LGE2024 Kama umekuta kituo cha Kuandikisha Wapiga kura hakina Wakala wa Chadema Toa Taarifa kupitia uzi huu, nitafikisha kwa Wahusika

LGE2024 Kama umekuta kituo cha Kuandikisha Wapiga kura hakina Wakala wa Chadema Toa Taarifa kupitia uzi huu, nitafikisha kwa Wahusika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Yeyote aliyeona Kwenye Kituo chochote Tanzania labda Hakuna Wakala wa Chadema, Basi atoe Taarifa kupitia Uzi huu (Siyo PM), Mimi nitawasiliana na Viongozi wa Chadema kwa njia mbalimbali na kuwapa Taarifa haraka iwezekanavyo.

Au kama umemkuta Wakala wa Chadema ana shida yoyote kituoni hapa, iwe fedha au Chakula lete Taarifa hapa hapa tutawajulisha Viongozi wake haraka.

Chadema ina zaidi ya Wanachama mil 15 walio hai Nchi Nzima(Kwa mujibu wa Chadema Digital), ,hakuna sababu yoyote ile ya kukosa Wakala popote pale, na wala hakuna sababu yoyote ya Wakala wao kukosa hela au Chakula.

Soma Pia:
Ikumbukwe kwamba hii siyo Special Thread, Ni uzi tu mfupi kwa ajili ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa, Na wala kutoa Taarifa kama hizi siyo Kosa Kisheria, hivyo huna haja ya kuogopa chochote, Usikalie Taarifa.

Nakala: Boniface Jackob, Mwenyekiti Kanda ya Pwani
Sidhani kama kuweka wakala kunasadia chochote kwasababu hivyo vitabu wanachapa wao waandikishaji wamewaajiri wao sasa wakitaka kufanya chochote wanaweza wakafanya. Kitu kikubwa ninachokiona uchaguzi huu hauna mwamko kabisa kwa upande wavijana waupinzani ukilinganisha na uchaguzi wa 2014/2015 na 2019/2020 vijana wamekatishwa tamaa sana na mambo ya hovyo ambayo yamefanywa na wagombea wa upinzani kukubali kununuliwa wakati vijana waliwapigania mpaka wengine kuuwa nakufungwa magerezani. Upinzani unapaswa uwahakikishea wananchi kuwa hili kama siyo daraja la wao kujipatia umaarufu na mitaji.
 
Tanzania nzima vituo vya kuandikisha wapiga kura havina mawakala wenu
Mmechelewa sana ccm mawakala wao ni walimu posho imetembea mno
Je nyie mawakala wenu mnawapa nini au wanajitolea tu? Tengeni mafungu kabla kuingia kwenye mambo kama haya enzi za kujitolea zimepitwa na wakati
Poleni
Mawakala wa ccm ni walimu! Wanalipwa na serikali! Kupitia kodi ztu!? No wonder... !!
 
Back
Top Bottom