LGE2024 Kama umekuta kituo cha Kuandikisha Wapiga kura hakina Wakala wa Chadema Toa Taarifa kupitia uzi huu, nitafikisha kwa Wahusika

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
kwa hili jibu lako unafikiri ikiwa chama chako kinashindwa kuwajibika kwa vitu tu vidogo hivyo itakuwaje wakipewa nchi,wataweza kutatua changamoto zakitaifa...?
Kwanza Uzi huu hausemi Viongozi wameshindwa, lengo ni kujaribu kutatua changamoto tu
 
Mh! kwanini hao mawakala wenu wasiwasiliane wao na uongozi mahali husika mpk wasemewe!,na vipi mahali husika viongozi wenu kwani wanakuwa hawajui kuwa kuna mawakala hivyo watahitaji uangalizi...??
Tatizo la CHADEMA hawajielewi. Hivyo tu inatosha Mimi kutowapa kura yangu
 
Yeyote aliyeona Kwenye Kituo chochote Tanzania labda Hakuna Wakala wa Chadema, Basi atoe Taarifa kupitia Uzi huu (Siyo PM), Mimi nitawasiliana na Viongozi wa Chadema kwa njia mbalimbali na kuwapa Taarifa haraka iwezekanavyo.

Au kama umemkuta Wakala wa Chadema ana shida yoyote kituoni hapa, iwe fedha au Chakula lete Taarifa hapa hapa tutawajulisha Viongozi wake haraka.

Chadema ina zaidi ya Wanachama mil 15 walio hai Nchi Nzima(Kwa mujibu wa Chadema Digital), ,hakuna sababu yoyote ile ya kukosa Wakala popote pale, na wala hakuna sababu yoyote ya Wakala wao kukosa hela au Chakula.

Soma Pia:
Ikumbukwe kwamba hii siyo Special Thread, Ni uzi tu mfupi kwa ajili ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa, Na wala kutoa Taarifa kama hizi siyo Kosa Kisheria, hivyo huna haja ya kuogopa chochote, Usikalie Taarifa.

Nakala: Boniface Jackob, Mwenyekiti Kanda ya Pwani
Acha kuchafua hali ya hewa ,chadema ndio mdudu gani hapa nchini?
 
Mh! kwanini hao mawakala wenu wasiwasiliane wao na uongozi mahali husika mpk wasemewe!,na vipi mahali husika viongozi wenu kwani wanakuwa hawajui kuwa kuna mawakala hivyo watahitaji uangalizi...??
Katani kwangu hata Hao wanachama wenyewe hawapo.Tatizo mnapeana matango pori kwa kujidanganya kuna wanachama kila Kona wakati kiuhalisia icho kitu hakipo. Ruksa kunikosoa
 
Yeyote aliyeona Kwenye Kituo chochote Tanzania labda Hakuna Wakala wa Chadema, Basi atoe Taarifa kupitia Uzi huu (Siyo PM), Mimi nitawasiliana na Viongozi wa Chadema kwa njia mbalimbali na kuwapa Taarifa haraka iwezekanavyo.

Au kama umemkuta Wakala wa Chadema ana shida yoyote kituoni hapa, iwe fedha au Chakula lete Taarifa hapa hapa tutawajulisha Viongozi wake haraka.

Chadema ina zaidi ya Wanachama mil 15 walio hai Nchi Nzima(Kwa mujibu wa Chadema Digital), ,hakuna sababu yoyote ile ya kukosa Wakala popote pale, na wala hakuna sababu yoyote ya Wakala wao kukosa hela au Chakula.

Soma Pia:
Ikumbukwe kwamba hii siyo Special Thread, Ni uzi tu mfupi kwa ajili ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa, Na wala kutoa Taarifa kama hizi siyo Kosa Kisheria, hivyo huna haja ya kuogopa chochote, Usikalie Taarifa.

Nakala: Boniface Jackob, Mwenyekiti Kanda ya Pwani
Kwa hiyo ndg unatutaka tukifika kwenye kujiandikisha lazima tuulizie kwanza wakala wa CDM kama yupo!? Na kama hayupo tukupe taarifa au siyo!!??
 
Huu ni mwanzo tu bado wagombea sidhani kama wataweka wagombea nchi nzima
Kama wameshindwa kuweka wakala mmoja tu kwa kituo je kuweka watu sita kugombea nafasi sita za uongozi wa mtaa katika kila mtaa nchi nzima wataweza?

Watanganyika ni wanafiki sana hao mnaosema wanachama milioni 15 nadhanu si halisi ni opportunists ambao wana kadi za vyama zaidi ya kimoja. Mngekuwa na wanachama effective hata milioni mbili t.u nchi mngeitikisa..

Ifike mahali sharti la kuwa mwanachama mtu awe na kadi ya kupigia kura ndipo aruhusiwe kuwa mwanachama.
 
Kwa hiyo ndg unatutaka tukifika kwenye kujiandikisha lazima tuulizie kwanza wakala wa CDM kama yupo!? Na kama hayupo tukupe taarifa au siyo!!??
Una haki ya kuuliza kuhusu mawakala wa vyama
 
Tanzania nzima vituo vya kuandikisha wapiga kura havina mawakala wenu
Mmechelewa sana ccm mawakala wao ni walimu posho imetembea mno
Je nyie mawakala wenu mnawapa nini au wanajitolea tu? Tengeni mafungu kabla kuingia kwenye mambo kama haya enzi za kujitolea zimepitwa na wakati
Poleni
Nimeona kwa macho yangu kabisa wakati na jiandikisha mawakala wa CCM wanaulizwa wale wa ugali ngapi na wale wa wali ngapi!? Nikatania kidogo nami niagize nikaambiwa poa agiza,sema wife akasema tuondoke, la sivyo ningekua peke yangu kipunga cha CCM ninge kipiga live!! CDM hata karibu hawana!!
 
Yeyote aliyeona Kwenye Kituo chochote Tanzania labda Hakuna Wakala wa Chadema, Basi atoe Taarifa kupitia Uzi huu (Siyo PM), Mimi nitawasiliana na Viongozi wa Chadema kwa njia mbalimbali na kuwapa Taarifa haraka iwezekanavyo.

Au kama umemkuta Wakala wa Chadema ana shida yoyote kituoni hapa, iwe fedha au Chakula lete Taarifa hapa hapa tutawajulisha Viongozi wake haraka.

Chadema ina zaidi ya Wanachama mil 15 walio hai Nchi Nzima(Kwa mujibu wa Chadema Digital), ,hakuna sababu yoyote ile ya kukosa Wakala popote pale, na wala hakuna sababu yoyote ya Wakala wao kukosa hela au Chakula.

Soma Pia:
Ikumbukwe kwamba hii siyo Special Thread, Ni uzi tu mfupi kwa ajili ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa, Na wala kutoa Taarifa kama hizi siyo Kosa Kisheria, hivyo huna haja ya kuogopa chochote, Usikalie Taarifa.

Nakala: Boniface Jackob, Mwenyekiti Kanda ya Pwani
 
Unaomba msaada, unapewa msaada alafu unakataa huo msaada!

Sasa kama si kweli, huu uzi una maana gani?

Ulichotakiwa kufanya ni kuomba ufafanuzi ili uweze kufanyia kazi taarifa husika maana wewe haupp tanzania nzima

Unaweza kuja na list ya vituo vyenye mawakala wenu Tanzania nzima na ukaomba wanachama wawasaidie kama hakutakuwa na wakala wawape taarifa ili mchukue hatua

Ukijaza ubishi kichwani na mashindano plus ujuaji, sidhani kama huu uzi utafikia lengo
 
Tujitahidi kujikita kwenye hoja, uzi umejieleza vizuri mno, malumbano ya nini tena?
 
Mkuu hali sio shwari kabisa nahisi viongozi wa kata na majimbo wanakula hizo hela za posho. Maana kata ya Makumbusho tu hali ni mbaya jana kuna kiongozi wa jimbo alijitolea 22k nashangaa Kiongozi wa kata anapika chakula kwake na kuanza kusambaza kwenye vituo tena saa 9 alasiri hapo Wakala kakaa toka asubuhi hajanywa hata chai. Hiyo ni Makumbusho je huko Uvinza, Luangwa, Msoga hali ikoje?
Haya mambo ni lazima myafanyie u serious sasa kama serikali za mitaa hivi je uchaguzi mkuu utakuwaje?
 
Back
Top Bottom