Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Mi mwaka 2018 nikiwa BTP(Field) shule X mkoani Mwanza kuna dogo alipewa mkoba na babu yake then baada ya kufika shuleni dogo alianguka chooni na kupoteza maisha

Mwaka huu 2019 nikiwa BTP(field) katika taasisi x hapa nchini nilishuhudia binti mmoja aliyekuwa anasomea ualimu ktk taasisi hyo akiugua na kuwa bubu wakati pindi nariport alikuwa mzima kabsaaa. But mpaka namaliza tp alikuwa bubu.Hayo ni currently tu ila nikianza kuandika hapo sitomaliza.

Mwisho kabisa kuna jamaa alilala na mwanamke alipomaliza uume hukuweza kusimama lkn alinieleza nikampa dawa hivyo alipona hii imetokea mwezi uliopita hapa Arusha. Nina shuhuda nyingi sanaaaa
 
Mwaka 2013 nahitimu chuo nikiwa mzima wa afya na michakato yangu ya kuingia jeshini ikawa imepamba moto
Ghafla nikakumbwa na upofu, nikawa sioni, Amana hospital wakasema nenda muhimbili, nakumbuka muhimbili nikakutana na dokta mmoja kuleee clinic ya macho, akanchana live kuwa mie nshakua kipofu mishipa ya macho imesinyaa bora nirudi home tuu
Nikashauriwa na wadau mbalimbali niende CCBRT nako kuchekiwa yale yalee, ila sababu haijulikani
Nakumbuka mfanyakaz mmoja wa hiyo hospital alimstua sister angu jiongezeniii
Basi bhana baada ya kujiongeza kuhangaika huku na hukoo leo naona tena
 
Pole sana mkuu
 
Kipindi nasoma lutheran junior seminary morogoro tulikuwa tunatoka kila weekend kwenda vigodoro siku iyo tulienda chakaribu ila watu walikuwa wengi sasa kwenye vigodoro kuna watu wale wanauza vimishikaki na bublish na vimahindi vya kuchoma mmoja wao akamwambia rafiki yangu niliekuwa nae anunue chochote kiukweli hatukuwa na pesa ila yule jama akaforce sana ila ukweli hatuna kitu yule muuzaji sijui alifanya nini ila mkono wa kulia wa rafiki yangu ulipotea hiv hiv nikiwa naona kwa takribani dakika nne tunamuomba jamaa aurudishe ni ukweli hatuna kitu mpaka ukarudi baada ya hapo akatupa muhindi wa kuchoma aiseee sintokaa nisahau

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]mlikoma aiseee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2013 nahitimu chuo nikiwa mzima wa afya na michakato yangu ya kuingia jeshini ikawa imepamba moto
Ghafla nikakumbwa na upofu, nikawa sioni, Amana hospital wakasema nenda muhimbili, nakumbuka muhimbili nikakutana na dokta mmoja kuleee clinic ya macho, akanchana live kuwa mie nshakua kipofu mishipa ya macho imesinyaa bora nirudi home tuu
Nikashauriwa na wadau mbalimbali niende CCBRT nako kuchekiwa yale yalee, ila sababu haijulikani
Nakumbuka mfanyakaz mmoja wa hiyo hospital alimstua sister angu jiongezeniii
Basi bhana baada ya kujiongeza kuhangaika huku na hukoo leo naona tena
Aisee noma mzee.. Uchawi haufaii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna rafiki yang mmoja wakat tupo watoto ilikua inasemekana kwamba kwao ni Wachawi
Siku moja katika kuchezacheza jioni yule rafiki yang akanichania shati langu nikawa namdai anishonee yeye akawa hataki tukaenda hadi kwao bado namuambia kanishonee shato lang, tulivyofika kwao mi nikavua lile shati nikamuachia pale mbele ya mama yake nikamwambia kanishonee shati langu kesho nakula kulichukua

Mimi nikarudi nyumbani kitumbo wazi, nyumbani mambo yaliendelea kama kawaida tumekula chakula tumefunga milango yote tumeingia kulala, naamka asubuhi nalikuta lile shati la kuchanika nliloliacha kwa rafiki yangu lipo juu ya kiti

Aisee tangu siku hiyo ndo tukahakikisha kua hawa ni Wachawi laivu na sikumbuki kama tuliendelea kucheza kama marafiki nikawa namuogopa sana.
 
Watu wengi hawaamini uchawi mpaka yawakute. Kwa upande wa ukoo wetu mtu hawezi kutuambia lolote eti tusiamini uchawi maana tuna shuhuda za kutosha: Ya kwanza nimeishaisimulia ya bibi yetu kuchukuliwa meno yote usiku mmoja na kubaki kibogoyo maisha yake yote. Tukio ka pili ni babu yetu kupachikwa mfupa mkubwa wa samaki ndani ya mguu kuanzia kwenye ankle mpaka gotini na ulitolewa kwa operation hospitalini na wazungu walioshangazwa na sayansi hii ya sisi waswahili. Mfupa huo tumeutunza mpaka leo kama kumbukumbu.

Tukio hilo la mfupa lilianza kwa mzee mmoja kumwomba babu samaki aliyetoka kumvua. Babu alikataa kumtoa huyo samaki kwa kuwa alikuwa ni huyo huyo mmoja na ndiye alitegemewa kwa kitoweo cha siku hiyo nyumbani.

Babu alianza kuumwa mguu siku hiyo hiyo usiku hadi akaanza kushindwa kutembea. Maumivu yaliongezeka kadiri siku zilivyokwenda na matibabu yote aliyopewa hayakufua dafu. Babu alikuwa akilia kama mtoto mdogo kwa maumivu na ilimchukua mwaka mzima akiwa ni mtu wa kitandani tu.

Siku ya ukombozi kwa babu ilitokea pale hospitali yetu ya mission ya KKKT ilipopata wataalamu wa kizungu. Walipomfanyia operation waliutoa mfupa mkubwa wa katikati wa samaki ulionyoka toka kisiginoni hadi gotini. Tukabaki tunashangaa tulipoitwa kuushuhudia mfupa ule

Tukio la tatu ni mama yetu mdogo kutolewa vipande vya ngozi mbichi ya ng'ombe na makongoro tumboni hospitalini hapo hapo na wazungu hao hao waliomtibu babu. Hivyo vitu viliingiaje tumboni na kumsababishia maumivu makali mama yetu? Kazi ya mama yetu ilikuwa ni kuuza supu ya makongoro iliyovuta wateja wengi kwa jinsi alivyoitengeza vizuri. Wivu wa kibiashara ulimgharimu na kidogo apoteze maisha maana alidhoofika sana. Wa kubisha hayajamfika, na aendelee kubisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom