Kama umeajiriwa sehemu yoyote shika sana kazi yako hakikisha huipotezi, ukiipoteza utajuta

Mazingira yanadumaza fikira haswa, watanzania tumedumaa sana, yaani unasema hata kama unapata 3000 kwa siku ambayo haitoshi, inaishia kula tu na wakati mwingne isitoshe, unaishia kukopa mpaka basi lakini bado unashauri mtu asiache aganganie mpaka kufa kwake. Kwani akiamua kupambana na kujiajiri mwenyewe kwa nguvu zote unafikiri hatafanikiwa? uvivu wa kufikiri na woga ndio unapelekea useme yote hayo na kuiona ajira ndoo kila kitu.

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
 
Tatizo linaanza hapo kwenye kutaka kujiajiri mwenyewe, huo mtaji unatolea wapi?
 
Acha kutisha watu Kila kitu kinatokea kwa sababu wapo wanaojuta kupoteza kazi vilevile wapo wanaofurahi maamuzi ya kuacha kazi kubase upande mmoja maana yake umeyawekea mawazo yako mipaka.
 
Mwenye maskio na askie ujumbe wako wa dhati. Thawabu zikurejee kwa kutenga mda kuandaa ujumbe mchungu lakini wa ukweli na wenye faida hasa.
 
kuajiriwa ni UTUMWA kasoro minyororo.
Jiajiri ili ufurahie maisha na familia yako.
kuajiriwa ni stresss.
 
Mkuu kwa hiyo tusiweke tumaini letu kwa Mungu Mwenyezi, bali tuweke kwenye kazi, au mimi ndo sijakuelewa.....
 
Mentality ya Kuajiriwa naona ndio inatuweka kuwa watumwa,....sisemi kuwa kuajiriwa ni kubaya la hasha. Nasema, unaajiriwa na kuanza mchakato wa kuangalia mbele baada ya miaka kadhaa malengo yangu ni yapi? Kwenye kuajiriwa kuna fanya mwaajiriwa kutofikiri nje ya Box, kwa maana kua anaangalia mwisho wa mwezi atapata mshahara, hata kama hautoshi(Na hautatosha maisha yote), yeye atajituma muda woote kufanya kazi ya kuajiriwa!

Sasa basi, suluhisho ni, tumia kazi ya kuajiriwa kama ngazi ya kuanza kujijenga, ukitumia kipato cha kazini, anza kuchukua mkopo wa kuanzisha kijibiashara.....usianze biashara kubwa, anza kitu kidogo kama hata kibanda cha kuuza vocha na soda. baada ya kumaliza mkopo huo, biashara inakua yako na ndio faida......chukua mkopo mwengine, anzisha biashara nyengine, hata kinyozi na kuendelea.

Baada ya miaka michache, utakuta umekua mjasirimali na vibiashara kadhaa. Anza kulea na kuboresha hizo biashara.
Itafika wakati, hizo biashara zako zinakupa zaidi ya mshahara............hapo sasa ndio unaweza kuachia pole pole huo utumwa.

Tatizo wafanyi kazi wengi huanza na kuchukua deni kununua gari...kujenga nyumba, kununua makochi..na kadhalika!

Kuajiriwa ni Slavery ndungu zangu.........mimi ni muajiriwa, lakini, ningepata ushauri mapema, ningekua Muajiri kwa sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…