Stress za kawaida unaweza kuzikandamiza kwa kusikiliza muziki, kucheki series, n.k. lakini stress nzito ni ishu nyingine
Wengi kimbilio la kupunguza stress huwa ni pombe, nyapu, bangi, madawa, n.k. na mwishowe tunapata tatizo la ziada "addiction"
kama umeweza kudeal na stress bila kilevi weka hapa mbinu
nilishawahi kupitia kipindi kigumu sana maishani mwangu, chenye stress hadi nilikuwa naongea peke yangu, wengi walijua nataka kuchanganyikiwa. shida nyingi kila kona na unachekwa hakuna wa kukusaidia. hii ilikuwa kati ya 2007 hadi 2011. Niliamua kumgeukia Mungu, hapo ndipo nilipoamini Neno la Mungu linavyosema kwamba Yesu Kristo ni mfalme wa amani, nilipata amani ya ajabu, isiyoelezeka, amani yenye furaha, amani isiyo ya kipimo hata kueleza hapa siwezi, ataiujua tu yule atakayeipata.
amani ambayo hata kama nilikuwa sina pesa, nilikua na amani na ninabubujiko la Mungu moyoni, kumbe baada ya kugeukia kwa Mungu kwa kuokoka kwa kweli ndipo Mungu akaanza kunitengeneza polepole, kunipa fadhila polepole, hadi nikasimama, nikajijenga, nimebaki tu namtukuza Mungu maishani.
hiyo ni amani ambayo ulimwengu huu hauwezi kuitoa. pome haiwezi kutoa amani kama ile, pesa haziwezi kutoa amani kama ile, mwanamke hawezi kukupa amani kama ile, nayo ndiyo ninayoipambania mara kwa mara, ikipotea huwa namtafuta Mungu hadi inarudi.
YOHANA 14:27 INASEMA: Amani nawaachieni; amani yangu nawapa; niwapavyo mimi sivyo kama ulimwengu utoavyo. Msifadhaike mioyoni mwenu, wala msiwe na woga
ISAYA 9:6 INASEMA;
Maana kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, Tumepewa mtoto mwanamume;
Na uweza wa kifalme utakuwa begani mwake; Naye ataitwa jina lake,
Mshauri wa ajabu, Mungu mwenye nguvu, Baba wa milele, Mfalme wa amani.
USHAURI; ukipita kipindi kigumu, chenye stress na depression, labda kwasababu ya uhaba wa kipato, magonjwa, ugomvi mbalimbali, kuachwa au chochote, TAFUTA AMANI KWA YESU. mpe Yesu maisha yako kwa kuokoka na ujiunge na waliookoka kama wewe. usikatishwe tamaa na wale wanaosema wameokoka ila wanatenda dhambi, hayo ni madhaifu ya dunia, ambatana na wenye nia moja na wewe. Yesu atakupa amani ya kweli. usitafute amani kwa waganga, pombe au wanawake, utapotea mazima. na ukienda kwa Yesu, hatakutupa nje kamwe.
Yohana 6:35 - 37 inasema: Yesu akawaambia, Mimi ndimi chakula cha uzima; yeye ajaye kwangu hataona njaa kabisa, naye aniaminiye hataona kiu kamwe. 36 Lakini naliwaambia ya kwamba mmeniona wala hamwamini. 37 Wote anipao Baba watakuja kwangu;
wala ye yote ajaye kwangu sitamtupa nje kamwe.