Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Na anaesema hakuna uchawi jua hayajamkuata
Miee mpaka kupona nlizurura mnooo
Na nikajionea mengi aiseee ya kushangaza
Na kiukweli kupitia tukio hiloo kiasi nliongeza ufaham kuhusu hii dunia tunayoishii
Me kuna mshkaji wangu yeye alikuwa ikifika siku ya mtihani tu anaumwaa hoii... Yani kitu kinaitwa mtihani hapatani nacho... Karudia madarasa mpaka necta wakasema aisee inatosha kufanya mitihani ya taifa sasa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii Kuna nyumba moja hapa mtwara, imeshauzwa mara nane, kila ananunua hakai anapiga mnada,..... Chanzo aliyeuza alikuwa na wake wawili.... Sasa alikuwa na madeni bank, akamuomba mke mkubwa auze nyumba yake, mke mkubwa akakataa akamwambia akauze ya bi mdogo, mume kwa kiburi akauza ya mke mkubwa heheheheheh balaaaa mke mkubwa akaenda kwa mganga Ile nyumba anaenunua akiingia ndani anakuta miti tupu mle ndani yaani poriii[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] mwisho wiki zilizopita imetangazwa kuuzwa tena

Sent using Jamii Forums mobile app
Bei gani babe tuinunue nataka tuishi huko.
 
Nishawahi sikia kisa kinschohusishwa na uchawi

Kuna masela wawili walienda kwa mganga ili wapate utajiri

Mganga akawapa dawa akawaambia wakaoge usiku makaburini na wakitoka mlangoni kwa mganga hawatakiwi kugeuka nyuma

Basi unaambiwa safari yao iliandamwa na misukosuko yakutisha, mara wasikie muunguroma wa simba akiwa nyuma yao na vimbwenga vingi lakini walijitahidi kukaza ili kutovunja sharti la kugeuka nyuma

Sasa ulipofika usiku majira ya saa 8 ikabidi waende makaburini kuoga ili kumalizia zoezi lao la mwisho ili wawe mamilionea

Walipofika makaburini wakavua nguo wote nakubakia uchi kisha wakapanda juu ya kaburi ili waoge

si unajua ukiwa katika ile mood flani hivi unaoga halafu umefumba na macho ili maji yasiingie machoni.

wakastukia tu paap! wameshikwa makalio kwa nyuma.

Aaah unaambiwa wote ilibidi wageuke nyuma kwa haraka huku wanakimbia na kupiga makelele

Kesho yake kijiweni wakaanza kulaumina "aaah wewe ndiye ulizingua, we ungekausha bila kupiga mikelele mi nisingechochora kwani kushikwa tako kitu gani bwana" yani leo nisingekua nakunywa kahawa hapa ningekua nimejikoki huko kwenye hotel zinazotambulika na dunia"
Da mkuu umezingua kinoma yani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2013 nahitimu chuo nikiwa mzima wa afya na michakato yangu ya kuingia jeshini ikawa imepamba moto
Ghafla nikakumbwa na upofu, nikawa sioni, Amana hospital wakasema nenda muhimbili, nakumbuka muhimbili nikakutana na dokta mmoja kuleee clinic ya macho, akanchana live kuwa mie nshakua kipofu mishipa ya macho imesinyaa bora nirudi home tuu
Nikashauriwa na wadau mbalimbali niende CCBRT nako kuchekiwa yale yalee, ila sababu haijulikani
Nakumbuka mfanyakaz mmoja wa hiyo hospital alimstua sister angu jiongezeniii
Basi bhana baada ya kujiongeza kuhangaika huku na hukoo leo naona tena
Hebu tiririka mlivyojiongeza!
 
Mkuu wewe una uwezo wa asili Kama Mimi pia hizo ndoto unitokea mara kwa mara.
Katika kufuatilia nikaambiwa kwamba hao ni mizimu ndio hutoa msaada Kama huo wa kukuonesha wabaya wako na sio akili yako.

Sent using Jamii Forums mobile app
Aisee! Mimi ninachojua niliambiwa babu yangu alikuwa mtu wa dini sana! Alifika tu mkoa fulani, akaoa na akafia hapo. Hawajui ni wapi alipotokea na sijawahi kumuona! Ajabu hata picha hakuwahi kupiga! Baadhi ya ndugu waliyomuona babu akiwa hai wakimuota wanamuona amesimama huku nyuma yake kukiwa na nyumba inang'aa sana.
 
Me ktk maisha yangu nimeshuhudia mambo mengi sana ya kichawi ingawa mengine ni katka ndoto lakini yalikua na uhalisia

Ila tukio ambalo siwezi kusahau ni ktk hizi nyumba za kupanga ambapo nilipanga na mmama mmoja hivi wa kiha kutoka Kigoma, basi kuna rafiki yangu yeye alikua na mashetani ya uganga na nilikua nalala naye

Siku moja akaniambia ndg yangu huyu mama jirani yetu ni mchawi nimemuona aliingia humu ndani na Lengo lake nikutuchezea nikachukulia kawaida

Basi yule jamaa aliondokaga nikabaki Mimi na ndg yangu mmoja hasa hapo Yule mama akawa anafanya utawala sasa yaani full kututesa usiku kuna kipindi nikawa namuona kabisa anaingia kupitia mlango na ukiwa umefungwa mida ya usiku lakini nikawa nashikwa na bumbuwazi nashindwa kusema

Siku moja nilipoona mambo yamekua si mambo ikabidi niende Kwa dr mmoja hivi akanipa dawa akaniambia nenda kadeki ndani na utadeki Kwa muda wa siku 3

kweli Kesho yake asubuhi nikafanya hivyo kabla sijaenda kwenye Mishe

Asa nilikuja kushangaa usiku nilipo lala mishale ya saa usiku niliskia sauti ya paka alilia mara3 nachakushangaza alitokea mlangoni na mlango nilikua nimefunga akaelekea uvunguni wa kitanda

Mpaka kuna kucha akawa yupo mle ndani na hali ya pale nyumani ikawa imezorota Fulani yaani mtoto wa Yule mama alikua mpole sana na hata mama yake akawa haonekani ovyo na hata nikikutana naye namuona yupo katka Hali ya unyonge na kisasi cha Hali ya juu

Ila nilimfuata Yule Mganga nakumuelezea akaniambia Yule ni adui alivyoingia mle ndani alikuta bahari hivyo akawa hana jinsi na akaniambia nenda kamalizie kudeki hiyo dawa

Ingawa kuna siku wakati nachanganya ile Dawa ili nideki alikuja Yule mtoto wa Yule mama akainyooshea kidodole ndoo ya dawa , ila hapa usiniulize nilimuona vp majibu nitakayokupa huenda hautaamini......

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka ya nyuma tunatoka mererani usiku wa manane tuko na pikipiki almaarufu baja tullikutakana na moto mkubwa ukiwa umetanda barabarani kama vile unavuka ,tulikuwa sita tukajishauri sana lakini kwasababu tulikuwa wengi tulipata ujasiri wa kupita ila cha kushangaza tulivuka na hatukuungua wala kuhisi chochote kuangalia nyuma baada ya kuvuka moto uko vile vile
Hiyo miujiza ni mwanga unaotokana na madini yaliyo ardhini
 
Aisee! Mimi ninachojua niliambiwa babu yangu alikuwa mtu wa dini sana! Alifika tu mkoa fulani, akaoa na akafia hapo. Hawajui ni wapi alipotokea na sijawahi kumuona! Ajabu hata picha hakuwahi kupiga! Baadhi ya ndugu waliyomuona babu akiwa hai wakimuota wanamuona amesimama huku nyuma yake kukiwa na nyumba inang'aa sana.
Kwa hiyo Babu yako ndio anayekulinda?
Au wewe ndio umerithishwa uwezo wake aliokuwa nao?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom