Yeyote aliyeona Kwenye Kituo chochote Tanzania labda Hakuna Wakala wa Chadema, Basi atoe Taarifa kupitia Uzi huu (Siyo PM), Mimi nitawasiliana na Viongozi wa Chadema kwa njia mbalimbali na kuwapa Taarifa haraka iwezekanavyo.
Au kama umemkuta Wakala wa Chadema ana shida yoyote kituoni hapa, iwe fedha au Chakula lete Taarifa hapa hapa tutawajulisha Viongozi wake haraka.
Chadema ina zaidi ya Wanachama mil 15 walio hai Nchi Nzima(Kwa mujibu wa Chadema Digital), ,hakuna sababu yoyote ile ya kukosa Wakala popote pale, na wala hakuna sababu yoyote ya Wakala wao kukosa hela au Chakula.
Soma Pia:
Ikumbukwe kwamba hii siyo Special Thread, Ni uzi tu mfupi kwa ajili ya Uchaguzi wa serikali za Mitaa, Na wala kutoa Taarifa kama hizi siyo Kosa Kisheria, hivyo huna haja ya kuogopa chochote, Usikalie Taarifa.
Nakala: Boniface Jackob, Mwenyekiti Kanda ya Pwani