Kama umewahi kushuhudia live nguvu za giza pita hapa uweke ushuhuda wako

Wakuu habari zenu, ni matumaini yangu kuwa hamjambo.

Leo nataka kuweka ushuhuda wangu kwa niliyoyashuhudia live juu ya nguvu za giza, kwa wasioamini nadhani uzi huu hautakuwa na thamani kwao, kama na wewe unao ushuhuda usisahau kushea nasi.

1. Ushuhuda wangu unaanzia mwaka 1992 nikiwa nafundisha shule X wilaya ya Sengerema, kuna mwalimu nilikuwa nafundisha naye kituo kimoja.

Siku hiyo kuna kamvua kalinyesha sana, baada ya kupungua mwalimu mwenzangu alimuagiza mtoto wake wa kiume aliyekuwa akisoma darasa la kwanza kwenda kuchuma maharage shambani.

Bahati mbaya mtoto akiwa shambani aligongwa/aliumwa na nyoka na kupeleka kifo, tulifanya taratibu za mazishi na kumsitiri mtoto huyo.

Cha kushangaza mwaka 2008 mtoto huyo alionekana akiwa uchi na nywele ndefu sana alikuja moja kwa moja nyumbani na kupitiliza ndani nyumbani kwao, alikuwa ameshakuwa baba mzima, nywele zilikuwa ndefu sana pamoja na mikono iliyofikia usawa wa magoti.

Watu walistaajabu sana lakini hakudumu sana alifariki baada ya kukaa uraiani kwa wiki mbili.

2. Ushuhuda wangu bado unabaki huko huko Sengerema katika kijiji cha Bubandwamhela.

Nikiwa nafundisha shule X, kuna binti kijijini aliyekuwa akisoma darasa la saba aliugua ghafla baada ya kutoka shuleni.

Wazazi wake walipompeleka hospitali daktari aliwaambia mtoto hana ugonjwa, wazazi waliamua kujiongeza na kumpeleka kwa mganga wa jadi.

Cha kushangaza kesho yake shangazi ya binti alikutwa kwa mganga akiwa uchi, huku akiweweseka na akili zimemruka, shangazi mtu alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini kwa kuwa serikali haiamini ushirikina aliachiwa huru, lakini hadi leo hii alishakuwa chizi. Binti yeye alipona kabisa.

3. Kisa cha tatu na mwisho ni hiki kilichotokea Liwale shule ya sekondari X nikiwa na walimu wenzangu ambao tulikuwa tunasoma chuo cha SAUT-Mtwara.

Tulipangiwa field katika wilaya ya Liwale ilikuwa mwaka 2009, mwanachuo mwenzetu akiwa zamu siku hiyo alikumbana na mtoto ambaye kwao iliaminika kuwa bibi yake alikuwa mtaalamu wa mambo ya giza.

Mwanafunzi huyo alichelewa kufika shule, mwalimu alipotaka kumuadhibu aligoma, wakasumbuana sana mwisho wa siku akamuadhibu yakaisha, jioni tukiwa uwanjani tunafanya mazoezi yule mwanachuo mwenzangu alianguka na kupoteza fahamu, ikawa jumla hadi kifo.

Kama na wewe umewahi kukutana/kushuhudia live ushirikina share nasi kisa chako watu tupate ilimu.

Mungu ni mwema siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi nimemuona Lisu anachangisha michango gari liwekwe makumbusho na alikua ulaya kwa wafadhili wake kitambo kidogo tu
 
wanasema mwezi wa Ramadhani wachawi na majini huwa wanafungiwa ama kuwa likizo.

kisa cha kwanza ni mwezi huo huo wa Ramadhani, tulikuwa kijijini, kwa sasa ni mji, Morogoro wilaya ya Mvomero kwa sasa, ilikuwa ni kipindi cha likizo, Brother ameenda chooni, kujisaidia haja kubwa, choo hakikuwa na umeme akawa anatumia mwanga unaotokana na mbalamwezi, lakini baada ya kukata gogo, kabla hajachukua kopo, akasikia anatawazwa, yaan ghafla tu anasikia mkono pyaa umepita unamchambisha, Brother alitoka na mlango.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
2010 nipo ndani ya fuso, natokea Ifakara kwenda dsm. Kufika Maseyu mida kama saa 8 usiku dereva akapaki, akasema amechoka anapumzika kidogo. Akatuambia saa 10 tumwamshe tuanze safari.

Sijui kama ni uchawi au ni nini, tulipitiwa na usingizi mzito, na wote, tulikuwa watatu tuliota ndoto ya aina moja. TUNAPIGA MECHI. tumejipiga mabao wote, kuangali saa ni dk 20 tu zimepita. Nilichowaeleza wenzangu ndio walichoota. Mwanamke niloyeota namgonga ndio huyo huyo wenzangu walikuwa wakiota wanamgona.

Niliota vipele vya baridi kwa uoga. Tukaondoka kuendelea na safari. Tangu siku hiyo sipandi tena malori ya mzigo yanayosafiri usiku.

Sent from my SM-G570F using Tapatalk
vipi mashine ilikuwa tight ya huyo jini.
 
Amina best mwanzo nilikua naogopa sana ila sasa nina ujasiri siogopi chochote kwani mungu yu pamoja nasi. .mpaka wakati huu ni kwa upendo wake tu .
Pia kingine baba mtoto nae ( shemeji) anasali sana kuombea familia yake Kwani hataki michanganyo ya waganga mara kanisani. .kuna kipindi dogo alikata tamaa akataka kwenda kwa waganga mumewe akamwambia akikanyaga kwa waganga tu wamewapa nafasi maadui ... anasisitiza wasali sana . ..sasa huyo kijana anataka amchukue mkewe ndo balaa lililopo kwasasa je kama ndugu yenu mtafanyeje ? ? Ukoo hauelewi cha ndoa wala nini. ..mtatuulia mwanetu. . Huyo mtoto tutalea vizuri tu binti yetu Harudi ng'o ..
Ukweni wanataka mjukuu wao akakae kwao kwa bibiyao mzaa baba ambao wajukuu wengine wote wapo huko eti damu yao haiendi mbali. Mpaka mtoto alelewe kwao .baba mtoto hataki mtoto akakae kwao anaenda kinyume na wakwao. . Kama ndugu yenu mngefanyeje? ?

Cc Smart911

Sent using Jamii Forums mobile app

Mara ya kwanza nlidhani upo serious. Ulipoandika Troobaaaa nikaona kumbe una fanya masikhara. Mtu mwenye uelewa na akili nzuri hawezi andika upuuzi kama huo. Ungeandika kwa lugha ya u serious na kuonesha unajielewa.
 
Nyingine Sumbawanga wakati wa Ujenzi wa shule za kata ile wananchi kuchangia nguvu kazi, mzee mmoja alikuwa haendi wala nini... Afisa Mtendaji wa kata akampa adhabu kuwa hadi kesho yake asubuhi wakute kasomba tanuru mbili za tofali na kusogeza site, vinginevyo atapelekwa polisi. Mzee akasema sawa nitafanya usiku.

Asubuhi wanaamka, tanuru halipo, ila Kijiji chote, wazee, watoto, watumishi kanisani hadi Mtendaji kata wapo hoi, wamechafuka umbi la tofali. Mzee hakuguswa tena na kazi za jamii...

Hii Chai tumesimuliana sana toka miaka ya nyuma.
 
Wakuu habari zenu, ni matumaini yangu kuwa hamjambo.

Leo nataka kuweka ushuhuda wangu kwa niliyoyashuhudia live juu ya nguvu za giza, kwa wasioamini nadhani uzi huu hautakuwa na thamani kwao, kama na wewe unao ushuhuda usisahau kushea nasi.

1. Ushuhuda wangu unaanzia mwaka 1992 nikiwa nafundisha shule X wilaya ya Sengerema, kuna mwalimu nilikuwa nafundisha naye kituo kimoja.

Siku hiyo kuna kamvua kalinyesha sana, baada ya kupungua mwalimu mwenzangu alimuagiza mtoto wake wa kiume aliyekuwa akisoma darasa la kwanza kwenda kuchuma maharage shambani.

Bahati mbaya mtoto akiwa shambani aligongwa/aliumwa na nyoka na kupeleka kifo, tulifanya taratibu za mazishi na kumsitiri mtoto huyo.

Cha kushangaza mwaka 2008 mtoto huyo alionekana akiwa uchi na nywele ndefu sana alikuja moja kwa moja nyumbani na kupitiliza ndani nyumbani kwao, alikuwa ameshakuwa baba mzima, nywele zilikuwa ndefu sana pamoja na mikono iliyofikia usawa wa magoti.

Watu walistaajabu sana lakini hakudumu sana alifariki baada ya kukaa uraiani kwa wiki mbili.

2. Ushuhuda wangu bado unabaki huko huko Sengerema katika kijiji cha Bubandwamhela.

Nikiwa nafundisha shule X, kuna binti kijijini aliyekuwa akisoma darasa la saba aliugua ghafla baada ya kutoka shuleni.

Wazazi wake walipompeleka hospitali daktari aliwaambia mtoto hana ugonjwa, wazazi waliamua kujiongeza na kumpeleka kwa mganga wa jadi.

Cha kushangaza kesho yake shangazi ya binti alikutwa kwa mganga akiwa uchi, huku akiweweseka na akili zimemruka, shangazi mtu alikamatwa na kupelekwa kituo cha polisi lakini kwa kuwa serikali haiamini ushirikina aliachiwa huru, lakini hadi leo hii alishakuwa chizi. Binti yeye alipona kabisa.

3. Kisa cha tatu na mwisho ni hiki kilichotokea Liwale shule ya sekondari X nikiwa na walimu wenzangu ambao tulikuwa tunasoma chuo cha SAUT-Mtwara.

Tulipangiwa field katika wilaya ya Liwale ilikuwa mwaka 2009, mwanachuo mwenzetu akiwa zamu siku hiyo alikumbana na mtoto ambaye kwao iliaminika kuwa bibi yake alikuwa mtaalamu wa mambo ya giza.

Mwanafunzi huyo alichelewa kufika shule, mwalimu alipotaka kumuadhibu aligoma, wakasumbuana sana mwisho wa siku akamuadhibu yakaisha, jioni tukiwa uwanjani tunafanya mazoezi yule mwanachuo mwenzangu alianguka na kupoteza fahamu, ikawa jumla hadi kifo.

Kama na wewe umewahi kukutana/kushuhudia live ushirikina share nasi kisa chako watu tupate ilimu.

Mungu ni mwema siku zote.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwana mi nilikua sjjawahi kuloga.
Hapo nimesota sana mtaani nikapata kazi wiki 2 huku wife kanizingua.
Ingia mzigoni nikakata bia 2 hizi draft.
Kumbe pale ndani kuna mzee ananichora tu.
Badae ananiita nikaomba msamaha pale yakaisha maana tulikua wawili tu.
Boss alikua Canada huko alivyorudi kapewa taarifa.
Kuna jamaa huko ofisini kaja kunishtua "e bana kaa tayari"
Kunani tena?
Ulikutwa unakula bia.
Ikawa ile kesi ilifika huko?
Ikawa ipo.
Dah nikatoka kinyonge sana.
Nimekutana na mwanangu mmoja namsimulia kasema kesi ndogo twende kwa mtaalamu.
Dah tulipiga duah ,sijui nini,kisomo siku nzima.
Nikapewa maji yalichanganywa na damu ya njiwa.
Nikaambiwa mwaga pale anaäpita kwenda ofisini.
Yule mzee alikutana na matukio
Mpk kaachishwa kazi.
Yule mtaalamu alikataa malipo
Kabisa.
 
wanasema mwezi wa Ramadhani wachawi na majini huwa wanafungiwa ama kuwa likizo.

kisa cha kwanza ni mwezi huo huo wa Ramadhani, tulikuwa kijijini, kwa sasa ni mji, Morogoro wilaya ya Mvomero kwa sasa, ilikuwa ni kipindi cha likizo, Brother ameenda chooni, kujisaidia haja kubwa, choo hakikuwa na umeme akawa anatumia mwanga unaotokana na mbalamwezi, lakini baada ya kukata gogo, kabla hajachukua kopo, akasikia anatawazwa, yaan ghafla tu anasikia mkono pyaa umepita unamchambisha, Brother alitoka na mlango.
Masikini wee kaguswa kinyeo
 
Sio nyoka alikuwa anataka kuingia kwenye tundu la tako?
 
Siku flani za Mwezi Nov mwaka wa 2023 ilikuwa siku ya kushangaza kwelikweli. Kwa umri wangu wa 27 kipindi hicho sikuwahi Kuona miujiza yoyote yenye chembechembe za uchawi na ushirikina. Sikuwa home Kwa miaka kadhaa hivyo siku hizi nilikuwa nimewatokea kuwacheki hali zao.
Njia ya kuelekea home huwa Kuna miti mikubwa minne iitwayo MIKUYU. Hii miti bwana husemwa na wanakijiji kama miti yenye kuwa makazi ya majini. Na stori hizi nikizisikia toka utotoni.
Sasa basi siku hiyo naelekea home mida ya saa 1:30 hivi usiku nilipofika karibu na miti ile ghafla kulitokea upepo jirani na nilipokuwa nilipocheki ghafla nikaona kiumbe flani nguo nyeusi mfano wa mtu kinakimbia Kwa Kasi kubwa bila kugusa chini Kwa umbali wa karibu MITA 70 hivi then kikapotea. Ghafla nikahisi kichwa kinavimba na nywele zinacheza.
Nikakimbia kuelekea home Kwa mbio ndefu. Nilipofika home nikamwambia Maza. Maza alishtuka sana akisema eneo Lile limepoteza watu wawili mpaka Leo Kwa kifo kwani yasemekana walikumbana na majini. Dah hofu nami ikanshika nisije kuwa watatu.
Bahati nzuri mpaka Leo Nipo.
 
Back
Top Bottom