Mkuu kwani kwa kiswahili chako neno kazi linamaana gani?
Unaposema South Africa hakuna kazi kwa foreigners huku ukikiri tena mwenyewe kuwa wazimbabwe (ambao ni foreigners) wana kazi za hovyo unamaanisha nini?
Je kama hizo kazi wanazofanya wazimbabwe zingekuwa za hovyo kama unavyojaribu kuaminisha watu, unafikiri wazawa wangeingia barabarani kuanzisha fujo na kudai kuwa wageni hasa wazimbabwe wanachukua kazi zao? Kuna vitu ambavyo ndugu zangu wabongo wengi hawavifahamu kuhusu hii country na mmoja wao ni wewe.
Let me tell you something that you don't know about it. Mwaka 2009 hadi 2015, nilikuwa nafanya kazi katika restaurant moja maarufu hapa SA inaitwa Spur, ipo ndani ya RandPark Ridge mbele ya Cresta jijini Johannesburg. Yani 98% ya wafanya kazi wa pale walikuwa wazimbabwe, huku mbongo nikiwa peke yangu na wazawa wa3. Waiters tulikuwa tunakunja R6500 ya kipindi kile kila mwezi, na keep change ambayo tulikuwa tunaachiwa na wazungu ndo ilikuwa kufuru. Mtu ulikuwa unaondoka na R400 au 500 kila siku, na weekends unaondoka mpaka na R800.
Wazimbabwe wengi walijenga kwao, walinunua mifugo, magari nk. Hata mimi pale ndo nilipopatia akili ya kununua kiwanja changu cha kwanza bongo na kuanza kujenga nyumba yangu ya kwanza. Mwaka 2015, nikarudi bongo kuweka mambo sawa, ila nilichelewa kurudi hivyo nafasi yangu kuchukuliwa na mtu mungine.
Sasa unaweza kuangalia mwenyewe kima cha mshahara wa R6500 plus R300 au 400 ya kila siku, kama una akili ya kuweka ukizijumlisha kwa mwezi unakuwa na bei gani? Ni Wa South wangapi ambao wanaweza kupata kima hicho cha pesa kila mwisho wa mwezi. Kuna msemo wa kiswahili unaosema kuwa usilolijua ni sawa na usiku wa giza. Hizi kazi watu wengi au naweza kusema wote kutoka East Africa hawazijui ndo maana wewe unaita eti kazi za hovyo. Maana hata mimi nilitafutiwa kazi hiyo na demu wangu wa kishona (mzimbabwe) ambae alikuwa ni manager pale Spur.
Hiyo ni moja kati ya kazi nyingi zinazowapa maisha wazimbabwe. Na sasa wamegeukia kwenye Uber, Bolt nk, huku wabongo tukiendelea kusimama kwenye kona za barabara kuuza vikete viwili vitatu vya bangi na hapo hapo wazee wapite uwaungie na kubaki na ela ya kula. Maisha hayo mtu utaishi mpaka lini?