Kujiajiri kunahitaji moyo, uvumilivu na maono ya kutosha
Mtaji sio pesa tuu, bali ni muda,watu, connection pia elimuā¦
Vijana wengi huwa tunafeli pale kwenye muda na watu connection zinakuja baadae
Muda:
Muda wa uvumilivu, muda wa kujenga jina la biashara na kuijua biashara au kupata uzoefu, kujua njia na watu.
Watu:
Watu sahihi kwenye biashara ambao unaweza kupata ushauri, kujifunza, ku runa nao mission kukushika mkono.
Wateja eneo sahihi au watu sahihi lengwa wa biashara.
Connection:
zinakuja pale utapokuwa ume hit watu sahihi na wakati /muda sahihi.
Elimu:
Sio ile ya darasani tuu , kuna muda ukiingia kwenye kujiajiri kuna elimu unakutana nayo ambayo iko tofauti na ile ya darasani au inakataa ile ya darasani, sasa haoa unakuta wasomi wengi tunaanzaga kuchanganyikiwa tuna force mavitabu kumbe field iko tofauti, kuna muda inabidi ujishushe uwe kama wao ili ujue yale ya ile level yao halafu unakuta kuongezea zako za darasabi inakuwa rahiiisi.
Tutaendelea siku nyingine