Maisha yana safari ndefu sana usipofunga mkanda haswa unaweza zeekea nyumbani hasa kwa sisi tuliotoka kwenye familia masikini.
Nakumbuka wakati nimepata ajira kampuni Fulani ujira ulikuwa mdogo sana licha ya elimu niliyo nayo ilinibidi nifanye hivyo hivyo mshahara ulikuwa 200k kwa mwezi.
Kipindi hicho bado nipo home, nyumbani kila kitu nilikuwa napata licha ya kupata kila nitakacho sikuridhika kukaa pale maana niliona nampa mzigo mkubwa mzazi wangu Mama baba alisha tangulia mbele za haki ( RIP)
Nikamwambia bi mkubwa mimi nataka nikajitegemee, akagoma akasena wewe bado sana kwanza tu kazi umeanza juzi hakuna kwenda kokote.
Baadae nilifanya maamuzi ya kuondoka nyumbani kwa nguvu japo bi mkubwa hakunipa baraka maana hakukubaliana na hatua niliyochukua.
Maisha ya kigheto gheto yakaanza bi mkubwa hakuta kuja hata kujua ninapo ishi 🤣🤣🤣 kasusa.
Aiseeh, nilikuwa najimeki siyo masihara ndani ya muda mfupi gheto likapendeza, Mungu siyo Athumani nikapata kazi sehemu nyingine kidogo masilahi mazuri mambo yakanoga, sasa Nina mke na mtoto mmoja, 🤣🤣🤣 sasaivi bi mkubwa anakuja home anacheza tu na mjuu wake asusi tena 🤣🤣🤣
View attachment 2126023