Nia visa viwili vitatu.
Cha Kwanza:
Mwaka 2004 tukiwa Dodoma Wilaya ya Kondoa Kijiji kinaitwa Mondo.
Kuna Jamaa tulikuwa tunapiga nao mishe hapo bush halafu Washikaji walikuwa Wazee wa Totozi na tunaishi chumba kimoja ambacho tulipewa na mwenyeji wetu.
Mmoja Kati ya Wenzangu alimlamba Mke wa Mzee Mmoja pale bush wakati sisi Wengine tumeenda Kondoa Mjini.
Usiku wake Sasa ilikuwa ni balaa.... tuling'atwa na SIAFU kiasi ambacho ilibidi tutoe Godoro na Nguo zote hadi tulizovaa Nje.
Tukaenda kuchukua Mashuka kwenye mabegi na kulala kwenye Chaga za Kitanda lakini siafu wapo palepale.
Tukachukua magazeti na kuwachoma Moto lakini ile tunarudi kulala shughuli ipo palepale.
Kiukweli hatukulala kabisa hadi Asubuhi na kadhia ilikuwa Chumbani kwetu tu.
Ilipofika Asubuhi hatukuona hata Siafu aliyekufa wala Mzima licha ya kupekua huku na kule.
Jamaa yetu aliyefanya Kosa baada ya kutishwa ikabidi amuombe Mwenyeji wetu akatuombee Msamaha, hapo hali ikawa Shwari.
Kwa lile tukio nilisema SHIKAMO.. WARANGI.
Sent using
Jamii Forums mobile app