Yaani mwanaume huwezi kusonga mbele kimaisha kama huna mwanamke wa kudumu.
Wazungu walisema, kila mwanaume mwenyeafanikio, nyuma yake kuna mwanamke.
Ukiwa na mke unakuwa na utulivu wa kiakili na kuweza kupambana vizuri.
Pia, ukiwa na mwanamke pasua kichwa inakuwa kinyume.
Kimsingi, mwanamke anampa mwanaume hamasa sana.
Kumbuka katika jamii, mwanaume aliyeoa anaaminika zaidi kuliko asiyeoa.
Zamani ili uwe kiongozi, ilimpasa mwanaume awe ameoa.
Usipokuwa na mke maana yake huna maisha ya kudumu yenye msimamo yaani ni muhuni tu.