Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Mkuu line yangu sija sajili kwa alama za vidole shusha story yako before sijatoka hewani [emoji120][emoji120]
Hizo ni lugha za kuzimu. .....

Yani najua mambo ya kichawi utadhani nami ni mchawi. . Hawa mahousegel muwe mnawapeleka Makanisani/ nyumba za mungu mara tu wanapofika kwako jamani! ? kisa kilianzia kwa housegal

Thanks God

Cc Smart911



Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kanisani kwetu mpaka sasa kuna binti mmoja aliekufa 5 years. . Badae alionekana akiwa kama huyo. .minywele mirefuuu kucha ndefuu yani alivo kwa mara kwanza ukimuona unaeza dhani ni mzukule. .The way anavokula sasa ... hata yeye anaongea lugha ambayo hatuielewi kabisa. .


Cha kushangaza hio lugha aliyokuwa anayoongea alielewana na kusikilizana na binti yangu wakazi kipindi nimempeleka binti kanisani kwenye maombi ya kufunguliwa baada ya kutaka kunifanyia mauzauza ya kutaka kuua . Binti yangu wakazi hapo kanisani kwenye maombi Kuna kipindi alikua sawa na anaongea kawaida tu ila wakianza kumuombea tu mapepo yanapanda anabadilika..anaongea lugha ambayo hatuielewi. . Ila alielewana nahuyo binti mwingine alieonekana baada ya kufa kwa miaka 5 iliyopita na ndugu zake wakampeleka kanisani. Hapo kanisani kuna muda Walikua wanaongea wanacheza wanaimba sijui vitu gani wanachekaaa sisi hatuvielewi. .. wachawi kwa wachawi wanajuana hata wakikutana wana alama zao wewe mtu wa kawaida huwezi kuziona/ kujua.
Nilishangaa sana Kwani mimi eneo hilo nilikua mgeni na binti nilimtoa sehemu nyingine mbali kabisa but alielewana lugha nahuyo mzukule wa hapo kanisani
Ni story ndefu na ina mengi ndani yake
Saint anne

Cc Smart911


Hata Mimi natamani kujua hilo,pia napenda kujua alivyorudi alikuwa na mawasiliano na kuwatambua ndugu zake?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hii kitu nishaisikia sana tu nikabisha..[emoji23][emoji23][emoji23]
Nimekumbuka hiki kisa,

Mbeya mjini nilikutana na kisanga cha kubebeshwa mkojo na wazee wanacheza drafti, bao na kunywa kahawa,
Unakuta wanacheza wewe unaenda shangaa pale (mimi nilikua nasubiri coaster za usiku za dar) nimeshangaa wee baada ya dk 20 hivi nkabanwa mkojo nkarudi kwa mwenyeji nkamuomba anielekeze pa kujisaidia, nimerudi kujisaidia naenda kushangaa na kuskiliza stori zao, yaani ndani ya lisaa nilienda chooni mara 3, nkawa najisemea mapema yote hii hata maji sijanywa mkojo mwingi hivi?
Kwa sababu nilikua na safari niliogopa kunywa maji japo nilikua na kiu sana kwa hofu ya kusumbua gari njiani kuchimba dawa,

Gari ilivyokuja nkaanza pakia carolight zangu nkamaliza nilipotaka kurudi pale kuendelea kushangaa mwenyeji wangu akaniambia twende huku (hapo tunasubiri gari ijae abiria) tukakaa mahali tunapiga stori za hapa na pale ndio akaniambia nimekuona unabebeshwa mikojo tu hata huelewi, nkabaki namshangaa...
Ndio akaniambia ukienda shangaa pale kama hauko vizuri wale wazee wakiskia mkojo wanakubebesha wewe unaenda kuukojoa badala yao, yaani wanaweza kukaa asubuhi hadi jioni hata chooni wasiende ila wee kila mda unapiga ruti tu..
Hiyo ilikua mwaka 2010 pale uyole.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Bibi yangu ni mchawi, anamtesa sana Mama yangu, anataka kumuua. Ni muda sasa mama anateseka na maradhi yasiyo pona. Tumezunguka sana... ila basi tu
Mkuu habari yako.... ninaweza kukusaidia kwa maombi (kama upo mkoa wang) au kukuelekeza jinsi ya kusali ni rahisi sana sema tu Ur Mam inabidi awe tayari kusali na kuwa na imani.....

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa kesi ya housegal wangu. .Wakati anaombewa aliongea mambo mengi sana yanayofanywa na wachawi duniani na kuzimu huko. .

Alisema kwa wale wanaokufa kwa kuchukuliwa kiuchawi na badae kuonekana/ kurudi kwenye Jamii inakua kwamba wengine wanashindwa vyakula vya huko kuzimu kabisa na wanakua na mizimu mikali sana yani ile too much ambayo kila kitu yahuko kuzimu haipatani nayo haiitaki yani mzukule hata apigwe vipi hata afanywe nini hali ngo'o akiambiwa afanye hiki hafanyi wee fanya ufanyavo mzukule anagoma kabisa mwisho wanaamua kumrudisha duniani. ..wanamrudishaje sasa hilo hakuongelea .... Au wale wanaoshindwa kutimiza mara nyingi wanayoagizwa na wakuu wao huko kuzimu yani wale vilazaaaaaa kama huyo binti yangu wakazi . Alionekana kuwa mzito sana kufuata maekekezo .
Alipofika kwangu tu mkuu wao wa uchawi aliona mtoto mchanga wa kiume wa mdogo wangu niliyekuwa naishi nae eti ana damu, nyota nzuri, pamoja na nguvu sana yani nguvu NYINGI SANAAAAAAAA Kumbe housegel huyo alikua duniani kama agent tu wa kuua watu kuwafanya mizukule, kuwatafutia damu na nyama za watu wakuu wao huko kuzimu. . Na alishaelekezwa mara kibao afanye nini tangu alipofika hapo kwangu kwa ajili ya kumuua huyo mtoto mchanga by that ime. Alipewa dawa za kumpa na kumuwekea ka changa hako lakini binti hakuweza kufanya hivo na alikua anamuonea imani huyo dada na roho inamuuma sana Kwani walikua wa naishi vizuri hapo nyumbani kwangu . shortly alikua kama ndugu yetu. Nayeye ndiye aliekua anashinda nyumbani akiwahudumia mama na mtoto muda mwingi mimi nikiwa kazini Sasa sijui kama ni kweli au laa but nimeshuhudia hayo na mpaka Leo naishi nao mama na mtoto

Katika uhalisia huyo mtoto wa mdogo wangu ana nguvu sijawahi ona. . Hata Ukimbeba ni mzito jamani jamani na ana akili sana. .Ni mtoto mdogo ila ukimuangalia mambo yake mwenyewe unabaki mdomo wazi.
Pia kwa matendo yake naezasema Ni wale talented ones

Ni story ndefu yenye mengi.
ThanksGod

Cc Smart911
Hiyo story ya mtoto aliyerudi n mikono mirefu mpaka magotini tafadhali nyosha mkanda je alikuwa anakula anaongea na alisema alikuwa wapi ?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom