Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kuna jamaa angu alifumaniwa na mke wake,ugomvi ulikua mkubwa kiasi ya kwamba mwanamke alishaanza kufungasha mizigo yake aondoke,jamaa alichofanya alimpgia mtalaam wake simu aisee,baada ya masaa 5 mwanamke amesahau kila kitu,hali ikawa shwari


Sent from my iPhone using JamiiForums
Mkuu uchawi ktk mapenzi nakubali asilimia zote


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 1987 alikuja mtu mmoja kutoka Kasulu kwa lengo la kufanya kibarua cha kulima hapo kwenye familia yetu. Hicho kipindi kulikuwa na misiba sana nyumbani pale. Kulikuwa tayari wadogo zangu 5 wameshafariki kwa interval ya mwaka hadi miaka 2,3. Yule jamaa akawa anakwenda kulala kwa shangazi yangu, shangazi alikuwa jirani yetu sana.

Siku moja yule jamaa akamwambia mzee wetu kuwa ameshafikisha mara kadhaa anakutana na shangazi akitoka kuroga hapo nyumbani kwetu akiwa uchi. Mzee wetu alikasirika sana. Mzee alitoweka kwa kutoroka hadi miezi 2 au 3 hivi. Nakumbuka siku ametoroka tulimaliza kuzika mdogo wangu wa kike. Siku ya kurudi alirudi na mganga wa kike, alitoka sehemu moja inaitwa Kanadi huko Bariadi. Nakumbuka siku ya pili yake yule mganga alisema familia nzima wawepo nyumbani na asitoke mtu ikifikia saa 12 jioni

Mimi nikawa nawaza nini kitatokea. Alichukua yai la kuku (alikuja nalo nadhani) akazunguka nalo kwenye mpaka wa eneo la familia kisha akampa kaka yetu (mtoto wa baba mkubwa) akamwelekeza aende akalitupe lile yao kwenye familia ya shangazi na alifanya vile

Mungu wangu, usiku tu kabla ya saa 7 usiku huo. Pale nyumbani walikamatwa mbweha wengi, wale mbweha wanalia kama binadam (wanalia kama wanawake). Yule mganga alielekeza hakuna mtu kutoka. Kesho yake asubuhi, wale mbweha walikuwa wamekufa na wamevutwa wakawekwa kwenye shimo la choo kilichokuwa hakijajengelewa.

Siku chache baadae shangazi akajitokeza kama mwehu hivi akatembea kitongoji kwa kitongoji akisema yote ambayo huwa anayafanya, washirika wake wote humo mtaani, alisema pia mipango yake yote ambayo anatarajia kuyafanya.

Siku chache pia washirika wote wale nao wakaanza kufanya kama alivofanya mwenzao. Hakika, wale wote walikufa wakiwa wehu na kaburi zao huwa zinaota vichuguu hadi leo licha ya kujengelewa kokoto, huwa zinapasuka na kuota vichuguu vikubwa

Nilishaogopa sana, Nilishaogopa waganga na wachawi tangu hicho kipindi. Nilisha kataa habari zote za waganga maana nao ni wale wale tu.
 
Salange, Hii,nishawahi kusikia watu wanaazima meno yako na kwenda kutafunia nyama huko na baadaye unarejeshewa, sometimes naskia unaweza rudishiwa yakiwa hayajasafishwa vizuri,ukiamka asubuhi meno yana damu damu + nyama nyama ,wakati usiku huo ulikula maharage[emoji3][emoji3] sayansi zipo hizi jamani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa una maswali. Kwan wewe hiyo sayansi ulithibitishaje?
Sasa wewe unanijibu swali kwa swali halafu hapo hapo unanisema nina maswali?

Sayansi imethibitishwa kwa mantiki isiyokanushika katika majaribio yanayoweza kurudiwa na wengine kwa uthibitisho zaidi.

Wewe uchawi unauthibitishaje huu ni uchawi na si kitu kingine usichokijua?
 
Niliwahi kuishi kwenye nyumba X, nikiwa mimi, mwanangu na mama mdogo na ndugu yangu mwingine. Ile nyumba sijui nieleze vipi lakini kitendo cha kusikia mtu amegonga hodii au kugonga mlango na mkitoka hakuna mtu kilikuwa cha kawaida kabisa. Unakuta mko sebuleni wote mnapiga stori au kuangalia Tv, mnasikia hodiiii, akitoka mtu kuangalia hakuna mtu. Na hausemi labda mtu amegonga ameondoka maana unakuta interval ya muda wa kugonga mlango au kubisha hodi na kwenda kufungua mlango ni sekunde tu.

nyumba ilikuwa ina vyumba viwili juu, unashuka ngazi unakuta na sebule na chumba kingine ambacho mimi ndo nilikuwa nalala. Usiku mara nyingi unasikia mtu anashuka ngazi nko, nko, nko.

Kuna kipindi ndugu zangu hao wakarudi makwao nikabaki mi na mwanangu nikaona isiwe tabu nikatafuta nyumba nyingine nikatoka ndukiiiiiii!
 
Back
Top Bottom