Your genius man❌Daaah your genius man mkuu solute kwako..
Umeongea kitu ambacho very important aiseeee 😂
Nenda kwa matembezi pako poa.Kama Mimi Yani sijawah kufika lakini nmetokea kupaona sio sehemu salama, na mtoa mada amathibitisha Hilo kwa hiyo ya kutokaa kwenye daladala SITI ya mbele
Your genius ❌ you are genius ✅Daaah your genius man mkuu solute kwako..
Umeongea kitu ambacho very important aiseeee 😂
Nipe experince ya durban nitakuwa huko kwa miaka kama minne hv nafanya kazi professional na ni mmenda K kwa asiliHabari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.
Nianze kwa kusema kuwa dunia ina mengi, na kamwe hauwezi kuyajua kama haujaambiwa au kuyaona. Ndio maana waswahili wanamsemo wao unaosema "tembea uyaone". Hii haimaanishi kwamba utembee uyaone magorofa, magari au barabara, bali uone mambo mapya ambayo hapo kabla ya kutembea ulikuwa haujawahi kuyaona au kuyasikia popote.
Sasa leo ningependa nije na mada inayowatahadharisha ndugu zangu wabongo, ili kuwafungua macho na akili ya kujua yale ambayo hapo kabla walikuwa hawajayajua kuhusu South Africa, Dzonga, Afrika borwa, Afrika kusini, bondeni, Kaburu na kila jina linalotambulisha taifa hili.
Ni mambo sita tu ambayo ningependa kukutahadharisha nayo, uyazingatie kabla ya safari. Ila kama kuna mengine ya kuongezea basi wenzangu ambao wako humu pia wataongezea mengine katika comment. Na uzi wangu wa leo unajikita katika mambo yaliopo ndani ya mipaka ya South tu. Kuhusu changamoto zingine za njiani kabla ya kufika South nk, hizo sintozizungumzia kwa sasa. Maana thread za changamoto hizo zipo nyingi na mimi nishawahi kuandika moja.
Tuendelee hapo chini na yale unayotakiwa kuzingatia.
1. Hakikisha una document zote muhimu zinazohitajika safarini. Na kama uliambiwa kuwa gharama ya safari ni laki tatu, basi uandae angalau laki nne, ili moja uiweke pembeni itakusadia mbele ya safari. Kumbuka kuna dharura njiani, dola au rand kupanda nk.
2. Wakati unapanga safari, jitahidi kwanza ujue kingereza. Na kama una kichwa kizito cha kujifunza ngeli, basi upambane ujue hata salam, kuomba kitu au kuaga. South ni nchi inayoongea lugha 11. Ambapo lugha 9 ni za wenyeji na 2 za wazungu. Lakini lugha ya taifa na ambayo inapewa kipaumbele zaidi ni English.
Sasa ukijua English, hata kama hauna elimu ya maaana, uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa ukilinganisha na wale ambao hawajui English. Ndomaana wazimbabwe wamedhibiti kazi nyingi na haswa zinazomilikiwa na wazungu, maana wao English kwao ni kama maji na mtungi, halafu wanaongea British safi kuliko waafrika wengine. Kutokujua English kumewanyima watu wengi (haswa kutoka bongo) fursa za kazi, hivyo kusababisha wengine kuamua kufanya deal hatari, halali na zisizo halali ili mradi mtu aishi.
3. Kabla ya kuanza safari hakikisha una address au contacts za wenyeji wako zaidi ya mmoja. Nchi hii kuna watu wengi wameuwawa, wameibiwa, wamekamatwa na kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kukimbiwa au kuzimiwa simu na wenyeji wao kabla ya kuingia au baada ya kuingia South. Na hii sio kwa wabongo tu, bali ni nchi zote za East Africa watu wana tabia za kuwaingiza maboya ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba waje tu watawapokea na kuwafanyia mpango wa kuishi, lakini ndugu, jamaa au marafiki hao wanapoingia tu mwenyeji huzima simu, hubadili namba nk. Hivyo ukiwa na address au namba za sim zaidi ya 3, itakusaidia ku deal na mwingine baada ya mmoja au wawili wa mwanzo kukuzimia simu.
4. Usiwaze kwamba utafanya kazi fulani tu, bali wewe ujiandae kufanya kazi yoyote (ya halali) kujiingizia kipato. Hili swala la watu kuja huku wakiandaa akili, na saikolojia zao za kichwa kwamba anakuja kufanya kazi fulani tu. Ndio limesababisha baadhi ya wabongo kupoteza mwelekeo wa maisha, na kujikuta wanajitupa katika biashara hatari na zisizokuwa halali.
5. Usilete usela mavi usiokuwa na maana. Vijana wengi waliotaka kuleta usela wa Mbagala, Mburahati, Manzese, Temeke, Tandika nk tumewazika wakiwa bado wadogo. Hii ni kwa sababu huku watu hawana muda wa kukimbizana na mwizi wajichoshe. Ukileta usela mavi, watu wanakutafutia target, wanafumua ubongo, kazi imekwisha. yumbani watu wanarudisha nguo au maiti na kesi hamna. Pia usije kwa lengo la kutafuta na kufanya starehe kupitiliza mpaka ukasahau kilichokuleta. Maana kama starehe hata bongo zipo na umeziacha, kama mademu bongo wapo na umewaacha, kama tungi pia bongo lipo umeliacha. So focus kwa kile kilichokufanya utafute nauli uje. Sio kuendekeza kulewa na chupi za Kaburu utapotea mazima na hakuna mtu atakaekurudisha katika chanel yako tena.
6. Ukifika hapa kama wewe ni mpya usikimbilie kukaa kiti cha mbele katika daladala (tax), hata kama imejaa na imebaki siti moja ya mbele, ni bora usubiri nyingine alafu ndio upande. Hii ni kwa sababu huku majimbo mengi daladala zao hakuna kondakta anaezunguka ndani ya daladala kuomba nauli. So ukisema unakimbilia mbele kukaa na dereva, utashangaa watu wanakusanya hela zote huko nyuma, alaf wanakutupia wewe ndio uhesabu na kama kuna mtu ametoa hela kubwa umrudishie chenji, na ikiwa pungufu uhakikishe waliokupa wanazieneza. Dereva yeye hupokea nauli ambayo imeshahesabiwa tayari na iwe imetimia. Ikipungua hata sh hamsini basi ataanza na wewe uliepokea hela kabla ya kuendelea na waliopo ndani ya gari. Pia asilimia kubwa ya madereva wa hapa wana silaha mbali mbali ndani ya gari zao, kama sio bunduki basi fimbo inayofanana na mkia wa taa. So hela yake isipoenea na wewe ndo New comer (mpya) haujui lugha, basi imekula kwako. Hata ujitetee kwa English yako ya kuunga unga hatokuelewa. Naomba niishie hapa.
Umeanza kuniponda kwanza 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂Your genius man❌
You’re genius man, or you'r✔️
Mzee wa mishangazi, kule sasa ndio kuna mishangazi yenye nyama na roho nzuri.
Sipangiwi cha kuandika..Your genius ❌ you are genius ✅
Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.

Kwa hakika Mungu alikuwa upande wako mkuu, inatakiwa amshukuru kila siku ya maisha yako.Mungu mwema nilifika cape saa kumi jioni kesho saa Moja asubuhi nikaanza kazi JM mall customer assistant na kiingereza sijui wazungu walikuwa wanarudia nachowaambia mf go zea ' utasikia aah go zea !? In turn ikawa ndio lucky point kwangu ikawa kama nembo yangu
Ulikuwa na bahati sana mkuu.Nilikuwa na host kabisa na hakuwa msela ni mtu na familia nilishikwa mkono hadi kazini na jamaa alikuwa tayari ameshajenga mazingira hata makaratasi sikuombwa
Unajua kinachofanya washike mapema hizo lugha, ni kwa sababu hizi lugha za kibantu zinaingiliana sana. Japo kiswahili nacho kimechomekewa kibantu ndani yake lakin bado kinajitegemea kwa kiasi fulani. Ukikisikia kiyao cha mangochi nchini Malawi kina asilimia 98 ya kiyao cha tunduru mkoani Ruvuma nchini Tanzania.Kuzishika hizo lugha lazima uwe hujui kiingereza wala kiswahili. Waburundi ndo huwa ni ma-master wa kujua lugha za watu. Wenyewe wanasema french ni lugha ya kimaskini.
Hawa washenzi wapumbavu sana.Asante kwa ushauri.
Ila tangu waanze ubaguzi wao kwa waafrika wenzao, watu wengi wamewatoa maana. Wanawaona ni wajinga tu. Hamna mtu mwenye hamu ya kwenda huko
Ya hovyo kivipi mkuu? Fafanua!South ni nchi ya hovyo sema tu basi yani
Ni kweli mkuu. Hata watu wa Tunduma, Mbeya na Rukwa huwa wepesi sana kujua lugha za Zambia.Unajua kinachofanya washike mapema hizo lugha, ni kwa sababu hizi lugha za kibantu zinaingiliana sana. Japo kiswahili nacho kimechomekewa kibantu ndani yake lakin bado kinajitegemea kwa kiasi fulani. Ukikisikia kiyao cha mangochi nchini Malawi kina asilimia 98 ya kiyao cha tunduru mkoani Ruvuma nchini Tanzania.
Huyu ni wale ambao wanasimuliwa na kujifanya wanajua kile walichosimuliwa. Wengine tushafanya kazi hadi katika maeneo ambayo mtu akihadisiwa anajiuliza uliwezaje wezaje kuipata kazi hiyo.Mtu kama hujafika sehemu utaona kama miujiza baadhi ya mambo. Huyo jomba ni wale wanaosoma sheria za nchi hiyo mitandaoni na kudhani kila kitu kinaenda kama kilivyoandikwa. Mimi siipendi Namibia kwasababu mara kadhaa nimeshuhudia matukio yao ya kinoko mno kutoka Immigration department.
Dah aisee hongera sana bingwa. Ni kama vile umejitoa katika tanuri la moto mkuu.Hapana nilirejea mda kuendelea na maisha hapa hapa tz
Ni kweli bangi zinaruhusiwa?Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.
Nianze kwa kusema kuwa dunia ina mengi, na kamwe hauwezi kuyajua kama haujaambiwa au kuyaona. Ndio maana waswahili wanamsemo wao unaosema "tembea uyaone". Hii haimaanishi kwamba utembee uyaone magorofa, magari au barabara, bali uone mambo mapya ambayo hapo kabla ya kutembea ulikuwa haujawahi kuyaona au kuyasikia popote.
Sasa leo ningependa nije na mada inayowatahadharisha ndugu zangu wabongo, ili kuwafungua macho na akili ya kujua yale ambayo hapo kabla walikuwa hawajayajua kuhusu South Africa, Dzonga, Afrika borwa, Afrika kusini, bondeni, Kaburu na kila jina linalotambulisha taifa hili.
Ni mambo sita tu ambayo ningependa kukutahadharisha nayo, uyazingatie kabla ya safari. Ila kama kuna mengine ya kuongezea basi wenzangu ambao wako humu pia wataongezea mengine katika comment. Na uzi wangu wa leo unajikita katika mambo yaliopo ndani ya mipaka ya South tu. Kuhusu changamoto zingine za njiani kabla ya kufika South nk, hizo sintozizungumzia kwa sasa. Maana thread za changamoto hizo zipo nyingi na mimi nishawahi kuandika moja.
Tuendelee hapo chini na yale unayotakiwa kuzingatia.
1. Hakikisha una document zote muhimu zinazohitajika safarini. Na kama uliambiwa kuwa gharama ya safari ni laki tatu, basi uandae angalau laki nne, ili moja uiweke pembeni itakusadia mbele ya safari. Kumbuka kuna dharura njiani, dola au rand kupanda nk.
2. Wakati unapanga safari, jitahidi kwanza ujue kingereza. Na kama una kichwa kizito cha kujifunza ngeli, basi upambane ujue hata salam, kuomba kitu au kuaga. South ni nchi inayoongea lugha 11. Ambapo lugha 9 ni za wenyeji na 2 za wazungu. Lakini lugha ya taifa na ambayo inapewa kipaumbele zaidi ni English.
Sasa ukijua English, hata kama hauna elimu ya maaana, uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa ukilinganisha na wale ambao hawajui English. Ndomaana wazimbabwe wamedhibiti kazi nyingi na haswa zinazomilikiwa na wazungu, maana wao English kwao ni kama maji na mtungi, halafu wanaongea British safi kuliko waafrika wengine. Kutokujua English kumewanyima watu wengi (haswa kutoka bongo) fursa za kazi, hivyo kusababisha wengine kuamua kufanya deal hatari, halali na zisizo halali ili mradi mtu aishi.
3. Kabla ya kuanza safari hakikisha una address au contacts za wenyeji wako zaidi ya mmoja. Nchi hii kuna watu wengi wameuwawa, wameibiwa, wamekamatwa na kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kukimbiwa au kuzimiwa simu na wenyeji wao kabla ya kuingia au baada ya kuingia South. Na hii sio kwa wabongo tu, bali ni nchi zote za East Africa watu wana tabia za kuwaingiza maboya ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba waje tu watawapokea na kuwafanyia mpango wa kuishi, lakini ndugu, jamaa au marafiki hao wanapoingia tu mwenyeji huzima simu, hubadili namba nk. Hivyo ukiwa na address au namba za sim zaidi ya 3, itakusaidia ku deal na mwingine baada ya mmoja au wawili wa mwanzo kukuzimia simu.
4. Usiwaze kwamba utafanya kazi fulani tu, bali wewe ujiandae kufanya kazi yoyote (ya halali) kujiingizia kipato. Hili swala la watu kuja huku wakiandaa akili, na saikolojia zao za kichwa kwamba anakuja kufanya kazi fulani tu. Ndio limesababisha baadhi ya wabongo kupoteza mwelekeo wa maisha, na kujikuta wanajitupa katika biashara hatari na zisizokuwa halali.
5. Usilete usela mavi usiokuwa na maana. Vijana wengi waliotaka kuleta usela wa Mbagala, Mburahati, Manzese, Temeke, Tandika nk tumewazika wakiwa bado wadogo. Hii ni kwa sababu huku watu hawana muda wa kukimbizana na mwizi wajichoshe. Ukileta usela mavi, watu wanakutafutia target, wanafumua ubongo, kazi imekwisha. yumbani watu wanarudisha nguo au maiti na kesi hamna. Pia usije kwa lengo la kutafuta na kufanya starehe kupitiliza mpaka ukasahau kilichokuleta. Maana kama starehe hata bongo zipo na umeziacha, kama mademu bongo wapo na umewaacha, kama tungi pia bongo lipo umeliacha. So focus kwa kile kilichokufanya utafute nauli uje. Sio kuendekeza kulewa na chupi za Kaburu utapotea mazima na hakuna mtu atakaekurudisha katika chanel yako tena.
6. Ukifika hapa kama wewe ni mpya usikimbilie kukaa kiti cha mbele katika daladala (tax), hata kama imejaa na imebaki siti moja ya mbele, ni bora usubiri nyingine alafu ndio upande. Hii ni kwa sababu huku majimbo mengi daladala zao hakuna kondakta anaezunguka ndani ya daladala kuomba nauli. So ukisema unakimbilia mbele kukaa na dereva, utashangaa watu wanakusanya hela zote huko nyuma, alaf wanakutupia wewe ndio uhesabu na kama kuna mtu ametoa hela kubwa umrudishie chenji, na ikiwa pungufu uhakikishe waliokupa wanazieneza. Dereva yeye hupokea nauli ambayo imeshahesabiwa tayari na iwe imetimia. Ikipungua hata sh hamsini basi ataanza na wewe uliepokea hela kabla ya kuendelea na waliopo ndani ya gari. Pia asilimia kubwa ya madereva wa hapa wana silaha mbali mbali ndani ya gari zao, kama sio bunduki basi fimbo inayofanana na mkia wa taa. So hela yake isipoenea na wewe ndo New comer (mpya) haujui lugha, basi imekula kwako. Hata ujitetee kwa English yako ya kuunga unga hatokuelewa. Naomba niishie hapa.
Jamaa ni mshamba sana. Kuna wabongo hatari wapo hadi kwenye systems za nchi jirani wanakula na wakuu wa huko. Wengine hadi NIDA za huko wanazo hawasumbuliwi.Huyu ni wale ambao wanasimuliwa na kujifanya wanajua kile walichosimuliwa. Wengine tushafanya kazi hadi katika maeneo ambayo mtu akihadisiwa anajiuliza uliwezaje wezaje kuipata kazi hiyo.
Kwa vile ndugu zetu wamekariri kuwa ili uishi hapa lazima uuze bangi, upige mchomoko au kuuza unga. Basi wenye akili tukipata mshtuo wa kazi za maana huwa tunapiga kimya kimya bila mbongo yoyote kujua.