Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nikipita bila kusema nitakuwa sijampa Mungu wangu utukufu anaostahili! Kiukweli nilikuwa nazisikia habari za nguvu za Giza na nilikuwa muombaji wa kawaida tu hadi hapo siku moja ndan ya mwaka huu nilisikia upepo mkali umenivamia mapigo ya moyo yanaenda mbio na mwili wote unatetemeka mithili ya mtu mwenye kifafa! Nilishuhudia mengi baada ya hapo! Hospital walisema nimepata hypertension na moyo unashida nikapewa referral ya muhimbili kitengo cha moyo.

Pale muhimbili nilipima vipimo vyote vya moyo na nilionekana sina shida yeyote.Kuna rafiki yangu mmoja aliniambia upepo ndo ukaanza kuwa hivi hauumwiii twende kwenye maombi, nilishuhudia sura yangu inageukageuka, nilishuhudia nina vidole zaidi ya 10 mkono wa kulia it’s like vingne vinatoka vingine vinabaki! Nilitapika stepo pins nikashuhudia kwa macho yangu! Ninachoweza kusema Nguvu za giza zipo na Mungu yupo na unapomuita anaitika! Nimebadili mfumo mzima wa maisha yangu na hakika Mungu amenikumbatia!

Ilinichukua miezi miwili kupambana na ile hali.Kuna muda upepo ulikuwa unakuja nasikia kabisa kicheko chenye mwangwi, mwanzo nilikuwa siwez kufanya kitu zaidi ya kupiga ukunga baadae nikawa naweza kuita damu ya Yesu na kuifunika nafsi yangu kwa damu ya Yesu.. hili ni funzo kubwa sana kwangu mwaka huu wa 2019! Yani upepo ulikuwa unakuja ni naomba namuita Yesu inaweza chukua dakika 10 hiyo hali lakini mwili unavyotweta jasho....Jamani tumkimbilie tu Yesu! Atupe jicho la rohoni tuone yaliyojificha
 
Nakumbuka miaka ya nyuma niliamua kuanzisha biashara ya bar maeneo ya wazo hill, target kubwa ikiwa ni marafiki zangu ambao walikuwa wanafika sana kwa mwanangu mmoja ambaye alijenga huko na wanakunywa sana hata idea ya kuanzisha iyo bar walinipa wao kwa sababu ilikuwa ndio michongo yangu

Ile bar ilianza vizuri sana na mimi binafsi sikuwa hata na muda wa kwenda sana huko ila nilimuachia dada mmoja mchakarijaji kweli kweli kama manager mimi weekend mnaenda kufunga mahesabu

Iyo siku balaa lilianza kuanzia mida ya saa moja usiku hamna mteja yoyote aliyefika pale na siyo kawaida mida ya saa 3 usiku wakaja watu wawili kila mmoja na gari yake mwanamke na mwanaume, mwanamke akaagiza kreti nzima ya soda, na mwanaume akaagiza ya bia, na wanataka ziwepo hapo hapo walipokaa, mhudumu akaenda kuchukua walivyoleta wakakuta wameongezeka wamekuwa wanne na hapo walipokaa ni juu kwenye ghorofa na kupita ni lazima mtu wa counter chini akuone...mhudumu akawauliza mbona sijawaona mkipita wakasema sisi tumekuona ongeza kreti ya soda na bia, akawabia kunyweni kwanza hizo wakamkazia macho akaenda kuongeza na bia wanazotaka na soda ni za aina zozote zilizopo, muhudumu kirudi akakuta wapo 8, na gari nje zimeongezeka, akaambiwa aongeze tena 8, zile 2 za mwanzo zimeisha, akampigia mtu wa bia za jumla amletee japo alikuwa amefunga akakubali

Zilipofika kupanda juu akakuta wameongezeka wamekuwa wengi na hakuwaona wakiingia ghafla akamuona mmoja anapiga hatua kupanda juu, yani yupo parking kapiga hatua kupanda ghorofa ya kwanza, alizimia hapo hapo jamaa wa jikoni alikuja kukutwa amepooza baada ya kutibiwa kiasili alipona na yule wa counter aliokotwa kwenye kile kibwawa kisichokauka pale wazo ukielekea madale, hizo taarifa ziliniogopesha sana na uwekezaji wangu ukaishia hapo hapo sikuwahi hata kufuatilia kijiko pale...kumbe mwenye nyumba alikuwa na mambo yake alinipigia simu nikamwambia nimesafiri hivyo vitu avichukue
 
Naona kitumbua kishaingia Mchanga
Wewe Kiranga umekuja kuharibu uzi

Sasa kama unataka kujua uchawi upo tumia hiyo hela hapo $1000 tafuta Mganga yoyote yule mkali Hata mkoani nenda, Mpe hela mwambie naomba nioneshe uchawi
Kivyovyote Utaoneshwa Hata ukitaka akufanyie Wewe anakufanyie
As long as umpe hela na ufate masharti yake
 
Naona kitumbua kishaingia Mchanga
Wewe Kiranga umekuja kuharibu uzi

Sasa kama unataka kujua uchawi upo tumia hiyo hela hapo $1000 tafuta Mganga yoyote yule mkali Hata mkoani nenda, Mpe hela mwambie naomba nioneshe uchawi
Kivyovyote Utaoneshwa Hata ukitaka akufanyie Wewe anakufanyie
As long as umpe hela na ufate masharti yake
Yani unapewa offer ya $1,000, halafu kazi unataka niifanye mimi ninayetoa offer?
 
Marias, Mkuu kuna vitu tumefanana na hali iliyowahi kunitokea.....huko kusisimka mwili usiku nmezoea na ni kama tu nimenena kwa lugha mda mrefu na kumzingua alieingia room..... Mara zote kwenye hatari ambayo roho yangu inaona naweza angamia Yesu huwa anaingilia kati uoga unaondoka na naanza nena.... Uzuri nashukuru naweza fungulia baraka za kunena kwa lugha... Pole sana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cjawahi kuona mazingahombwe live Ila nimekuwa na tatizo la kuishiwa damu na hata Nile nini kuipandisha ni mitihani. Hili tatizo Sikuwa nalo kabla. Tatizo lilinianza baada tu ya kuishi wilaya flani kibiashara ambapo nilipigwa vita sana niifunge ile biashara nikakomaa.
Wanasema hivi,Ni Jini Makata as soon as possible utakata Moto.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani niongee kidogo kuhusu swali lako, sijajua kama umepata majibu maana comments ni nyingi kidogo siwezi kuzisoma moja moja hadi mwisho.
Kutokana na hii Hali. Napenda kujua mchawi na mganga.je ni halali kwenda kwa mganga sababu unahisi mauzauza au kuchzewa kichawi?na je ni uchawi kweli unaweza kumfanya mtu awe chizi?tusaidiane kwa hili kwani sikuwa napenda kuamini kuwa ushirikina upo. Pili waubiri wengi wa Sasa hutupelekea kuamini uchawi upo na kulogwa kupo

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom