Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Kama una mpango wa kuja South, zingatia mambo haya sita kabla ya kuanza safari yako

Habari zenu wanaJF wenzangu, ama baada ya salam ningependa kuendelea na mada yangu hapo chini.

Nianze kwa kusema kuwa dunia ina mengi, na kamwe hauwezi kuyajua kama haujaambiwa au kuyaona. Ndio maana waswahili wanamsemo wao unaosema "tembea uyaone". Hii haimaanishi kwamba utembee uyaone magorofa, magari au barabara, bali uone mambo mapya ambayo hapo kabla ya kutembea ulikuwa haujawahi kuyaona au kuyasikia popote.

Sasa leo ningependa nije na mada inayowatahadharisha ndugu zangu wabongo, ili kuwafungua macho na akili ya kujua yale ambayo hapo kabla walikuwa hawajayajua kuhusu South Africa, Dzonga, Afrika borwa, Afrika kusini, bondeni, Kaburu na kila jina linalotambulisha taifa hili.

Ni mambo sita tu ambayo ningependa kukutahadharisha nayo, uyazingatie kabla ya safari. Ila kama kuna mengine ya kuongezea basi wenzangu ambao wako humu pia wataongezea mengine katika comment. Na uzi wangu wa leo unajikita katika mambo yaliopo ndani ya mipaka ya South tu. Kuhusu changamoto zingine za njiani kabla ya kufika South nk, hizo sintozizungumzia kwa sasa. Maana thread za changamoto hizo zipo nyingi na mimi nishawahi kuandika moja.

Tuendelee hapo chini na yale unayotakiwa kuzingatia.

1. Hakikisha una document zote muhimu zinazohitajika safarini. Na kama uliambiwa kuwa gharama ya safari ni laki tatu, basi uandae angalau laki nne, ili moja uiweke pembeni itakusadia mbele ya safari. Kumbuka kuna dharura njiani, dola au rand kupanda nk.

2. Wakati unapanga safari, jitahidi kwanza ujue kingereza. Na kama una kichwa kizito cha kujifunza ngeli, basi upambane ujue hata salam, kuomba kitu au kuaga. South ni nchi inayoongea lugha 11. Ambapo lugha 9 ni za wenyeji na 2 za wazungu. Lakini lugha ya taifa na ambayo inapewa kipaumbele zaidi ni English.

Sasa ukijua English, hata kama hauna elimu ya maaana, uwezekano wa kupata kazi ni mkubwa ukilinganisha na wale ambao hawajui English. Ndomaana wazimbabwe wamedhibiti kazi nyingi na haswa zinazomilikiwa na wazungu, maana wao English kwao ni kama maji na mtungi, halafu wanaongea British safi kuliko waafrika wengine. Kutokujua English kumewanyima watu wengi (haswa kutoka bongo) fursa za kazi, hivyo kusababisha wengine kuamua kufanya deal hatari, halali na zisizo halali ili mradi mtu aishi.

3. Kabla ya kuanza safari hakikisha una address au contacts za wenyeji wako zaidi ya mmoja. Nchi hii kuna watu wengi wameuwawa, wameibiwa, wamekamatwa na kurudishwa nyumbani kwa sababu ya kukimbiwa au kuzimiwa simu na wenyeji wao kabla ya kuingia au baada ya kuingia South. Na hii sio kwa wabongo tu, bali ni nchi zote za East Africa watu wana tabia za kuwaingiza maboya ndugu, jamaa na marafiki zao kwamba waje tu watawapokea na kuwafanyia mpango wa kuishi, lakini ndugu, jamaa au marafiki hao wanapoingia tu mwenyeji huzima simu, hubadili namba nk. Hivyo ukiwa na address au namba za sim zaidi ya 3, itakusaidia ku deal na mwingine baada ya mmoja au wawili wa mwanzo kukuzimia simu.

4. Usiwaze kwamba utafanya kazi fulani tu, bali wewe ujiandae kufanya kazi yoyote (ya halali) kujiingizia kipato. Hili swala la watu kuja huku wakiandaa akili, na saikolojia zao za kichwa kwamba anakuja kufanya kazi fulani tu. Ndio limesababisha baadhi ya wabongo kupoteza mwelekeo wa maisha, na kujikuta wanajitupa katika biashara hatari na zisizokuwa halali.

5. Usilete usela mavi usiokuwa na maana. Vijana wengi waliotaka kuleta usela wa Mbagala, Mburahati, Manzese, Temeke, Tandika nk tumewazika wakiwa bado wadogo. Hii ni kwa sababu huku watu hawana muda wa kukimbizana na mwizi wajichoshe. Ukileta usela mavi, watu wanakutafutia target, wanafumua ubongo, kazi imekwisha. yumbani watu wanarudisha nguo au maiti na kesi hamna. Pia usije kwa lengo la kutafuta na kufanya starehe kupitiliza mpaka ukasahau kilichokuleta. Maana kama starehe hata bongo zipo na umeziacha, kama mademu bongo wapo na umewaacha, kama tungi pia bongo lipo umeliacha. So focus kwa kile kilichokufanya utafute nauli uje. Sio kuendekeza kulewa na chupi za Kaburu utapotea mazima na hakuna mtu atakaekurudisha katika chanel yako tena.

6. Ukifika hapa kama wewe ni mpya usikimbilie kukaa kiti cha mbele katika daladala (tax), hata kama imejaa na imebaki siti moja ya mbele, ni bora usubiri nyingine alafu ndio upande. Hii ni kwa sababu huku majimbo mengi daladala zao hakuna kondakta anaezunguka ndani ya daladala kuomba nauli. So ukisema unakimbilia mbele kukaa na dereva, utashangaa watu wanakusanya hela zote huko nyuma, alaf wanakutupia wewe ndio uhesabu na kama kuna mtu ametoa hela kubwa umrudishie chenji, na ikiwa pungufu uhakikishe waliokupa wanazieneza. Dereva yeye hupokea nauli ambayo imeshahesabiwa tayari na iwe imetimia. Ikipungua hata sh hamsini basi ataanza na wewe uliepokea hela kabla ya kuendelea na waliopo ndani ya gari. Pia asilimia kubwa ya madereva wa hapa wana silaha mbali mbali ndani ya gari zao, kama sio bunduki basi fimbo inayofanana na mkia wa taa. So hela yake isipoenea na wewe ndo New comer (mpya) haujui lugha, basi imekula kwako. Hata ujitetee kwa English yako ya kuunga unga hatokuelewa. Naomba niishie hapa.
Ndugu yangu domokeka alizamia huko miaka 15 iliyopita mpaka leo hatujawahi wasiliana nae. Sijui mzima au ashachinjwa. Maana na yeye aliendekeza sana usela mavi. Si unajua watoto wa tandale kwa tumbo tena!
 
Abiria wote ni makondakta unampa jirani yako nauli na unachukua chenji yako kama ipo, wa mwisho ambaye amekaa karibu ya dereva anamkabidhi dereva pesa kamili na ikipungua ni juu yako kufidia, vinginevyo utasurubiwa na dereva.
Huu ni ujinga wa kusululishana bila sababu ya msingi ingelikua huku bongo dereva wangelikua wanasikosa pesa zote kwa mfumo huu.
 
Anatoboa tena vizuri sana si Bora huyu hata anaweza kuweka sentence ikaeleweka Kuna wengi wanajua thank you na sorry na baada ya mda Wana master na maisha yanaendelea
SA kwa kingereza mtaani wana pidgin Yao ukiwa mwepesi ndani ya miezi 3 hakuna shida
Wale ambao hatupendi kuwa watumwa wa lugha za wakoloni ndo basi tena?
 
Na dunia iliyoendelea Ulaya na marekani hakuna conductor mkusanya hela ni unalipia kwenye mlango kwa driver kwa kadi au cash japo wengi ni kwa card tena unakuta ni ya mwezi mzima (kama kwenye train au hizo bus za town ) hii ya konda na abiria ni huku kwetu
Ni mfumo wa zamani sana ndo unaotumika kwetu. Lakini sometimes naelewa. Nchi zetu bado hazijaendelea. Watu wengi wanategemea usafiri wa umma ambao kuupanda kwake tu ni kwa fujo, kubanana na kujaza kupita kiasi ili kila mmoja awahi anapokwenda hasa makazini asubuhi, na nyumbani jioni.

Ukiwawekea ustaarab wa huku wa kujikusanyia hela wenyewe, inamaana wengi hawatolipa na dereva hatoweza kujua idadi ya waliopanda daladala. Maana ni mwendo wa kugombania, kubanana nk.
 
Sio msimuliaji mzuri ila mleta mada kafafanua Yale Yale yaliyonipa changamoto mfano hela nilichukua kidogo sana
Documents zilinisaidia sana maana Musina nilikamatwa
Border ya Zambia waliambia hujui kingereza na unaenda SA!?
Nikiwa cape town nilipanda tax nikakaa mbele same situation ikatokea na driver akaniuliza "are you new in town!?"huku akicheka akanipa hiyo knowledge aliyotoa mleta mada
Labda kuongezea ni usitembee usiku na kuwa na mahusiano hovyo hovyo
Are you new in town🤣🤣😂 unabaki unakodoa macho
 
Ndugu yangu domokeka alizamia huko miaka 15 iliyopita mpaka leo hatujawahi wasiliana nae. Sijui mzima au ashachinjwa. Maana na yeye aliendekeza sana usela mavi. Si unajua watoto wa tandale kwa tumbo tena!
Inawezekana akawa ashakufa, yupo jela au mtaani ila kapoteza na kuacha kuwasiliana na familia. Kama yupo hai basi kuna siku tu utapata habari zake.
 
Naskia wazulu ndio wakurya wa south africa wanapenda fujo na ubabe balaa
Wakurya ni watoto wadogo sana mbele ya hawa jamaa. Wakurya wanafujo za mmoja mmoja hasa akikukuta raia ni mnyonge. Ila wakurya hawana ujanja wa kulianzisha kupambana na serikali.

Ila hawa jamaa tukianza kwenye historia mfalme wao Shaka Zulu ndio aliekuwa na nguvu kuliko mfalme yoyote katika nchi zote za kusini mwa Afrika. Aliwahenyesha wazungu mpaka wakaja na style ya kioo 🤣🤣🤣 (kweli mzungu noma)

Wazulu chini ya uongozi wa Shaka Zulu walitembeza kipigo kwa kila aliekuwa sio mzulu mpaka ikapelekea wangoni kusambaratika wengine wakakimbilia Tanzania, wengine wakakimbilia Malawi, wengine Zambia nk. Kama hiyo haitoshi wakavamia mpaka Msumbiji tena mji mkuu maputo wakateka watu na kwenda kuwafanya watumwa wao na wengine kuwazalisha. Kama hiyo haitoshi wakatembeza kipigo kwa jamii nyingine iliyokuwa karibu yao hadi jamii hiyo ikakimbilia katika eneo ambalo leo hii ndio linaitwa Swaziland.

Kama hiyo haitoshi wakatembeza kipigo tena kwa jamii nyingine ya Ndebele hadi jamii hiyo ikakimbilia Zimbabwe na kuanzisha makazi na kuwa kabila rasmi la Zimbabwe. Hapa hapa tu walianzisha fujo mwaka 2019, baada ya raisi mstaafu ambae ni wa kabila lao kukamatwa. Fujo hiyo ilikuwa kubwa hadi kupelekea kutumwa jeshi la taifa kuingilia kati baada ya vyombo vyote vya ulinzi kushindwa kuwatuliza.

Sasa kabila la namna hiyo unawezaje kulifananisha na wakurya ambao hawana historia yoyote. Leo hii popote utapokwenda iwe nchi yoyote ya Afrika, Ulaya au Marekani ukiuliza kuhusu makabila ya South kila mtu atakutajia wazulu. Jamaa wanashika mila zao balaa, wana umoja balaa. Fikiria wana mpaka dini yao ya shembe na inatambulika kitaifa. Sometimes mpaka viongozi wa kitaifa ambao ni kabila lao na imani yao huudhuria ibada zao mchana kweupe.
 
Aisee chief natamani ungekuwa unanipa hii story live maana kuandika kunachosha ...hio story ya shaka zulu na wazungu kutumia staili ya kioo iko vipi maana sijaielewa
 
Back
Top Bottom