Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Na anaesema hakuna uchawi jua hayajamkuata
Miee mpaka kupona nlizurura mnooo
Na nikajionea mengi aiseee ya kushangaza
Na kiukweli kupitia tukio hiloo kiasi nliongeza ufaham kuhusu hii dunia tunayoishii
Me kuna mshkaji wangu yeye alikuwa ikifika siku ya mtihani tu anaumwaa hoii... Yani kitu kinaitwa mtihani hapatani nacho... Karudia madarasa mpaka necta wakasema aisee inatosha kufanya mitihani ya taifa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bei gani babe tuinunue nataka tuishi huko.
 
Da mkuu umezingua kinoma yani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu tiririka mlivyojiongeza!
 
Mkuu wewe una uwezo wa asili Kama Mimi pia hizo ndoto unitokea mara kwa mara.
Katika kufuatilia nikaambiwa kwamba hao ni mizimu ndio hutoa msaada Kama huo wa kukuonesha wabaya wako na sio akili yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee! Mimi ninachojua niliambiwa babu yangu alikuwa mtu wa dini sana! Alifika tu mkoa fulani, akaoa na akafia hapo. Hawajui ni wapi alipotokea na sijawahi kumuona! Ajabu hata picha hakuwahi kupiga! Baadhi ya ndugu waliyomuona babu akiwa hai wakimuota wanamuona amesimama huku nyuma yake kukiwa na nyumba inang'aa sana.
 
Me ktk maisha yangu nimeshuhudia mambo mengi sana ya kichawi ingawa mengine ni katka ndoto lakini yalikua na uhalisia

Ila tukio ambalo siwezi kusahau ni ktk hizi nyumba za kupanga ambapo nilipanga na mmama mmoja hivi wa kiha kutoka Kigoma, basi kuna rafiki yangu yeye alikua na mashetani ya uganga na nilikua nalala naye

Siku moja akaniambia ndg yangu huyu mama jirani yetu ni mchawi nimemuona aliingia humu ndani na Lengo lake nikutuchezea nikachukulia kawaida

Basi yule jamaa aliondokaga nikabaki Mimi na ndg yangu mmoja hasa hapo Yule mama akawa anafanya utawala sasa yaani full kututesa usiku kuna kipindi nikawa namuona kabisa anaingia kupitia mlango na ukiwa umefungwa mida ya usiku lakini nikawa nashikwa na bumbuwazi nashindwa kusema

Siku moja nilipoona mambo yamekua si mambo ikabidi niende Kwa dr mmoja hivi akanipa dawa akaniambia nenda kadeki ndani na utadeki Kwa muda wa siku 3

kweli Kesho yake asubuhi nikafanya hivyo kabla sijaenda kwenye Mishe

Asa nilikuja kushangaa usiku nilipo lala mishale ya saa usiku niliskia sauti ya paka alilia mara3 nachakushangaza alitokea mlangoni na mlango nilikua nimefunga akaelekea uvunguni wa kitanda

Mpaka kuna kucha akawa yupo mle ndani na hali ya pale nyumani ikawa imezorota Fulani yaani mtoto wa Yule mama alikua mpole sana na hata mama yake akawa haonekani ovyo na hata nikikutana naye namuona yupo katka Hali ya unyonge na kisasi cha Hali ya juu

Ila nilimfuata Yule Mganga nakumuelezea akaniambia Yule ni adui alivyoingia mle ndani alikuta bahari hivyo akawa hana jinsi na akaniambia nenda kamalizie kudeki hiyo dawa

Ingawa kuna siku wakati nachanganya ile Dawa ili nideki alikuja Yule mtoto wa Yule mama akainyooshea kidodole ndoo ya dawa , ila hapa usiniulize nilimuona vp majibu nitakayokupa huenda hautaamini......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo miujiza ni mwanga unaotokana na madini yaliyo ardhini
 
Kwa hiyo Babu yako ndio anayekulinda?
Au wewe ndio umerithishwa uwezo wake aliokuwa nao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…