Kama umewahi kutumia hivi vitu, wewe ni legend

Kama umewahi kutumia hivi vitu, wewe ni legend

Kuna raba flani za plastiki,ukivaa kuanzia saa 6 mchana,zinalainika na jua linachoma sana miguu...

Zilikua maarufu kwa jina la UTANIKOMA SAA NANE..
😂😂
 
Kama umewahi kusoma gazeti liitwalo Mfanyakazi basi inabidi uwe kwako!

Kama uliwahi kuwaona O-level students wa Tambaza hama kwenu haraka.

Kama Uliwahi kusikia shule ya sekondari Forodhani hupaswi kuendelea kumtegemea babako.

Kama uliwahi kunywa juice ya sun vita basi wewe mkongwe.

Kama uliwahi kuhadithiwa kuwa Nyerere aliwahi kupigwa mtama na bodyguard wake basi unapaswa uwe na wajukuu...
😂😂Hii ya Nyerere sijawah kuisikia
 
Vyombo vya usafiri

1. DCM (Japo siku hizi bado chache zipo)
2. Mabasi ya Leyland
3. Chai maharage hii mnakaa mnatazamana Kama mnacheza draft
4. Peugeot
5. Datsun N.k
Nb: zilikua ndio luxury pindi hizo, nyingine ongeza.

Vyakula
1. Sambusa za ubwabwa ( shuleni)
2. Kachori za chachandu ya machicha ya Nazi
3. Koni za kwenye vikopo vya bati
Nyingine mtaongeza wadau.

Vinywaji
1. Juice ya kutengenezwa kutokana na unga wa kwenye vipakti, siku hz zipo jusi cola lakini hz zilikua noma pakti moja inatolewa ndoo mbili au tatu afu zinawekwa barafu...kumbuka hyo ni sikukuu wakubwa wanapiga soda watoto mnaishi na hzo ndude af mna enjoy sana.
2. Kuna soda flani ilikua ya njano inatengenezwa na kampuni ya coca nadhani jina nimeisahau
3. Chai ya chai jaba Nk.

Mavazi and accessories
1. Suruali za kodrai zikipigwa jua zinawakawaka Kama gold ya geita, sikuuu mnaeza jikuta mtaa mzima mmevaa Aina moja.
2. Magauni ya spesheli.
3. Njumu flani za mpira Kuna wajomba wameenda nazo Hadi shule zipo kama raba flani
4. Mifuko ya sports
5. Viroba vya unga kufanywa mfuko wa kubebea daftari

N.k
Matusi na matukano hasa ya wazazi
1. Nyau kasoro mkia ww
2. Nyambafu
3. Macho kumchuzi ww
4. Shenzi type

Ongezeeni na ya kwenu maana nimekumbuka nimecheka sana

Kuna shoes ziliitwa FILA, nyingine TAHIMA, pia kuna tracksuit ziliitwa OPEL[emoji91][emoji91][emoji91][emoji91]
 
Kama umewahi kuvaa chupi za VIP wewe ni legendary. Hapo kwenye Machicha ya nazi dah, umenikumbusha mbali sana. Pia kulikuwa na Michele unaitwa "Pepeta" dah
 
Kuna Land Rover zilikua hazina automatic ignition zinaingizwa chuma kama bpedal ya baiskeli kwenye fan ya rejeta inazungusha kwa nguvu ndio ziwake ...ukiwa mzembe zinaeza vunja mkono... Kama kick ya Honda 110 ilikua na tabia hiyo nayo
Chuma kilikuwa kinaitwa Hendeli (nadhani kutokana na neno la kiingereza handle)
 
Kuna raba flani za plastiki,ukivaa kuanzia saa 6 mchana,zinalainika na jua linachoma sana miguu...

Zilikua maarufu kwa jina la UTANIKOMA SAA NANE..
Kuna raba flani za plastiki,ukivaa kuanzia saa 6 mchana,zinalainika na jua linachoma sana miguu...

Zilikua maarufu kwa jina la UTANIKOMA SAA NANE..
Ziliitwa chachacha🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3] hiyo unayosema nishaijua
Hata mm nilikuwa naziogopa kupanda kwenye kona nahisi ni kama zigapindukq
Km wewe legend wa kkoo hiyo ISUZU ilipaki ilikuwa pale mtaa TANDAMTI karibu na msikiti wa idrisa pembezoni mwa OFISI YA STAR TIME miaka ya 2013 lilikuwa bovu lilikaa pale karibu miaka 3 au miwili hivi
Sema zile hazikuwa JOURNEY
zile nhisi zilikuwa modified kama unavyoona hizi TX hapa BODI ya kuchongaView attachment 2519106
Kichwa ng'ombe ziliitwa
 
Kwenye kuchagua shule primary Mtihani starndard 7
Edhi hizo masomo matatu MAARIFA YA JAMII LUGHA na HESABU
Unachagua shule tatu uzipendazo
Forodhani chaguo la kwanza
Kibasira chaguo la pili
Kambangwa kipindi hicho ndo inaanza nikaiweka ya tatu

Asikwambie mtu edhi zetu DAR ES SALAAM nzima shure za SECONDARY ZA hazikuzidi 8
Na wanafunzi tulikuwa wengi balaa
kama kuna mtu humu kasoma JAMUHURI ya edhi hizo nakusalimu sana LEGEND mana ilikuwa shule ya MALEGEND wanasona lkn hawana uhakika kama watafanya paper ya TAIFA ya FORM 4 malegend wa edhi hizo watanielewa

Forodhani ni shule waliosoma BRO zangu nikawa naipenda sana hiyo SHULE
Kwanini unasema EDHI AU NDO TUNAKUMBUSHIA UTOTONI.
 
Back
Top Bottom