Naomba na Mimi niandike hiki kisa
Wakati nikiwa form three mkoa wa Mwanza, waliokua mbele yetu kidato cha nne walikua wakifanya mtihani wa taifa sasa kuna mwenzao mmoja hakutokea asubui ya siku ya mtihani na wakati alipanga kabisa dawati na namba yake alibandika mwenyewe.
Siku ya Kwanza yaani jumatatu hakuonekana, siku ya pili pia hakuonekana, alikuja kuonekana siku ya tatu yaani jumatano na alikutwa barabarani akiwa amelala hajitambui, akawa amekosa mtihani hivyo ikabidi arudishwe nyuma yaani afanye mtihani mwaka ujao na Sisi kidato cha tatu pindi tutakapokua kidato cha nne.
Basi mwaka wetu uliofatia ukafika na kipindi cha mtihani kikafika pia, kama kawaida tukapanga madawati na namba siku ya ijumaa, tukaondoka sasa huyo mwenzetu alierudia darasa akaenda kwa dada yake ili jumatatu aamke mapema awahi shuleni maana kwa dada yake kulikua karibu na shule ukilinganisha na kwao alipokua akiishi.
Kama kawaida ikafika siku ya mtihani yaani jumatatu, mwenzetu kumuangalia sehemu yake hakuonekana mpaka tunaanza mtihani na tunamaliza siku ya kwanza hakuonekana,
Jumanne asubui tukapata taarifa kutoka kwa mwanakijiji kuwa amemuona mwanafunzi alievaa nguo kama za kwetu (Sare ya shule) amelala karibu na mto na amejaa matope maana karibu na shule kuna mto unapita, basi ikabidi baadhi ya wanafunzi na waalimu waende kumchukua walimkuta hajitambui wakamleta mpaka shuleni akapatiwa huduma ya Kwanza na kusafishwa matope ndio akaanza kujitambua
Baada ya kupata ahueni akaanza kusimulia, muda huo tumetoka kwenye mtihani wa tatu na unavyojua huwa kuna gape kubwa la muda Kati ya mtihani mmoja na mwingine so akawa anasimulia kuwa alitoka kwa dada yake saa 12 asubui akapita njia ya mkato ambapo huo mto unapita, then alipofika mtoni akakutana na paka mmoja mweusi amesimama njiani alipotaka kumfukuza ili apite ndio hakuekewa ikawaje mpaka alipokuja kubebwa siku ya jumanne
So kuanzia hapo niliamini bwana haya mambo yapo maana kitu kumtokea mtu mara mbili mfululizo hiyo sio coincidence bali kuna kisababishi behind
Sent using
Jamii Forums mobile app