Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Dizain ya kuua ( hii nilisoma sehemu sijui kuna ukweli gani )

1.Kwa kusaini hati ya kifo inakua hivi. .
From nowhere mtu anaweza kukupigia cm au hata kukuuliza tu bila simu kuwa kesho utakuepo?? Wewe Bila kujua unaeza jibu hapana sitakuepo ( labda kama hio kesho una ratiba fulani? Unknowingly Utajibu sitakuepo ..pale unapojibu sitakuepo tu tayari unakua umeshasaini hati ya kifo wewe mwenyewe. .mtu akikuuliza hivo unachotakiwa kujibu ni kuwa : ndio kesho nitakua sehemu fulani ( unaitaja hio sehemu mfano kesho saa fulani nitakua kanisani au nitakua sokoni au kwa fulani ) automatic unakua umevunja na kuharibu huo mpango/kapo cha kifo wakukuua kwani watu wakiokufa ndio hawapo na wenye uhai wapo sehemu mbalimbali

2. Kutumia nyoka ( waliotumwa kichawi lakini )
Wachawi pia hutumia sana nyoka katika kutaka kuua. Inakua hivi. Wanamtuma huyo nyoka ( wakiwa wameshafanya madawa yao ) kwenda kwenye nyumba ambayo muhusika wa kuuawa yupo .
Kama mnavojua nyoka akionekana automatic watu hutaka kumuua hapohapo. So mkimuua huyo nyoka tu mnakua mmemuua huyo mtu alielengwa kuuawa kichawi. Kiuhalisia huyo mtu Anaeza asife hapohapo lakini ipo siku atakufa tu mtake msitake. So wengine husema kuwa ili kuepuka hili kemeeni kwanza pia hutakiwi kumuua huyo nyoka kitu ambacho ni kigumu sana na Sidhani kama Inawezekana kumuona nyoka nyumbani msimuue sijui inakuaje hapo na ukiona unaota manyoka nyoka mara nyingi kunakua na roho ya kishetani /kichawi inakufatilia

3. Kutumia vitu hivo vitu wakishavichukua huenda kuvifanyia dawa huku wakinena na kufanya mambo yao ya kichawi

So sometimes hawa wadudu wadudu pia hutumiwa (hii nilishuhudia kwa dogo) japo nyoka hupendelea kutumia zaidi ndiomana wengine wakiona nyoka na kukemea/ kusali / kuomba gafla huyo nyoka hupotea Saint anne

Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app
Duh hatari

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna kisa kingine
Hiki kimetokea mwaka 2018

Nilienda huko Kijijini..
Kuna kijana alikuwa anasifika kwa uchawi hapo Kijijini..kijana mdogo Kwenye late 20's au early 30's.
Basi wachawi huwa wanajuana wao kwa wao.

Kuna mzee mmoja hapo kijini Ni mganga wa kienyeji,
Huyo mzee kwake kulikuwa na sherehe Kama tambiko hivi,mtoto wake mkubwa wa kiume alikuwa amenunua gari akalipeleka kwa baba yake ambaye ndiyo huyo mganga wa kienyeji ili walizindike wanasema wao kulitambulusha kwa mizimu.

Sasa kawaida ya hizo sherehe,mwenye gari ananunua pombe za kutosha,wazee wa Mila wanakunywa Hadi waridhike ndiyo wanasema mizimu imebariki.

Mara wanaanza kunywa pombe zikawa na dosari,zimechacha zote.
Yule mzee(mganga)akaenda ndani ofisini kwake.. kuangalia Kwenye kioo akamuona huyo kijana yuko pale(niliyesoma pale juu kwamba kijana mdogo mchawi)
Sasa sijui alikuwa ameenda na dawa chache ,,yule mzee aksmzidi nguvu yule kijana.
Akamtungua..

Asubuhi tunasikia msiba unatangazwa,vijijini huko huwa wanapiga ngoma...Mara yule kijana amefariki.
Homa ilimbana usiku ,akaanza kugaragara chini kupelekwa hospital dk akawaambia mbkna hii Ni maiti tayari.

Hiyo siku amekufa,Jana yake alikuja pale nyumbani nilipokuwa,Kuna Kaka alikuwa anaishi pale alikuja kumuulizia,
Alivyonikuta hakunisemesha kitu nilikuwa nimetoka kusali,sijui kwanini alinipita hata salamu hakunipa,akaondoka

Basi msiba ukapita,kijana akawa ameenda.
Mara usiku wanamuona kwake anazunguka nje.
Mke wake alisema kwamba alikuwa anamgongea usiku.
Aliwatokea marafiki zake..
Nikawa namtania yule kijana wa pale nyumbani kwamba wewe hajakutokea!?
Maana ile siku anakufa mchana alikuja hapa,akasema hapana..ila nimemuota usiku.

Basi haukupita mwezi,mtoto wa yule mzee mganga aliyepeleka Lile gari nyumbani kwao ,,(alikuwa mwanajeshi) akafariki.
Yaani hakuugua chochote alikufa ghafla.

Yule mzee alilia,akasema Bora wangemchukua huyu mdogo.
Alilia Sana yule mzee.

Kuna kiss kingine Cha huyo mzee na mjukuu wake(yaani mtoto wa huyo mtoto wake mwanajeshi)
Nimechoka kuandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
Hilo zee jinga kweli eti bora angekufa mdogo[emoji1][emoji1][emoji1]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nililia msiba wa mzee miezi 7 au 8 before ajafariki ghafla, ilikua mara kwa Mara naota amekufa, tumezika na tumekaa vikao vya familia kujua hatima yetu maana tulikua wadogo, nilikua nalia ndotoni Nikiamka Nna machozi kabisa, ila Nikiamka baba yuko mzima kabisa nilikua sielewi naona Ndoto tu... Ilikua haipiti wiki mbili mfululizo. Now ndio naelewa.
Ni mengi, naweza nika predict kitu kwa usahihi kabisa. Naweza kuona mazingira nitakayofanya kazi hata mwakani ndotoni au kwa hisia
mkuu tunafanana sana:
Mimi mwaka 2010 wakati npo chuo cha cbe dar mzee wangu alikua anaumwa amelazwa muimbili hospital.

Ilikua Mara kwa Mara haipiti wiki lazima nimuote mzee wangu amefariki,basi nlikua nalia sana tena sana ukumbuke nipo ndotoni nikistuka najikuta ninamachozi mengi sana.
Basi nikiamka tu lazima niende hospital kuakikisha je amekufa kwel au laa lkn nlikua namkuta mzima.

siku namaliza tu mitihan ya mwisho ndo siku hiyo hiyo amefariki hakika nililia sana tena sana.

KUHUSU MAONO NDOTONI
Mimi Nina staili mbili za kuota nikiwa nimelala.
Huwa naota kwa kuona tukio kamili lkn pia huwa naota kwa kusikia sauti ya mtu masikioni mwangu akiniambia kitu.
Kuna siku niliota sauti ya mtu ikiwa IPO siriazi inaniambia kwa umakini kabisa kua utaenda kua manager katika kampuni hii theni nikaanza kuoneshwa laivu mazingira ya hiyo kampuni.
Nilivostuka niliomba mungu iyo ndoto na iwe kwel maana nilikua kweli sina kazi ya kuajiriwa naendesha bodaboda yangu.
Ikapita kama miezi mitatu mbaka nishaanza kusahau hiyo ndoto siku moja natoka kwenye interview ya kampuni flani dar wakat nipo chalinze baba yangu mdogo akanipigia simu akaniambia upo tayar kuajiriwa nikamwambia ndio mzee akaniambia nitumie CV yako kuna MTU nimtumie

Nlivotuma baada ya wiki nikaitwa kusailiwa nikaambiwa wiki ijayo niende kuanza kazi tanga.
Huwezi amini nilivofika mazingira ya pale kwenye ile kampuni ndo yaleyale ambayo niliyoyaota nankuoneshwa kwenye ndoto ambayo ilitokea zaidi ya miezi mitatu nyuma

Nilishangaa sana kwa kwel.na mengine mengi tu sitaki kuwachosha na wengine wachangie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom