Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Aise mnaujasili sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siku moja zamani sana tuliharibikiwa na bus maeneo fluni panaitwa makuyuni Arusha tukiwa tunatoka Dodoma tunaelekea Moshi kwa Bus enzi hizo ni mabus yalikuwa ni ya kampuni ya Rali hakuna mabasi mengine.

Kipindi hicho barabara ni mbovu sana gari inachukuwa siku mbili kufika Moshi.

Ikabidi konda na abiria mmoja wafuate spear Dodoma nayo ilichuwa siku mbili.

Ilibidi wazazi waniojiongeze tutafute nyumba za jirani ili angalau tupate huduma kama chakula, kuoga na kadhalika wazee na familia zingine walifanya hivyo pia.

Kutoka hapo kwenye bus mpaka kwenye nyumba ni umbali wa kama kilometa tano hivi tukakuta nyumba mbili tu lakini tunashukuru nyumba tuliofika tukawaeleza shida zetu walituelewa ambapo walikuwa wanaishi watu wawili tu kijana mmoja na mke wake ambaye alikuwa mrembo kweli wengi tulishangaa kwanini waliamua kuishi porini ili hali kwa muonekano walikuwa ni watu wastaarabu sana.

Basi baada ya wazazi wetu kupokelewa wakaanza mandalizi ya kupika na mambo mengine sisi watoto mimi na mdogo wangu na watoto wawili wa familia moja tulienda kucheza eneo fulani kama shamba hivi lakini kulikuwa na mteremko unaelekea kwenye mto hivi pembeni ya ya huo mto kulikuwa na ndizi mbivu basi tukazikimbilia tukazichuma tukaanza kula.

Kwakuwa ule mto haukuwa na maji tukavuka upande wapili hapo tuliona matunda ambayo siyakumbuki ni matunda gani lakini yalikuwa matamu sana.

Baadaye tukaona kijumba kidogo cha udongo kimeezekwa kwa nyasi tukaenda mpaka kwenye hicho kijumba tukamkuta bibi mzee sana anachuma mboga karibu na nyumba yake tukasalimia tukamweleza sikumbuki nini lakini akatuletea mziwa tukanywa.

Mara kukawa na wingu zito sana na radi baada ya dakika kumi mvua ilinyesha kunyesha tukaanza kukimbia nilibidi nimemshika mdogo wangu mkono alikuwa analia sana na mdogo wake na yule mwenzetu naye alikuwa analia sana, basi yule bibi alituzuia tusiondoke mpaka mvua itakatike ila mimi na na mdogo wangu tuliondoka na kuwaacha wenzetu tukaelekea mtoni ili tuvuke ngambo ya pili tuondoke ajabu ngambo ya pili tulimuona yule Bibi na fimbo yake amekunja uso anaonyesha ishara ya tukivuka tutaipata daa tulitetemeka sana huku dogo analia vibaya sana bibi anatunyooshea ile fimbo turudi.

Nyuma ya yule bibi tukaona kwa mbali mwanga wa tochi na sauti za watu kama wanaongea ndiyo kumbe mzee wanatutafuta.

Yule bibi kuona watu wanakuja akaja upande wetu huku akivuka mto huku anatembea kwa kuinama na fimbo yake tukampisha tukanza kumuita mzee huku tunatetemeka na dogo analia tumeloa chakari mzee alivyotuona walipatatwa na hofu sana wakatuuliza yaliotokea tukawaambia wenzetu wapo kwa bibi mmoja kule juu mwenyeji wetu na wazee waliwafuata kwa yule bibi huku mwenyeji akisema huyu bibi ni mchawi sana asije wazuru watoto wakakimbia kufika pale wakawakuta wapo ndani kwa yule bibi wanaota moto lakini wamejikunyata wamelegea sana hawajiwezi huku huyo bibi akiwa amejilaza kwenye kitanda chake anatamka sijui maneno gani.

Yule mwenyeji nasikia akamkoromea sana huyo bibi akamwambia lolote litakalo walata hawa watoto tunakumaliza ndiyo ikiwa salama yao.

Kufika pale kwa mwenyeji wetu hapo ni usiku kama saa 2:30 kunagiza tunawahadithia kilichotokea mh..wazazi waliogopa sana tukagombezwa sana lakini tunashukuru mpaka leo tupo salama ingawa mwenzetu mmoja alishatangulia kufa .

Hayo ndiyo nakumbula lakini ilikuwa siku mbaya sana na sitaisahau maishani.
 
Miaka ya 1995 - 2000 kuna bwana mmoja alienda kwa mganga mahali fulani wilaya ya Njombe ili apate utajiri.

Masharti aliyopewa pamoja na dawa ni kulala katikati ya reli ya TAZARA usiku. Kwamba akisikia treni inakuja asiondoke aendelee kunuiza anataka utajiri wa kiwango gani.

E bwana ee, jamaa alisikia chuma kinaunguruma kama kilometa 5 kuja uelekeo wake. Sasa shida ikawa upande mmoja sijui ni moyo au ubongo au vyote vikaanza mjadala. Hiki ni kifo hapana huu ni utajiri.

Kukatisha maelezo jamaa aliyoka mbio baada ya kuinua kichwa na kuona kichwa cha treni kinasonga bila mjadala.

Aliamua kurudi kwao kijijini kukomaa na mpini wa jembe.

Hii ni simulizi kutoka kwa mhusika katika mazungumzo ya utajiri wa haraka haraka.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2014 maeneo ya Boko, mimi na dada zangu watatu tunatoka zetu viwanja saa tisa usiku kwa mbele hivi tunaona mtu kalala katikati ya barabara mmh dada aliyekua anaendesha akasita alitaka asimame, dada mwingine akamwambia kwa sauti kubwa "pita juu yake bila hivyo wote unatuua", basi akapita juu na wote ndani ya gari tulihisi kabisa matairi yamekanyaga mtu, tulivyopita mbele kidogo tukageuka kuangalia huyo mtu vipi ajabu hatukuona kitu yaan road nyeupeee, basi story zilikata hakuna mtu aliongea hadi tunafika home.
 
Kaka yangu alisimulia akiwa na crew yake wametoka zao kuwinda ghafla gari ikagoma, wakaicheki kila kitu ipo fresh lakini haiwaki, wakashauriana walale kwenye gari kesho wataikagua vizuri, basi usingizini waliota kama wapo shamba wanalima, kuamka asubuhi wakashangaa miguu imejaa tope jekundu yaan wamechafuka mno gari inanuka vitunguu na ina maganda ya vitunguu kujikagua vizuri wakakuta vitunguu vinne na wao walikua wanne.

Moro hiyooo mwaka 2016.
 
Eti wachawi wa mvua hawapo? Ngoja nikupe msala huu hapa.

Mwaka 1986 nilikuwa kitoto cha darasa la 4, kipindi hicho huko usukumani ndio jeshi la Sungusung ndio liko moto. Kulikuwepo wazee wawili mmoja alikuwa anaitwa Radslaus (walizowea kumwita Silaus) mwingine alikuwa anaitwa Ndonkeye. Hawa wazee wao walikuwa hawapendani, kisa kumbe ilikuwa jinsi walivyokuwa wanazidiana ujuzi wa kuloga.

Hawa wazee vikitokea vipindi mvua ikakosekana katikati ya msimu wa mvua walikuwa wanatamba kwamba wapewe fedha au vyakula ili walete mvua. Mwisho wao ulikuwa mbaya sana.

Siku moja nzengo ikapiga mwano (mbiu) na watu wakakusanyika. Ndonkeye na Silaus wakaletwa. Nakumbuka ilikuwa mida ya saa 9 alasiri hivi. Wakaulizwa mbona mvua hainyeshi. Silaus akasema yeye huwa anajitahidi kuileta ila Ndonkeye huwa analeta upepo mkali mawingu yanapeperushwa.

Ndonkeye naye akaulizwa, yeye akasema ni mtaalam wa kuleta mvua kumzidi hata Silaus. Nzengo ikaona hawa wanawachezea akili. Nzengo ikatengeneza duara kama ya watu 30, wakaambiwa wapite wakiizunguka hiyo round ya watu walio na viboko ili wapigwe, wakapita na kila mtu akatandika kiboko kimoja mgongoni, kisha mzunguko wakaumaliza, yakaandaliwa maji kwenye ndoo yaliyotiwa chunvi, wakamwagiwa, kisha wakapita tena kwenye roundi kutandikwa

Baada ya hapo, Ndonkeye akaamua kusema ukweli kuwa yeye ndie mtaalam wa kuleta mvua na kama hawaamini alete wakati huo huo. Nzengo ikafurahi sana. Akaomba aende atafte dawa polini, nzengo ikampa watu wachache ili wamsindikize na arudi nao akiwa na dawa hiyo. Wakaondoka, walipofika huko polini Ndonkeye akawaambia wamsubiri (hakutaka waone ni dawa ya miti gani) kisha akamaliza na kurudi kwenye kusanyiko

Hicho kipindi nakumbuka kulikuwa na jua kali sana, mazao yalikuwa yameanza kukauka maana ni kami mwezi nakitu kitu mvua hainyeshi.

Ndonkeye akatafuna yale magamba ya miti, akawa anaongea lugha yake ya Kiha akiamrisha mawingu yakusanyike upande wa mashariki kutokea pale kwenye mkutano. Aliongea sana kama nusu saa akiamrisha, kweli yakaanza kukusanyika kwa mbali sana. Aliendelea kuamrisha hayo mawingu yasogee, yakasogea kama nyuzi 90 hivi. Akaamrisha yatande sehemu kubwa kwa lengo ili mvua ikinyesha iweze kunyesha eneo kubwa. Kisha upepo ukaanza kuvuma, akaamrisha upepo utulie, nao ukatulia

Baada ya hapo akawauliza wananzengo kama wako tayari kupokea mvua, wakashangilia kwa kukubali. Akarudia tena kama wanataka mvua ilete salam kwao, wakakubali....ilipiga radi mti mkavu karibu sana na ule mkutano, mti ulisambaa wote mpaka kubakia kisiki kidogo. Wtu wengine walianguka na kuzimia, wengine waklikimbia kusikojulikana, wenye rooho ngumu walibaki. Ilinyesha mvua kubwa sana. Kisha Wajumbe waliobaki walimwambia kesho asubuhi mktano utamuhitaji tena ili aendelee kuleta mvua. Usiku saa 8 ilianza kunyesha mvua mpaka kesho yake saa 10 jioni, nyumba zilianguka, mafuriko makubwa yakatokea na hiyo ndio ilikuwa pona yake Ndonkeye. Ndonkeye na Silaus ni Waha wa huko Kibondo.
 
Ukweli uchawi Upo tena uhakika

Mimi Nina visa 3 mwenyewe kwenye maisha yangu.

Cha kwanza kilinitokea nikiwa na miaka 6 mwaka 92 na cha pili kilinitokea mwaka 2008 nikiwa mkubwa na elimu yangu kwa hakika uchawi Upo tena sana

Mwisho nilipanga nyumba mtaa wa mecco Mwanza nyumba nzuri ipo katikati ya nyumba nyingi sana nikalipa zangu kodi 1.5m kipindi hiko nimehamia mwanza kikazi Niko zangu single

Usiku nilichapwa viboko sijawahi Ona ananichapa simuoni kesho yake nikasema labda ndoto,saa 2 tu usiku bakora za kutosha,nikaamua kwenda kulala guest asee

Baada ya siku nikahama

Hii nyumba mpaka leo ipo pale mecco kwa ambao hamuamini uchawi nenda kashuhudie mwaka wa 6 haina mpangaji wala binadamu anaishi pale

Waganga na waombaji hawajafua dafu

Inasemekana walimuua mwenye nayo wakaidhurumu malipo ndio hayo.
 
Ahahaa maeneo gani eroo!
 
Mkuu unanitukana kwa lipi? Stress za ugumu wa maisha unazileta kwangu? Je wewe unaakili sana kuliko mods waliouacha huu Uzi ueleee,by the way unamtukana mtu usie mjua? @Moderator
Mpuuzi na mpumbaavu tu wewe. Dizaini ya watu wenye mindest kama yako ndiyo milele wanalirudisha nyuma taifa la Watanzania. Wewe endelea kufukazana na ngiri kijijini kwenu karne ya 21 unaleta ujinga kama huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii niliisikia Morogoro na mganga hadi leo ana athari nguvu zote kwisha kabaki jina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uuuwiiii hatari hii,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika kijiji chetu M.kulikua na mzee mmoja naitwa Kapesa Alitangaza kukihama kijiji chetu ikapita kama miaka5 hivi akaja mganga kutoa uchawi pale kijijini walipofika kwa Yule mzee alipo hama mganga akacheka sana kisha akauliza mwenye nyumba hii munamjua watu tukajibu tunamjua mzee kapesa na Alishahama miaka mingi2 mganga akasema hajahama yupohapa tukajua mganga anatudanganya akamwaga maji kwa Ile nyumba kilichotokea mzee tukamuona kakaa ktka kiti cha Kulala kavaa msuli yupo na mkewe anasuka mkeka .Ile nyumba Ilikua inaonekana imechaa ikawa inaonekana Ipo kawaida .askali mmoja alikua haamini uchawi alikubali na kumpa mkono mzee kapesa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hahahahaha

Umenikumbusha mbezi beach makonde Kuna mjengo wa maana ukilipa kodi hulali..unakutana na vimbwanga hatari..Mara usiku vyombo vinaangushwa ukiamka asubuhi unakuta na nyayo zilizokanyaga maji kuanzia jikoni hadi sebuleni..

Kuna rafiki wa dada angu alipangiwa na mzungu wake ..akawa anamwambia nyumba ina mauza uza mzungu haamini..siku aliyolala pale aliyoyaona mbona aliondoka na mwanamke wake usiku uleule hata Kodi hakudai..

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…