LGE2024 Kama umekuta kituo cha Kuandikisha Wapiga kura hakina Wakala wa Chadema Toa Taarifa kupitia uzi huu, nitafikisha kwa Wahusika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Ni aibu kubwa Chama kinachotaka kushika Dola kwa hayo unayoyasema.
Yani uongozi hauna namna ya kujua hilo mpaka wasaidiwe na mtu kupitia uzi wa Jamiiforums.
Hiki chama kiko serious kweli? Hapana bado sana, kama tu kinashindwa kujisimamia nchi hawatoiweza.
Sasa siku zote hizo mlikuwa mnajiandaa na nini?
 
Server itajaa. Huku kwetu tandahimba tunajua chama cha nyerere tu.
 
CHADEMA HAWATAKI VIJANA WAJIANDIKISHE, JE WANAWAOGOPA KWENYE UCHAGUZI?

Sauti za Chadema sasa zinapaza malalamiko yasiyo na mashiko, wakidai kwamba Tume ya Uchaguzi (NEC) inaandikisha wanafunzi kwa lengo la kuwaandaa kupigia kura CCM. Ukweli ni kwamba, kila kijana mwenye miaka 18 ana haki ya kikatiba kujiandikisha na kupiga kura.

Hii siyo mbinu ya kisiasa bali ni utekelezaji wa sheria, kwani vijana waliozaliwa mwaka 2006, wakiwemo wa umri wa miaka 17 mwaka huu, watafikisha miaka 18 ifikapo mwakani. Je, Chadema wanataka kuwanyima haki zao kikatiba?

Chadema wanatakiwa kuelewa kuwa kila aliyeandikishwa ameonesha kitambulisho kinachoonesha umri wake halali. Kuibua tuhuma za "kuandikisha watoto" bila kutoa ushahidi wa vitambulisho ni mbinu ya kisiasa ya kutengeneza mazingira ya kujiondoa mapema au kutafuta kisingizio endapo watashindwa tena mwakani. Tumeona mbinu kama hizi mara kadhaaβ€”wakishindwa, hukimbilia kusema "tulibambikiwa."

Nani anaweza kuwazuia vijana wenye ari na shauku ya kushiriki kikamilifu katika uchaguzi? Hili si swali la wafuasi wa CCM bali ni ishara ya hofu ndani ya Chadema, wakijua kuwa kizazi cha sasa kinatambua haki zake na hakitadanganywa kirahisi. Wanapojaribu kupinga ushiriki wa vijana, wanaonesha wazi kuwa hawataki sauti za kizazi kipya zisikike.

Kwa kifupi, malalamiko ya Chadema si hoja ya msingi bali mbinu ya kuwatisha vijana na kuwapotezea imani katika mchakato wa uchaguzi. Uchaguzi si mchezo wa kuigiza bali ni nafasi ya kila raia, awe kijana au mzee, kuamua hatma ya taifa kupitia sanduku la kura.

Kama Chadema wana hofu ya kushindwa, basi wanapaswa kujipanga na kuja na sera bora badala ya kutengeneza visingizio visivyo na msingi.
 
Eneo langu ninalokaa huku,hakuna cha wakala wa CCM wala CDM
Ni anaye andikisha Peke yake,nimecheki kama sehemu tatu hivi
 
Hapo CCM ni kujipakulia tu minyama
 
Sawa mkuu tumekuelewa.

Nukuu ya baba wa taifa.
""UTII UKIZIDI SANAA HUZAA UOGA, UOGA UKIZIDI SANA HUZAA UNAFIKI NA KUJIPENDEKEZA NA MWISHO WAKE NI MAUTI""
 
Arusha
Kata ya Osunyai, mtaa wa Jr kituo cha kwa Jumanne, msikitini hakina wakala wa Chadema
 
Sasa nini mnachoweza ndugu zangu Chadema
Embu jitahidini kuwa serious Basi
Mlitakiwa muwe na pdf ya Vituo vyote mpaka Sasa hivi
Na wanachama wenu Kila Eneo

Chama kinajengwa kutolea chini sio kurusha chopa hewani

Bado naamini Bado mnaweza kwa miaka ya mbele na baada ya kubadilisha Safa ya uongozi ilifanya kazi kubwa Ila imeshachoka vibaya sana
 
Hujaelewa, hatusemi Chadema haina Mawakala, tunachotaka kujua ni kama kuna changamoto yoyote hapo walipo au kama hawapo tuambiwe
 
Hujaelewa hoja yetu
 
Kama hakibabaiki kwanini mmeanza figisu?
 
Ukitaka maendeleo wapeleke chadema ndio wanaokusanya kodi ewe mtafiti?
 
una buku teni hapo nitumie nikwambie wap hakuna wakala na kila kituo nitakacho kutajia teni vipo 20
 
Ukitaka maendeleo wapeleke chadema ndio wanaokusanya kodi ewe mtafiti?
chadema ni matajiri wa mihemko na malalamiko tu gentleman, hakuna wanachoweza zaidi ya hapo...

viongozi wao sasa 🀣
moja ni kibaraka ombaomba, na mwingine anakunywa huyo dah!πŸ’

wanachama wao wananatukana hao aiseee...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…