezi, haijarishi unalipwa mamilioni, haijarishi unatembea kwenye gari zuri la serikali au kampuni, nguvu uliyonayo sasa ndiyo inayokufanya uheshimike na kuchangamkiwa unapokwenda kikazi kwenye taasisi zingine,

Wasio na kazi au ajira hawajapenda au kutaka wawe hivo bali ni competition kali iliyopo mitaani

Kijana kama wewe ni boda boda umeoa unawatoto na unarisha familia heshimu sana hiyo kazi

Mwenye macho na asome kisha atafakari

Nawasilisha.
Mawazo ya kimasikini haya, ndio maana serikali yenu inawachezea sana. Mnakalishwa miaka kadhaa bila ongezeko la mishahara sababu ya uwepo wa wajinga kama ninyi.
 
Back
Top Bottom