Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nakumbuka kipindi hicho nikiwa na umri wa miaka 6. Usiku wa saa saba, mkojo ukanibana sawa sawa, ikabidi nimwamshe Mamdogo anitoe nje ili nitoe hiyo haja ndogo

Kwasababu Mamdogo alikuwa na usingizi kwa kutosha, ikabidi anipige biti la hatari na kufoka sana. Tukatoka, yeye akasimama mlangoni mie nikasogea kama mita nne hivi ili nijisaidie. Zile kelele za mother kufoka usiku akiwa mlangoni, tulisikia sauti ya kike kutoka nyuma ya jiko ikisema "MUACHE AKOJOE NAWEWE". Hahahahah!!! Sikutambua Mamdogo kaingia ndani sangapi maana kugeuka nyuma sioni mtu mlangoni. Kwakuwa nilikuwa mdogo niliendelea na haja yangu then nikarudi ndani......
Ulikuwa jasiri sana kijana
 
Mkuu na baada ya kuwaona kitaendelea ni siku zinazifuata?
Je wale wachawi hawatogundua kuwa umewaona?Na endapo watagundua kuwa umewaona nini kitatokea baadae?

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hapa anauliza swali au jibu? Yani ni sawa na kuuliza hivi " je ikitokea ninaishi na mgonjwa wa homa ya dengue, halafu akaja mbu wa dengue akamuuma yule mgonjwa, halafu akabeba vimelea akaja akaniuma na mimi, je nini kitatokea?"
 
Mkuu hapa anauliza swali au jibu? Yani ni sawa na kuuliza hivi " je ikitokea ninaishi na mgonjwa wa homa ya dengue, halafu akaja mbu wa dengue akamuuma yule mgonjwa, halafu akabeba vimelea akaja akaniuma na mimi, je nini kitatokea?"
Umejitahidi kujibu kwa mantiki ila jibu lako bado halitoshelezi.
Nilitaka jibu la kitaalamu zaidi kwa mtu mwenye uzoefu zaidi na hilo Jambo.
Yaani endapo ikitokea hivyo hatua zipi unatakiwa uzifuate ili kuzuia madhara yatakayojitokeza?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna ulijualo kuhusu elimu,unakimbilia kupinga badala ya kuuliza,nano a like a lb a ukiwa mwalimu huruhusiwi kusoma tena? Au unajua ualimu na walimu upon kwa viwango vingapi vya elimu?
Wewe ni muongo.

Umesema mwaka 92 ulikuwa umeshaanza kazi ya kufundisha halafu unasema tena mwaka 2009 ulikuwa unasomea ualimu, aisee hii chai yako imezidi tangawizi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Miaka kadhaa imepita, nilikuwa naaishinmbezi beach iyo siku nilikuwa nnaumwa nimekunywa dawa, ila ilibidi nikakutane na washkaji zangu samaki samaki, sikugusa pombe kabisa mida kama ya saa 7- 8, nikaondoka nimefika maeneo ya makongo nikamuona binti mwanafunzi, amevaa uniform anatembea kwa kuchechemea sana, huku mguu mmoja hauna kiatu wala soksi, nikafikiria kumsaidia nafdi ikaniambia acha, yani nilivyompita tuu nnachungilia simuoni kwenye vioo

Next time makongo hapo hapo saa kumi usiku ninarudi home tukakutana na mbibi na kijana wamevaa manguo meupe na kujipaka vitu vyeupe ila walikuwa wanatembea kwenye lane tofauti na tuliyokuwa na katika gari tulikuwa wanne na watatu wote tuliwaona, nikamwambia jamaa alikuwa anaemdesha wakiingia lane yetu usiwakwepe fumua
Hii kitu Zanzibar ipo! Hata kwenye baadhi za hotel Zanzibar mauza uza yapo.
 
Miaka ya nyuma tunatoka mererani usiku wa manane tuko na pikipiki almaarufu baja tullikutakana na moto mkubwa ukiwa umetanda barabarani kama vile unavuka ,tulikuwa sita tukajishauri sana lakini kwasababu tulikuwa wengi tulipata ujasiri wa kupita ila cha kushangaza tulivuka na hatukuungua wala kuhisi chochote kuangalia nyuma baada ya kuvuka moto uko vile vile
Wazee walikuwa kwenye kikao chao cha kahawa aisee hatari sana
 
Mzee Njemba Njemba namfahamu aliwahi kuleta maiti pale lake tanganyika mechi ya Yanga , kipindi hicho kigoma KUna Mbanga FC ilikuwa inacheza ligi kuu.....


Nimeshuhudia mambo na kusikia mambo Yake mengi ... Ujiji ni hatari usijifanye mjuaji kule.

Sent using Jamii Forums mobile app
chai hii bila sukari
 
Naomba na Mimi niandike hiki kisa

Wakati nikiwa form three mkoa wa Mwanza, waliokua mbele yetu kidato cha nne walikua wakifanya mtihani wa taifa sasa kuna mwenzao mmoja hakutokea asubui ya siku ya mtihani na wakati alipanga kabisa dawati na namba yake alibandika mwenyewe.

Siku ya Kwanza yaani jumatatu hakuonekana, siku ya pili pia hakuonekana, alikuja kuonekana siku ya tatu yaani jumatano na alikutwa barabarani akiwa amelala hajitambui, akawa amekosa mtihani hivyo ikabidi arudishwe nyuma yaani afanye mtihani mwaka ujao na Sisi kidato cha tatu pindi tutakapokua kidato cha nne.

Basi mwaka wetu uliofatia ukafika na kipindi cha mtihani kikafika pia, kama kawaida tukapanga madawati na namba siku ya ijumaa, tukaondoka sasa huyo mwenzetu alierudia darasa akaenda kwa dada yake ili jumatatu aamke mapema awahi shuleni maana kwa dada yake kulikua karibu na shule ukilinganisha na kwao alipokua akiishi.

Kama kawaida ikafika siku ya mtihani yaani jumatatu, mwenzetu kumuangalia sehemu yake hakuonekana mpaka tunaanza mtihani na tunamaliza siku ya kwanza hakuonekana,

Jumanne asubui tukapata taarifa kutoka kwa mwanakijiji kuwa amemuona mwanafunzi alievaa nguo kama za kwetu (Sare ya shule) amelala karibu na mto na amejaa matope maana karibu na shule kuna mto unapita, basi ikabidi baadhi ya wanafunzi na waalimu waende kumchukua walimkuta hajitambui wakamleta mpaka shuleni akapatiwa huduma ya Kwanza na kusafishwa matope ndio akaanza kujitambua

Baada ya kupata ahueni akaanza kusimulia, muda huo tumetoka kwenye mtihani wa tatu na unavyojua huwa kuna gape kubwa la muda Kati ya mtihani mmoja na mwingine so akawa anasimulia kuwa alitoka kwa dada yake saa 12 asubui akapita njia ya mkato ambapo huo mto unapita, then alipofika mtoni akakutana na paka mmoja mweusi amesimama njiani alipotaka kumfukuza ili apite ndio hakuekewa ikawaje mpaka alipokuja kubebwa siku ya jumanne

So kuanzia hapo niliamini bwana haya mambo yapo maana kitu kumtokea mtu mara mbili mfululizo hiyo sio coincidence bali kuna kisababishi behind

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi stori za humu baadhi ni chai ya rangi


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Nyingine hii nilisimuliwa na Mzee wangu

Alikua akifundisha shule Fulani huko mbeya wilaya ya kyela, sasa wakati wa mtihani wa darasa la saba kuna nyuki mmoja aliingia darasani akawa anzunguka juu ya kichwa cha mwanafunzi mmoja aliekua anajiweza kimasomo huyo mwanafunzi akaanza kuhisi kichwa kumuuma akamwambia msimamizi,

kipindi hicho Mzee wangu ndio mkuu wa shule, so msimamizi akatoa taarifa kwa mkuu wa shule ambae ni Mzee wangu, sasa kwa vile mzee wangu alikua amefanya kazi Hilo eneo kwa muda mrefu so alijua tu hapa kuna kitu kinachezwa , akaenda kwa Mzee mmoja kijijini hapo si mbali na shule akamwambia situation Yule mzee akampa Mzee wangu dawa aende akaiweke kwenye dawati la Yule mwanafunzi

Baada ya kuiweka Ile dawa Yule nyuki hakurudi tena na Yule mwanafunzi kichwa kikaacha kuuma hapo hapo, akafanya mtihani wake vizuri,

baada ya mtihani Mzee akaelekea kwenye klabu cha kijiji akakutana na Yule mzee aliempa dawa, Yule mzee akamuuliza maendeleo ya mwanafunzi yakoje Yule aliekuja kumchukulia dawa ,

Mzee akamwambia alifanya mtihani vizuri bila shida, Yule mzee ndio akamwambia kuwa huo ulikua ni mchezo anachezewa na mwanafunzi mwenzie yaani Yule nyuki alikua anampoteza maboya Yule dogo asifanye mtihani vizuri ndio maana akaanza kuhisi kuumwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom