Nadhani kuna dawa ya kichawi ambayo hupewa muhusika kabla ya kuchukuliwa kichawi ..
Kwa Kachanga by the time ilikua hivi. .
Kuna kipindi shangazi yake alikuja kichawi usiku na kumuelekeza huyo binti wakazi ambae tulikua tunaishi nae na alikua analala chumba kimoja na mama Kachanga vitu vya kufanya kwa Kachanga ili shangazi mtu sasa amuwekee dawa ya kuja kumumuua na kumchukua kirahisi mtoto atapotimiza mwezi mmoja kamili. .
Alikuja na kufanikiwa kumuwekea dawa katika kiganja cha mkono wa Kushoto. .( wachawi na washirikina hupenda kuutumia sana mkono wa Kushoto )Na ndiomana hata katika maisha ya kawaida mtu akikupa kitu kwa mkono wa Kushoto inaonekana dizain fulani tofauti. .na hata huko kwenu members muwe makini na kupewa vitu kwa mkono wa Kushoto iwe hela or whatever . ..kataa make mkono wa kushoto una connection kubwa na shetani except kwa wale ambao by nature ni left handed )
Nakumbuka kuna kipindi dogo alikua ananiuliza dada huyu mtoto vidole vikoje? ? Au ni kilema wa vidole? ? Yani muda mwingi anakaa amevifunga vidole. .nikamwambia huyo ni Kachanga wanatakiwa kunyooshwa nyooshwa viungo vilivo vingi kwahiyo hata vidole unakua unamfanya hivi ( namchukua mtoto namnyosha vidole ) unamnyoosha muda huo huo mtoto anavikunja namnyosha hapohapo anakunja. .
Kumbe sababu kubwa ilikua ni ile dawa aliyowekewa na shangazi yake kiganjani anakua kama anaishika .. ulikua ukiangalia mkononi mwa mtoto unaona hakuna kitu chochote ila mtoto anakua anakunja vidole kama ameshika kitu. . Na siku waliyotaka kuja kumchukua mchana mtoto alishinda vibayaa alikua wamotooo kama ana homa. .tulimpa dawa lakini hakuwa vizuri alilia lia sana. . Nakumbuka nilimpigia mama cm kumuelezea kua mtoto anajoto sana mama akaniambia mpeni kwanza panadol muangalie hali ikizidi ndio mumpeleke hospitali....badae jioni kabisa nikakumbuka ndio OMG mchana mzima hatukuenda kanisani ( walikua wametufunga akili ) badae ndio tukaenda wakati mama anaombewa nguvu za madawa yoote zilitoka na mtoto alilia sana wakati mamake anaombewa kule na kureact kama mamake alivokua anafanya kule kanisani wakati madude ya kichawi yanamtoka badae ndo moto ukawaka na chumba kizima kuwa kama kinatetemeka.
Kwahio sisi kikawaida Tungejua amekufa ila kiuhalisia kachukuliwa kichawi kutokana naile dawa kiganjani. ...
Kuna tukio la baba mmoja nilihadithiwaga. Huyo baba mwanae alikufa ila alichukuliwa kiuchawi ..sasa huyo baba alimjua mchawi wake na mtoto alipokufa tu babake akaenda kwa mganga. .mganga akampa dawa ya kupaka ili kuona mizukule mchana
Aliporudi nyumbani baba aliipaka na kwenda sehemu ilipokua maiti ya mwanae akawa anaona mgomba tu. .watu wanaona ni maiti kumbe ni mgomba. . Na hakuweza kumuona mwanae kwakua walikua bado hawajamfanyia madawa yao ya kumfanya mzukule. ( Mtu akiuawa kichawi wachawi hawamchukui siku hio hio au hapohapo mpaka atakapozikwa)Anakua yupo sehemu tu wengine husema eti anakua nyuma ya mlango sijui kuna ukweli gani sasa
Sasa alipoona mgomba alichukua shoka na kwenda ilipokua maiti na kuanza kuikata maiti kama anapasua kuni. .watu wakawa wanaona anaipasua maiti ya mwanae wakawa wanamkataza wengine walikimbia kwa kuogopa pasua maiti pasua maiti. ...badae walishangaa kuona vipande vya mgomba vilivopasuliwa nasio nyama za mtu aliyepasuliwa ...watu walikimbia kila moja na njia yake. ...badae hapohapo msibani huyo baba akamfata mchawi aliyemchukua mwanae na kutaka kumkata naile shoka kwa hasira. .mchawi akakimbia siku ya siku walimuona mtoto karudi
Cc
Smart911
Kwenye huu ulimwengu kuna viumbe vingi vya ajabu tunapishana navyo kila leo. .majini mizukule nk
Sent using
Jamii Forums mobile app