Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]unaweza kuzimia hv hv kudadeeki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sikuwahi shuhudia live uchawi ila niliwahi shuhudia matukio mengi ya kichawi...

Miaka 2007 hadi 9 niliinshi nyumba moja magomeni mikumi karibu na bondeni kule kwa mzee mmoja wanamuita Fungo,

Nikiamka usiku wa manane naenda kukojoa naskia ngoma inachezwa sebuleni kwao waliishi nyumba kubwa mimi chumba cha nje na hiyo ilikua mara nyingi sana kuskia hata ikitokea nikishtuka usingizini naskia wakiimba, kupiga ngoma na kucheza.

Siku nkapanga safari kwenda kusalimia kijijini ikabidi nikubaliane na mzee alale chumbani kwangu maana kulikua na wezi sana miaka hiyo,

Baada ya wiki kurudi nkakuta kapeti limechanwa chanwa sanaaaaa na ni maeneo yale yanayokanyagwa tu, na vipande vimejazana huko chini kibao,
Hata sikuuliza kwa mazingira niliyoyaona nkajua tu ngoma ilihamia gheto kwangu na watakua wanavaa viatu vyenye ncha kali ndio maana wakalichana vile..

Lakini cha ajabu matukio yote hayo sikuwahi kua na hofu hata chembe hata sijui kwanini...

Kuna nyumba tulipanga maeneo ya sinza mapambano, mara nyingi tu mke wangu huona watu wako uchi aidha nje wakichungilia dirishani na wengine wapo chumbani kwetu, na hapo yule macho live, lakini hata anaponiadidhia wala sipati hofu yoyote, hua naona kawaida tu, sijui ni kwanini.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Kweli duniani watu wana roho mbaya sana! Unamnyang’anya mtu miguu yake yote ati kwa vile amefukuza kuku wako shambani kwake? Huyo jamaa mwenye kuku ni “mshamba” sana
 
Muda si mrefu nitakuwa na afro kama avatar yako.
 
Gamboshi ipo kweli usukuman huko ila hizo story zake za kichawi zimetiwa chumvi. Nimesoma na jamaa mmoja mpwapw secondary form four 2004, Emmanuel Holehole alikua katokea Gamboshi. Alinambia Gamboshi kwa kawaida tu hakuna lolote Kama wanavyosema.
Gamboshi Ni ukweli au simulizi za kusadkika mkuu?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Watu wanaendelea kuweweseka na kushika watu uchawi badala ya kutunga sera mbadala...
 
Jirani yangu kuna siku alikuwa ananisimulia alikuwa anasafiri na broo wake usiku walikuwa kwenye gari yao. Safari ilivyokuwa inachanganya mbele wakamuona mtu kwa mbali kama anasimamisha gari. Kumuangalia vizuri kumbe ni mwanamke, halafu ni mrembo tu! Dogo akamwambia bro huyu mwanamke atakuwa jini tu haiwezekani usiku huu wote asimame njiani peke yake, tumpite tu.

Brother yake akamwambia usihofu. Akasimamisha gari. Akamwambie ndio mrembo! Yule mwanamke akamwambia naombeni lift nimekwama huu usiku naelekea eneo fulani. Brother yake akamwambia yule mwanamke ingia. Safari inachanja mbuga brother yake akaanza kumwambia yule mwanamke. Inakuaje unatusumbua unasimamisha gari wakati eneo unalotaka kwenda unaouwezo wa kufika?

Yule mwanamke akajibu sielewi unachozungumza. Brother yake akamwambia yule mwanamke, usi' panic! Sisi tuliokupa lift tunajua kwamba wewe ni jini! Ndiyo tunakuuliza kwa nini umetusumbua kusimamisha gari wakati kufika eneo unalotaka uwezo huo unao wewe kama wewe?

Yule mwanamke akawaambia simamisheni gari! Majamaa wakasimamisha. Wakasikia mlango wa siti ya nyuma unafunguliwa. Kugeuka yule mwanamke hawamuoni tena! Brother yake akasema, unatusumbua wakati uwezo wa kufika unao. Wakaendelea na safari.

Nikamuuliza sa mbona huyo jini katumia style ya zamani sana? Jamaa akanijibu, majini ni wapumbavu wapumbavu tu.
 
[emoji2]jini kaleta uduwanzi akakutana na binadamu mduwanzi vilevile!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kiboko ya wote nendeni GAMBOSH simiyu.ni kakijiji kadogo lakini ikifika usiku taa za umeme magari utafikiri upo dubai panawaka panachangamka ikifika asubuhi utashangaa nyumba moja moja za majani

Sent using Jamii Forums mobile app
Huko ndio kuliko wapatia idea Marvel wakatengeneza black panther.
Gambosh=Wakanda. [just saying]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu Uzi unatembea fasta utazidi ule wa Wala epo kimasihara

Binadamu wanakuwa ‘fascinated’ na ‘mystery’ au miujiza. Suala ambalo akili ya kawaida ya binadamu inashindwa kupata jibu lake humfanya apate dukuduku la kupata ufumbuzi wake. Kwa sababu hiyo mjadala huu utakuwa mrefu sana. Tunaomba wadau waendelee kutuletea vimbwanga zaidi vya ukweli. Ingawa inawezekana wengine wataleta ‘fix’ tu za kusimuliwa ambazo hazijathibitishwa.
 
 
Kweli duniani watu wana roho mbaya sana! Unamnyang’anya mtu miguu yake yote ati kwa vile amefukuza kuku wako shambani kwake? Huyo jamaa mwenye kuku ni “mshamba” sana
Ndo tabia za wachawi, wachawi hawapati faida yoyote wao wanataka kuona mtu anateseka tu ndo furaha yao. Hicho kisa ni cha kweli na kimetokea Ludewa mkoa wa Njombe ukiweza ulizia wenyeji wa huko watakuambia na jamaa amekuwa tegemezi wa kupewa misaada tu, miaka ya nyuma 2000's hiki kisa kiliandikwa kwenye gazeti fulani, it's a true story.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…