Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nia visa viwili vitatu.

Cha Kwanza:
Mwaka 2004 tukiwa Dodoma Wilaya ya Kondoa Kijiji kinaitwa Mondo.

Kuna Jamaa tulikuwa tunapiga nao mishe hapo bush halafu Washikaji walikuwa Wazee wa Totozi na tunaishi chumba kimoja ambacho tulipewa na mwenyeji wetu.

Mmoja Kati ya Wenzangu alimlamba Mke wa Mzee Mmoja pale bush wakati sisi Wengine tumeenda Kondoa Mjini.

Usiku wake Sasa ilikuwa ni balaa.... tuling'atwa na SIAFU kiasi ambacho ilibidi tutoe Godoro na Nguo zote hadi tulizovaa Nje.

Tukaenda kuchukua Mashuka kwenye mabegi na kulala kwenye Chaga za Kitanda lakini siafu wapo palepale.

Tukachukua magazeti na kuwachoma Moto lakini ile tunarudi kulala shughuli ipo palepale.

Kiukweli hatukulala kabisa hadi Asubuhi na kadhia ilikuwa Chumbani kwetu tu.

Ilipofika Asubuhi hatukuona hata Siafu aliyekufa wala Mzima licha ya kupekua huku na kule.

Jamaa yetu aliyefanya Kosa baada ya kutishwa ikabidi amuombe Mwenyeji wetu akatuombee Msamaha, hapo hali ikawa Shwari.

Kwa lile tukio nilisema SHIKAMO.. WARANGI.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tunataka ushahidi wa wachawi wenyewe pamoja na waganga waje hapa na wao
 
Sasa wewe unanijibu swali kwa swali halafu hapo hapo unanisema nina maswali?

Sayansi imethibitishwa kwa mantiki isiyokanushika katika majaribio yanayoweza kurudiwa na wengine kwa uthibitisho zaidi.

Wewe uchawi unauthibitishaje huu ni uchawi na si kitu kingine usichokijua?
Nini tofauti kati ya sayansi na uchawi (najua hapa huna jibu kwakuwa unajidai huamini kuwa kuna uchawi)
 
Mwanzoni mwa miaka ya 2001 nikiwa wilaya x mkoa wa Shinyanga kwa wasukuma..kama kawaida ya wasukuma vijana huwa wana umoja wa kusaidiana hasa hasa shughuli za kilimo na kwa njia ya mzunguko yaani kila mtu lazima asaidiwe wakati wake ukifika. Na anayesaidiwa hiyo siku ana jukumu la kuwalisha vijana wote kuanzia asubuhi mpaka jioni.

Basi Kuna familia moja ambayo ilikuwa inasadikika kuwa ni ya kichawi hiyo siku ndo ilikuwa zamu kupewa msaada wa kilimo na hicho kikundi cha vijana.. Ndani ya kikundi hicho cha vijana kulikuwa na kijana Mmoja aliyekuwa na nguvu nyingi sana kwenye shughuli za kilimo maana alikuwa analima bustani za kutosha na kupata hela za kutosha.. Kumbe wachawi walikuwa wanamtafuta siku nyingi.

Hiyo siku ya kazi ya kusaidia kwa hiyo familia ya kichawi zilipikwa nyama nyingi sana.. Watu walikula na kusaza.. Baada ya kumaliza shughu zote pamoja na kula watu walisambaa.. Baady kidogo Kama siku mbili kupita yule jamaa akaanza kuumwa sana.. Ikawa anadhoofika huku ugonjwa ukiambatana na kutapika chakula alichokula hiyo siku ya kazi.. Alikuwa anatapika zile nyama. Hali iliendelea kwa muda Mrefu mpaka akaja kufariki mwaka 2010 ..aliteseka sana kwa karibia miaka kumi.

Uchawi upo ndugu zangu cha msingi ni kumwamini mungu tuu.. Maana watu husema ukianza kwenda kwa waganga unawarahisishia kazi wachawi kukumaliza maana mnakuwa mnashindana kwa makombora.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unaweza kujaribu trick mojawapo?
Sijapata muda mchafu wa kujifunza sanaa ya chini ya aina hiyo.

Ila najua there is such a thing as a sleight of hand.

What, are you disputing that there is such a thing as a sleight if hand and psychological manipulation that passes itself as witchcraft?

Unafikiri karata tatu ni uchawi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu Kiranga namshangaa sana,kina visa vingi vya watu kufa na baadae kuonekana tena na wakienda kufukua pale wapozikwa hawakuti chochote,hili nalo unalizungumziaje?
Unazungumziaje mtu anayeota usiku analima shamba na asubuhi akiamka anakuwa na matope na uchovu mwilini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom