Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Nina chapter mbili (2), moja ya kwangu ma ya pili ni ya baba yangu,
Nitaanza na yangu mwenyewe..
Mwaka 2016 nikiwa na umri wa kati tu usio na tija kuwa mme wa mtu, ila kutokana na misukumo na vishawishi vya barehe ikanibidi nivute kibinti cha kiislam, kutokana na kuwa nilikuwa mpambanaji wazazi wake waliniamini na kunipa mtoto wao japo sikuwa na kigezo hata cha kuoa wakati ule (20+ yrs only) sasa basi baada kufanya process zote ilibidi niowe kiislam kutokana na kuwa waslam hawana mambo mengi(mimi sio muislam wala sina mpango wa kuwa), yaani wao hata mkiwa watu 10 ndoa inatamadadi na kukwishineyi...sasa wakati ule wa binti kuvundikwa baadhi ya wenyeji, dungu&jamaa walianza kumletea zawadi za hapa na pale, baadae ndoa ilifungwa na maisha ya ndoa yakaanza rasmi, sasa kimbembe kilianza baada ya yeye kutoka kwao tu, yaani binti yule akawa mgumu kutoa papuchi ilihali alinipenda mwanzo na alilia ndoa kwa udi na uvumba sasa nikawa najiuliza huyu vipi, ama ananiectia..basi kwa akili zangu za ujana ujana nikawa na-force game, kisha kibishi namaliza ila alikuwa analia sana kana kwamba alifosiwa kuolewa..
Baada ya zile siku saba za mwanzo baada ya ndoa (honey moon) huko kijijini kwetu, tukawa tumejisogeza maghetto kwangu ili tuyaanze maisha yetu wenyewe, sasa hapo ndipo picha lilianza yaani binti kuanzia asubuhi-saa12 mzima kabisa yaani yupo shwari kimbembe ni ile kigiza cha usoni kikianza kuingia yaani alikuwa mwehu kabisa, sasa nikaanza kujiuliza hii imekaaje ama ndio mke ana act ili asitoe mchezo, basi ikabidi nitoe taarifa ukweni maana hali ifikia pabaya sana,
Sasa wakawa wameniambia kuwa jambo hili linavinasaba vya kishirikina, kwa upande wangu sikuamini hata kidogo, sasa bibi wa mke wangu mzaa mama mkwe alikuwa ni mrokole kindakindaki, basi wakawa wame- organize mama&bibi ili mtoto wao atibiwe hayo maswaibu..basi bana siku hiyo nakumbuka niko zangu ghetto sina hamu hata kidogo na ile ndoa si mama mtu akaja na yule Bibi akiwa na wenzake na mama zake wadogo, mama mkwe na wadogo zake ilibidi wabaki nje kutokana na kulinda itifaki ya kutoingia chumba cha mkwilima wake,
Wakawa wametutaka siye wanandoa tupige magoti ili ombi lianze humo humo ghetto, mwanzoni me nilikuwa na- take easy tu nahisi kama vile movie za kibongo, lakini baada ya ombi kukolea nikamuona wife kaanza kupiga mwano, wakabidi wakomae nae me nipo nacheck tu (ilibidi nifumbue macho[emoji16]) ombi likawa ombi daaah mara mtu chini wapo nae tu, mara wakaanza kuyahoji majini baada ya yule binti kuanza kusema mtuache, mnatuchoma..sasa hapo me siamini tu baada ya kuzungumza nayo yakawa yamesema kuwa pindi binti yule anafundwa ndani siku zile za kuvumdikwa kuna mtu alimpea under wear (chupi) kupitia kwa mdogo wake, yeye pasina kujali akawa kaivaa, na ndipo yalianza maswaibu..me bado hapo sina imani tu na kile kinachoendelea, baadae kabisa baada ya ombi kukolea yule binti akaanza kutema nyama nyama kama stake hivi ila zipo mithiri ya damu iliyoganda, wakachukua mtandio wake wakaanza kumtoa zile nyama mdomoni pia alikuwa anatafuna meno kiasi kwamba unasisimuka kama mtu anae sugua sifuria, hapo sasa ndio nikaanza kupata imani kuwa kweli binti yule ana jambo tena kubwa tu, baada ya ombi kumchek yule binti mdomoni nilishangaa hakuwa na jeraha wala kovu ambalo lilisababisha kutoa nyama zile tena zimejaa kwenye mtandio wake wa kiislam..mzee nilidata mpaka nikakoma na kimbelembele changu cha kuyakimbilia mapenzi,
Baada ya ombi lile tukawa kama temeyaamsha, na siku zilizofuata ndio kikawa kimbembe zaidi ya mwanzo, maana kuna usemi unadai kuwa kama wewe umeombewa na kutokwa na majini basi unatakiwa uishike imani sana sana laasivyo huwa yakitoka 10 yanarudi 20 it means (2x2), sasa sisi tuka- take easy kabisa, yaani majanga yalizidi mpaka kufikia hatua ndoa kuota mbawa ndani ya mwezi mmoja tu(mpaka sasa nipo single, na sina hamu kabisa ya kuwa na mke).
Yaani yule binti alipoteaga, wazazi wake waliuza nyumba ili kumtafuta binti yao kwa wataalamu, walimpata baadaya ya mwaka mmoja (2017) ila waliyumba sana kiuchumi na kuhama mji waliokuwa wanaishi na kwenda kwingine kuanzisha maisha tena ya upangaji, baba mkwe wangu na baba yake mzazi mpaka leo hawasemshani maana ktk jopo lililohusika na hizo inshu pia mke mdogo wa huyu babu wa mke wangu alihusika sana, pia huyu babu hakuwahi kusimama kumtetea mjukuu wake wakati wote alisema kuwa mkewe anasingiziwa huenda ni kutokana na limbwata ama juju alilopewa na huyo mke wake

NB: pia kipindi tunamuuguza mke wangu tuliwahi kwenda kutibiwa kwa mmoja wa bibi zake wa ukoo tukiwa huko, me nyege zikanizidi ikabidi nimuombe show wife maana tulilala kitanda kimoja, alivyogoma kutoa mechi ikabidi nitumie force maana nilikuwa na kama wiki kadhaa pasipo kufanya chochote kwake na isitoshe kwa wakati huu alikuwa keshapona(hapandwi na majini wala hakuwa kichaa), yule bibi alituachia room ambayo ilikuwa ndio kilinge chake, Aiseee nakumbuka wakati na-force kuchojoa chupi nae hayumo kelele zikawa kibao wakati huo ni kama saa11 alfajiri, mara paaap nasikia sauti kwenye angle ya kuta ikisema shiiiiiiiiii, daah nilitoka nje nikiwa na boxer yangu tu hapo nipo kifua wazi nikamfuata yule bibi akaniambia nitulie tu nikiwa ndani maana kilingeni huwa hakuhitaji makelele, sikuomba match tena wala sikusinzia mpaka kunapambazuka kisha nikasepa zangu kurudi mjini..[emoji125][emoji125][emoji125][emoji125][emoji125]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kaka ulikosea sana kumpa ushindi shetani na wachawi? Ulishajua ushindi upo kwenye maombi kwanini ulienda tena kwa waganga nyumbani? Damu ya mwanao itakulilia daima.maana hajafa amekiwa msukule labda.

Sent using Jamii Forums mobile app
mtoto mchanga hawezi kuwa msukule, walichukua viungo vyake wavitumie kwa mambo yao ya kichawi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nia visa viwili vitatu.

Cha Kwanza:
Mwaka 2004 tukiwa Dodoma Wilaya ya Kondoa Kijiji kinaitwa Mondo.

Kuna Jamaa tulikuwa tunapiga nao mishe hapo bush halafu Washikaji walikuwa Wazee wa Totozi na tunaishi chumba kimoja ambacho tulipewa na mwenyeji wetu.

Mmoja Kati ya Wenzangu alimlamba Mke wa Mzee Mmoja pale bush wakati sisi Wengine tumeenda Kondoa Mjini.

Usiku wake Sasa ilikuwa ni balaa.... tuling'atwa na SIAFU kiasi ambacho ilibidi tutoe Godoro na Nguo zote hadi tulizovaa Nje.

Tukaenda kuchukua Mashuka kwenye mabegi na kulala kwenye Chaga za Kitanda lakini siafu wapo palepale.

Tukachukua magazeti na kuwachoma Moto lakini ile tunarudi kulala shughuli ipo palepale.

Kiukweli hatukulala kabisa hadi Asubuhi na kadhia ilikuwa Chumbani kwetu tu.

Ilipofika Asubuhi hatukuona hata Siafu aliyekufa wala Mzima licha ya kupekua huku na kule.

Jamaa yetu aliyefanya Kosa baada ya kutishwa ikabidi amuombe Mwenyeji wetu akatuombee Msamaha, hapo hali ikawa Shwari.

Kwa lile tukio nilisema SHIKAMO.. WARANGI.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mshukuru hamjatumiwa fisi
 
Mwaka 2005 hapo Tarime Secondary kuna jomba mmoja alikuwa ni classmate Msukuma huyo kutoka Magu ndani huko aliitwa Kija Charles.

Hiyo siku tupo prep, kuna mdada mmoja alikuwa na majini, akapandisha bana siku hiyo, watu taharuki, sasa yalivyokuwa yanazungumza yakamtaja huyo mlozi na alichotaka kumfanyia akashindwa. Kumbe yule jomba alishatomber dorm moja zima, la pili alikuwa kafika nusu, wadada wakaandamana kumtafuta huku kelele zikiwa zimetamalaki madarasani. Hakuonekana shule karibia wiki nzima.

Kumbe jamaa alikuwa anawatomber kichawi
Kha nimecheka
 
Hebu nisimulie hiki kisa changu...

Jumanne 23-08-2019.

Ilikuwa saa nne na nusu usiku nikiwa nimeketi sebuleni,mara gafula mzee akatoka chumbani na kuanza kunitukana matusi ya nguoni...

"Kijana gani wewe kazi kula na kujaza choo,huoni wenzio wanafanya kazi na wanategemewa na wazazi wao...ni bora ningezaa hata mbuzi ningefaidi mchuzi.."

Mara ghafula nashutuka kofi hili hapa sijakaa vizuri ngumi hii hapa,nikasimama imara na kumkazia tu macho...wadogo zangu na mama yangu wakitazama tu pasi na kusema neno.

Nikageuka taratibu na kutoka nje,chozi la uchungu likanitoka ilikuwa ni siku mbili tu toka nifukuzwe shule moja niliyokwenda kuomba ajira ya kujitolea..ati hawawezi kuajiri kiziwi!.

Nilitazama anga jeusi lililosheheni nyota nyingi,mwezi uliotoa nuru angavu nikajiuliza "Mungu upo wapi?".. Nikaingia chumbani na kuvaa viatu.. Nikatoka naenda wapi? Sijui!

Nikaambaa nisijue kama nakanyaga ardhi au ninapaa,napishana na mtu ama kisiki,ilinichukua nusu saa kuuacha mtaa wetu nikaingia mtaa wa pili,huu ulikuwa na watu wachache zaidi na nyumba zilikuwa mbalimbali kiasi.

Nikakatiza pembeni ya makaburi,nikasimama,nikayatazama na kujiuliza " kwanini nisingekuwa nimelala pale? Nipumzike!"...loooh lakini sauti nyingine ikaniambia "una uhakika ukilala pale utapumzika? Nikagutuka nikatazama huku na huko hakuna kiumbe nikaongoza njia kuliacha eneo la makaburi na kuzidi kupotelea mbali zaidi na nyumbani.

Hatimaye nikawasili sehemu pweke,barabara kubwa ya kokoto,kulia na kushoto kukiwa na msitu na vichaka vingi,kiza ni kingi kutupia macho simu yangu ni saa sita na robo usiku!

Ikafika mahali kuna njia panda na upande wa kulia kuna mti mkubwa sana aina ya mbuyu mahali pana pana joto sana bwana,pana joto kali,mapigo ya moyo yakanienda mbio " duuucha dunduncha ducha dunduncha" sasa mapigo niliyasikia hadi masikioni..

Nywele zikanisimama na vipele vya uoga vikanitoka hewa ikawa nzito na uvumilivu ukaniisha na sasa nikatimua mbio hata nilipoliacha eneo lile kwa umbali wa mita mia mbili hivi,na sasa nikaanza kutoka katika makazi ya watu.

Kufika hapa ikanipasa kujiuliza ni wapi naelekea,sikuwa napajua napoelekea kumbukumbu ya misukosuko ya kimaisha na masimango yasiyoisha zikanijia,woga wote ukabiisha donge zito la uchungu,hasira na kukata tamaa likanivaa,machozi yakanitoka,nikashika njia na kuendelea na safari,safari isiyojulikana!

Baada ya mwendo wa dakika ishirini hivi nikaingia katika barabara kubwa ya lami,nikashika uelekeo wa kushoto,ilielekea ufukweni,baada ya masaa mawili hatimaye nikawasili ufukweni,nikazitupia macho hoteli kadhaa zilizotamalaki eneo lile,nikaachana nazo na kushuka mchangani mbali kidogi na mahoteli yale,nikajikalisha kitako na kutafakari nilipotoka,nilupo na ninapoelekea,lakini mbona mbele kyna kiza kizito!

KIZAAZAA!

Hatimaye saa tisa ikawadia,nilichoka,na sasa ilikuwa ni safari ya kurudi,nikajizoa zoa na kushika njia kurudi nyumbani,bahati nzuri barabara hii ilikuwa na taa hivyo ikawa ahueni kwangu.

Baada ya mwendo wa dakika arobaini hivi nikahisi kama kwamba kulikuwa na mtu nyuma yangu,nikageuka kwa kasi, ebo! Nikaona nguo ya rangi ya khaki,aidha gauni au kanzu ikiishia na kufutika machoni kwangu....

Mshtuko uluonipata ukanifanya hata nguvu za miguu ziniishie nikajikuta nikiketi katika mfereji mfupi uliojengwa pembeni ya barabara.

"Ni nini hiki? Ni kweli au ni mawazo yangu tu?" Nikajiuliza,nukatazama huku na huko hali ni shwari,labda niliangalia vibaya bwana nikajizoazoa na kuendelea na safari..

Kiroja kingine tena! Ati nina vivuli viwili,kimoja ni changu na kimoja kimevaa kanzu kama si gauni!(mataa ya barabarani yanawaka hivyo mtu akipita kivuli chake kinaonekana kwa ufasaha kabisa) nikatetemeka kwa woga,nikageuka nyuma ati nacho kikageuka! Nikawa natembea kwa kurudi kinyume nyume,ati nacho kinarudi kinyume nyume!.

Lakini mbona kivuli changu kupo mbele yangu hiki cha nyuma ni cha nani? Na tumeachana umbali wa hatua kama tatu hivi toka kilipo hadi nilipo,nikaona huu sasa utani,nikifa si nife tu ebo! Nikakata shauri kukifuata he! Ati nacho kinageuza kila nikikifuata nacho kinaenda nyuma zaidi,ikabidi nikikimbize sasa..kikapotea.

Nikageuka na kuanza kukimbia kwa taratibu mithiri ya mbio za riadha,nikachoka nikaanza kutembea baada ya mwemdo mrefu kivuli kile kikarudi! Sikusimama nikaendelea kutembea tu.

Hata hivyo nikaanza kuhisi mwili kuchoka sana,miguu inauma na usingizi ni mwingi sana,nikajikalisha juu ya ukingo wa karavati kutafuta pumzi maana ilikuwa ni safari ya masaa mawili zaidi hadi nifike nyumbani...nikaanza kusinzia na hatinaye fahamu zikakomea hapo.

Kelele za watoto wakicheza ndizo zilizonigutusha,nikafumbua macho..afanalek! Nilikuwa nimelala chumbani kwangu..miguu ilikuwa imevimba kiasi na mwili mzima ulikuwa unaniuma...

"Lakini mimi mbona nilikuwa kule barabarani?" Nikajiuliza nisijue kilichotokea,nikaamka na kulibinua bati ninalotumia kama mlango,nikapenyeza kiubavuubavu hadi nje.

Nikawatazama nyusoni niliowakuta nje,wapo kawaida,hawana hata habari,pengine niliokotwa na wasamaria wema! Lakini mbona watu wapo kawaida kama hakuna kitu?...nikashindwa kuvumilia nikaamua kumuuliza mama ni muda gani niliingia kulala!

Akanijibu "we si uliingia kulala saa nne weww? Maswali gani hayo usinisumbue" ni nani aloyenirudisha nyumbani,na kile kivuli ni kiumbe gani? Je ndicho kilichonirudisha nyumbani? Lakini hakijanidhuru, hili ni fumbo niishilo nalo hata sasa kuna wakati natamani kukiona tena kivuli kile kilichovalia kanzu au gauni lililopauka lakini hakitokei tena.

Duh
 
Mwaka 2006 nipo Depo mkoa fulani, tulikuwa na utaratibu makuruta kwenda lindo usiku, na zamu ilikuwa ni vyumba, sasa siku hiyo ilikuwa zamu yetu tukaenda lindo mimi na washikaji wawili ambao tulikuwa tunakaa room moja, tukamuacha mmoja analinda room yetu.
Lindo letu lilikuwa karibu mtoto mkubwa, tumefika pale mida ya saa nne ilipotimu saa 7 usiku mauzauza yakaanza wale washikaji wawili wakaanza kupiga kelele kuweweseka kama vile wanagombana na mtu, "hatuji huko, hatutaki" nikawauliza ni nini hawanijibu, baadae wakakimbia wakaniacha mwenyewe kwenye lindo, baadae walikuja na guard commander wakadai kuna mtu alikuwa amekaa katikati ya maji alikuwa anawaita na kuwavuta kwa nguvu.

Kesho yake tumelala chumbani mmoja wa vijana akakimbia akazima taa ya chumbani akatulazimisha wote tujifunike blanket kuna mgeni na akatoa tahadhari atakayechukungulia atakiona, baada ya dakika moja nilisikia kishindo chumbani kama mtu ameshuka toka darini, baada ya robo saa nikasikia yule kijana anaongea anamuaga mtu.
Asubuhi tumeamka kijana amechanjwa chale mwili mzima, nilipomuuliza akasema ndugu zake walikuwa wamekuja kumtenengezea dawa kutokana na masahibu ya jana yake, kijana alikuwa mtu wa Rukwa.

Story ya pili.
Tupo lindo usiku tena tulikuwa watatu tena (sio wale wa mtoni) sehemu tuliyokuwa lindo ni njia ambayo raia wa kawaida hupita wakienda makwao, sasa siku hiyo mida kama ya saa sita kuna njemba moja ilipita, vijana wakaruka nae, pigwa sana, akagaragazwa sana, mimi nilikuwa nimepitiwa na usingizi, niliposhtuka nikawakataza wale wenzangu tukamwaachia akaenda zake, baada ya nusu saa yakaanza mauzauza, walikuja bundi wawili wakatuzunguka, halafu wakaondoka ghafla wale wenzangu wakaanza kuchapwa fimbo, chapwa sana lakini hawakimbii wanalia wanaomba niwasaidie, ilibidi usiku huo tutafute wenyeji waende kuomba msamaha kwa ile njemba iliyogaragazwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi sijawahi kutana na hayo mauzauza, na ninaomba MUNGU nisikutane nayo maana nitakufa hapo hapo. Ila kuna visa viwili nilihadithiwa na wazee wangu.
Cha kwanza ni baba yangu mzazi, wakati akiwa kijana barobaro alikuwa anapenda sana kutembea usiku. Alikuwa anaishi maeneo ya Tegeta. Siku moja wakati anarudi usiku akiwa anatembea akawa anasikia kama kuna mtu nyuma yake anamfuata ila akigeuka hamuoni, akakaza mpaka akafika magetoni. Akajiandaa kulala akafunga mlango na kuzima taa akapanda kitandani.
Wakati bado usingizi haujampitia vizuri akawa anahisi kama mtu anafungua mlango kwa nje anamchungulia, akapotezea akalala. Katikati ya usingizi akahisi kukabwa na mtu akiwa amelala, akajitahidi kujitetea lakini bado, akajaribu kupapasa akahisi ameshika jitu lenye manyoya mengi sana mikononi kama manyani yale. Hapo ndo akajua shit just got real. Akaamka akawasha taa hakulala mpaka asubuhi. Alikuja kusaidiwa na mzee mmoja hv alikuwa anakaa mwenge almaarufu kama Babu wa Mwenge marehemu. Akamwambia lilikuwa jini alikumbana nalo njiani. Lakini bado since then hakukoma kutembea usiku.

Cha pili ni mama yangu. Ni mchaga wa rombo, anakwambia zamani walipokuwa mabinti wadogo kulikuwa na majitu yanaitwa "Mangauneri" wajuzi mtanisaidia. Walikuwa kama binadamu tu wanakuja hadi nyumbani mnakula nao chakula cha usiku ila wanakijiji walikuwa wanayajua kwa hiyo wanamkaribisha tu akimaliza chakula anaaga anaondoka. Sasa baada ya hapo ni kuwasha moto mkubwa maana akiondoka anasikilizia mkishalala anakuja anachukua vijinga anawachoma navyo especially matakoni. Waliokuwa wanapasua mbao porini walikuwa wanakutana nao sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mangaunieri Ni vile tunaita vibwengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona zipo kila mahali? Kwa mfano nenda jukwa la wakubwa kule utaona live watu walivyotiwa giza kwa wanayojadili na kuyashabikia. Nguvu hixo xinatenda kazi hata sasa, ila wengi mnadhani ni tunguli tu.

Sent from my SM-T355Y using Tapatalk
Na wewe huwa unaenda mtumishi?[emoji16][emoji16]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna mama mmoja hapo Lindi, mwanawe wa kiume alioa, sasa yule mama hakumpenda binti aliyeolewa na mwanawe...... Akaenda kwa mganga ili awaachanishe, mganga akamwambia atampa dawa ambayo mtoto wake akilala na mkewe atageuka nyoka, yule mwanamke ataogopa atadai talaka,,, basi huyu mama akakubali mganga akatoa dawa, yule mama akamuwekea mwanawe kwenye chakula, ikawa ikifika usiku yule kijana akilala na mkewe anageuka nyoka, yule mwanamke kavumilia wiki Tatu, ikabidi aende kwao, wazazi wake wakamwambia afate talaka, akafuta na akapewa..... Kazi ikabaki kumrudisha kijana kwenye hali ya kawaida, yule mama akarudi kwa mganga kumwambia kazi imekamilika, hivyo anaomba mwanawe arudi kibinadamu, mganga akamjibu "nina dawa ya kumtengeneza awe nyoka tu sina ya kumrudisha kwenye hali ya kawaida" yule mama aliliaaaa,,,,,,.... Na huku home kijana anamwambia mama yake afanye amrudishe kwenye ubinadamu wake, basi hapo nyumbani taflani

Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseee
 
Back
Top Bottom