Me ktk maisha yangu nimeshuhudia mambo mengi sana ya kichawi ingawa mengine ni katka ndoto lakini yalikua na uhalisia
Ila tukio ambalo siwezi kusahau ni ktk hizi nyumba za kupanga ambapo nilipanga na mmama mmoja hivi wa kiha kutoka Kigoma, basi kuna rafiki yangu yeye alikua na mashetani ya uganga na nilikua nalala naye
Siku moja akaniambia ndg yangu huyu mama jirani yetu ni mchawi nimemuona aliingia humu ndani na Lengo lake nikutuchezea nikachukulia kawaida
Basi yule jamaa aliondokaga nikabaki Mimi na ndg yangu mmoja hasa hapo Yule mama akawa anafanya utawala sasa yaani full kututesa usiku kuna kipindi nikawa namuona kabisa anaingia kupitia mlango na ukiwa umefungwa mida ya usiku lakini nikawa nashikwa na bumbuwazi nashindwa kusema
Siku moja nilipoona mambo yamekua si mambo ikabidi niende Kwa dr mmoja hivi akanipa dawa akaniambia nenda kadeki ndani na utadeki Kwa muda wa siku 3
kweli Kesho yake asubuhi nikafanya hivyo kabla sijaenda kwenye Mishe
Asa nilikuja kushangaa usiku nilipo lala mishale ya saa usiku niliskia sauti ya paka alilia mara3 nachakushangaza alitokea mlangoni na mlango nilikua nimefunga akaelekea uvunguni wa kitanda
Mpaka kuna kucha akawa yupo mle ndani na hali ya pale nyumani ikawa imezorota Fulani yaani mtoto wa Yule mama alikua mpole sana na hata mama yake akawa haonekani ovyo na hata nikikutana naye namuona yupo katka Hali ya unyonge na kisasi cha Hali ya juu
Ila nilimfuata Yule Mganga nakumuelezea akaniambia Yule ni adui alivyoingia mle ndani alikuta bahari hivyo akawa hana jinsi na akaniambia nenda kamalizie kudeki hiyo dawa
Ingawa kuna siku wakati nachanganya ile Dawa ili nideki alikuja Yule mtoto wa Yule mama akainyooshea kidodole ndoo ya dawa , ila hapa usiniulize nilimuona vp majibu nitakayokupa huenda hautaamini......
Sent using
Jamii Forums mobile app