Mwaka 1987 alikuja mtu mmoja kutoka Kasulu kwa lengo la kufanya kibarua cha kulima hapo kwenye familia yetu. Hicho kipindi kulikuwa na misiba sana nyumbani pale. Kulikuwa tayari wadogo zangu 5 wameshafariki kwa interval ya mwaka hadi miaka 2,3. Yule jamaa akawa anakwenda kulala kwa shangazi yangu, shangazi alikuwa jirani yetu sana.
Siku moja yule jamaa akamwambia mzee wetu kuwa ameshafikisha mara kadhaa anakutana na shangazi akitoka kuroga hapo nyumbani kwetu akiwa uchi. Mzee wetu alikasirika sana. Mzee alitoweka kwa kutoroka hadi miezi 2 au 3 hivi. Nakumbuka siku ametoroka tulimaliza kuzika mdogo wangu wa kike. Siku ya kurudi alirudi na mganga wa kike, alitoka sehemu moja inaitwa Kanadi huko Bariadi. Nakumbuka siku ya pili yake yule mganga alisema familia nzima wawepo nyumbani na asitoke mtu ikifikia saa 12 jioni
Mimi nikawa nawaza nini kitatokea. Alichukua yai la kuku (alikuja nalo nadhani) akazunguka nalo kwenye mpaka wa eneo la familia kisha akampa kaka yetu (mtoto wa baba mkubwa) akamwelekeza aende akalitupe lile yao kwenye familia ya shangazi na alifanya vile
Mungu wangu, usiku tu kabla ya saa 7 usiku huo. Pale nyumbani walikamatwa mbweha wengi, wale mbweha wanalia kama binadam (wanalia kama wanawake). Yule mganga alielekeza hakuna mtu kutoka. Kesho yake asubuhi, wale mbweha walikuwa wamekufa na wamevutwa wakawekwa kwenye shimo la choo kilichokuwa hakijajengelewa.
Siku chache baadae shangazi akajitokeza kama mwehu hivi akatembea kitongoji kwa kitongoji akisema yote ambayo huwa anayafanya, washirika wake wote humo mtaani, alisema pia mipango yake yote ambayo anatarajia kuyafanya.
Siku chache pia washirika wote wale nao wakaanza kufanya kama alivofanya mwenzao. Hakika, wale wote walikufa wakiwa wehu na kaburi zao huwa zinaota vichuguu hadi leo licha ya kujengelewa kokoto, huwa zinapasuka na kuota vichuguu vikubwa
Nilishaogopa sana, Nilishaogopa waganga na wachawi tangu hicho kipindi. Nilisha kataa habari zote za waganga maana nao ni wale wale tu.