Kama umenunua Bajaji ya Milioni 20 ili upewe 20k kwa siku basi unafanya biashara kichaa

Nilitaka kumpinga mleta mada ila baada ya hesabu nimegundua ni ufala kweli.hata kwa mwaka mtaji haurudi huku bajaji yenyewe ndani ya mwaka tu inakuwa hoi bin taabani, ikizingua ukaamua kuipeleka chuma chakavu hata laki 5 hazifiki.
 
Kila biashara inalipa UKIHADITHIWA.
Cha kushauri ""INVEST IN YOUR HOBBY""

Mi binafsi kilimo na ufugaji Hapana.

Nilikuwa na mashamba kibao ila nimeuza yoteee, SIFIKIRII TENA KURUDI KWENYE KILIMO NA UFUGAJI.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
Shida ya kilimo na ufugaji ni uache vyote ufuate msalaba.

Maana yangu kama utalima na kifuga iwe hivyo usifanye mambo mengine, huoni wamasai hata shule hawaemdi na wanaoenda hawafugi.
 
Shida sio vijana tuu wa kitanzania hili ni janga la watanzania utakuta Mzee kapambana kweli kutafuta pesa kwa shida kajinyima mbaya alafu utawakuta baba, mama na mtoto wameenda wote kununua pikipiki tena kwa furaha bila kujua ni janga gani baya wamelikaribisha kwenye familia Yao.

Angalia wanasiasa wetu ni wazuri kuchota pesa ila hutosikia wanamiliki biashara kubwa Zaid ya nyumba ya kupanga.

Kuna mama mmoja nimemuona hazimo kabisa yeye na washauri wake yan ashakuwa waziri kwenye serikali kadhaa kipindi hiki kawa balozi eti akaacha ofisi ya ubalozi wazi kaenda kuomba vitu maalum kwenye kile chama kwa akili hizi unafikir Tanzania itakuwa taifa imara kweli
 
Sasa na invest vipi kwenye hobby ya kusasambua mbususu?
Pitia hii 👇👇👇


#YNWA
#YANGA_BINGWA
 
Kila biashara inalipa UKIHADITHIWA.
Cha kushauri ""INVEST IN YOUR HOBBY""

Mi binafsi kilimo na ufugaji Hapana.

Nilikuwa na mashamba kibao ila nimeuza yoteee, SIFIKIRII TENA KURUDI KWENYE KILIMO NA UFUGAJI.

#YNWA
#YANGA_BINGWA
We mzee uliuza mashamba kumbe. Ulinishawishi nitaenda uko Mungu akijaalia.
 
Nilitaka kumpinga mleta mada ila baada ya hesabu nimegundua ni ufala kweli.hata kwa mwaka mtaji haurudi huku bajaji yenyewe ndani ya mwaka tu inakuwa hoi bin taabani, ikizingua ukaamua kuipeleka chuma chakavu hata laki 5 hazifiki.
Chuma chakavu hata 50 haifiki
 
kununua chombo cha moto! na kumpa mtu akuletee hesabu, ni ujinga,upumbavu,uzembe,uvivu wa kufikiri na ufujaji wa mtaji. ni masikini wa AKILI tu, ndio anaweza kufanya upumbavu huo.
Sasa tuambie wewe kwenye transportation industry inabidi uendeshe vyombo vyote vya ya moto? 😁😁

Biashara nyingi za mitaji ya 10M faida yake hata ikitofautiana na bajaji ni kidogo sana. Risk ni biashara zote na ukiogopa risk sjui utafanya biashara gani
 
Aisee Kuna Mawzo ya wadau huku inabidi mtu ucheke tu.

But si ndio Uwekezaji huo wazee au inakuaje?
 
Kwa mawazo ya wengi humu biashara zote ni kichaa tu.

Lodge,Apartments,Duka etc huwezi kurudisha mtaji wako kwa mwaka!

Either ni mawinga/madalali,machinga au jobless wanaoishi kwa shemeji zao.
 
Mtoa mada anataka aaminishe watu kuwa makampuni yanayotoa bajaji za mkopo yana haki ya kukopesa bajaji na kupata riba ya asilimia 100

Anatetea makampuni kumnyonya mwananch kiwango cha juu, tena anajaribu kusema kuwa mwananchi anayeenda kuchukua bajaji ya mkopo anafaidika kuliko kampuni na ni uongo wa kiwango cha juu sana

Serikali aisemi chochote; ukweli ni kwamba makampuni ya kukopesha bajaji yanambana sana kijana anayekopa bajaji kwa riba isiyo rafiki
 
Kila mwenye hela yake afanye anachopenda!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…